Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 29 November 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 66....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Mnamo mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Sedekia alikwenda Babuloni pamoja na ofisa wa askari wake aitwaye Seraya mwana wa Neria na mjukuu wa Maseya. Kutokana na fursa hiyo mimi Yeremia nilimpa Seraya ujumbe.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Nilikuwa nimeandika kitabuni maafa yote niliyotangaza juu ya Babuloni na pia maneno mengine kuhusu Babuloni. Nilimwambia Seraya: “Utakapofika Babuloni ni lazima uwasomee wote ujumbe huu. Kisha umalizie na maneno haya: ‘Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa hata pasikaliwe na kiumbe chochote, mwanadamu au mnyama, na kwamba nchi hii itakuwa jangwa milele.’
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Utakapomaliza kusoma kitabu hiki, kifungie jiwe, kisha ukitumbukize katikati ya mto Eufrate, ukisema: ‘Hivi ndivyo mji wa Babuloni utakavyozama, wala hautainuka tena, kwa sababu ya maafa ambayo Mwenyezi-Mungu anauletea.’” Mwisho wa maneno ya Yeremia.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Ibada ya uongo na ya kweli
1Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Mbingu ni kiti changu cha enzi,
dunia ni kiti cha kuwekea miguu yangu.
Mtanijengea nyumba ya namna gani basi,
Mahali nitakapoweza kupumzika?
2Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote,
na hivi vyote ni mali yangu.
Lakini ninachojali mimi
ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto,
mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.
3“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka:
Wananitolea tambiko ya ng'ombe
na mara wanaua watu kutambikia.
Wananitolea sadaka ya mwanakondoo
na pia wanamvunja mbwa shingo.
Wananitolea tambiko ya nafaka
na pia kupeleka damu ya nguruwe.
Wanachoma ubani mbele yangu
na kwenda kuabudu miungu ya uongo.
Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.
4Basi, nitawaletea taabu;
yatawapata yaleyale wanayoyahofia;
maana nilipoita hakuna aliyeitika,
niliponena hawakusikiliza.
Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu,
walichagua yale ambayo hayanipendezi.”
Adhabu na wokovu
5Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,
enyi msikiao neno lake mkatetemeka:
“Ndugu zenu ambao wanawachukia,
na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu,
wamesema kwa dharau
‘Mungu na aoneshe utukufu wake,
nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’
Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
6Sikilizeni, ghasia kutoka mjini,
sauti kutoka hekaluni!
Hiyo ni sauti ya Mwenyezi-Mungu
akiwaadhibu maadui zake!
7 66:7 Taz Ufu 12:5 “Mji wangu mtakatifu,
ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu;
kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto.
8Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo?
Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo?
Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja?
Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja?
Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu,
alijifungua watoto wake.
9Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe,
halafu niwazuie wasizaliwe?
Au mimi mwenye kuwajalia watoto,
nitafunga kizazi chao?
Mimi Mungu wenu nimesema.”
10Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda!
Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!
11Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha,
nanyi mtashiba kwa riziki zake;
mtakunywa shibe yenu na kufurahi,
kutokana na wingi wa fahari yake.
12Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nitakuletea fanaka nyingi kama mto,
utajiri wa mataifa kama mto uliofurika.
Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga,
mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.
13Kama mama amtulizavyo mwanawe,
kadhalika nami nitawatuliza;
mtatulizwa mjini Yerusalemu.
14Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi;
mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi.
Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu,
lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”
15Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto,
na magari yake ya vita ni kimbunga.
Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali,
na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.
16Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto,
atawaadhibu watu wote kwa upanga;
nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
17Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wapo watu wanaojitakasa na kutawadha wapate kuingia kwenye bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu. Watu hao hakika watakufa wote pamoja. 18Nayajua matendo yao na mawazo yao. Naja kuwakusanya watu wa mataifa yote na lugha zote, wajumuike pamoja na kuuona utukufu wangu. 19Nitaweka kati yao alama ya uwezo wangu. Watakaosalimika kati yao nitawapeleka kwa watu wa mataifa huko Tarshishi, Puti,66:19 Puti: Kiebrania: Puli. Ludi, nchi zenye wapiga upinde stadi; watakwenda pia Tubali na Yowani na nchi ambapo watu hawajapata kusikia umaarufu wangu wala kuuona utukufu wangu. Hao wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo. 20Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu. 21Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
22“Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumba
zitakavyodumu milele kwa uwezo wangu,
ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.
23Katika kila sikukuu ya mwezi mpya,
na katika kila siku ya Sabato,
binadamu wote watakuja kuniabudu.
Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
24“Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”


Isaya66;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: