Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 29 May 2015

ZIARA YA MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI JIJINI TEHRAN TAREHE 24 - 27 MEI 2015











Maadhimisho ya SIKU YA AFRIKA yafanyika Washington DC


Balozi wa Misri nchini Marekani Mhe. Mohamed Tawfik akiongea kufungua sherehe ya African Union iliyofanyika siku ya Alhamisi May 28, 2015 katika hotel ya JW Marriott, Washington DC
Balozi wa Morocco nchini Marekani Mhe. Rashad Bouhlal akiongea machahce.
Msemaji mkuu wa sherehe ya siku ya Afrika Mhe. Donald Tetelbaum.
Mchungaji Jesse Jackson akiongea kwenye sherehe ya siku ya Afrika.


Maureen Umeh mfanyakazi wa kituo cha luninga cha Fox News DC akisherehesha sherehe ya siku ya Afrika.



Mambalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba.
Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Githae.

Thursday 28 May 2015

MISA YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA KUFANYIKA JUMAMOSI MAY 30, 2015


MZEE SAMUEL NTAMBALA LUANGISA

Familia ya Marehemu Mzee Luangisa na New York Tanzania Community, inawakaribisha kwenye MISA ya kumuaga Marehemu Mzee wetu, Baba yetu na Kiongozi wetu Mzee Samuel Ntambala Luangisa (83), kabla ya kwenda Bukoba kwa mazishi Siku Jumamosi MAY 30th, 2015
kuanzia Saa: 1pm - 5pm

Address: LEE'S Funeral Home L.L.C
160 Fisher Avenue
White Plains, NY 10606

Baada ya Misa sote tutajumuika nyumbani kwa Wafia The Luangisa Residence: 

374 Hawthorne Terrace, 
Mt. Vernon, NY 10552

Mpe taarifa mwenzako wote karibuni. 

Kwa taarifa zaidi wasikiana na:

1. Prof. K. Lwiza 631-273-3859
2. Dr. Abas Byabusha 914-584-7502
3. Shabani Mseba 347-712-8539
4. Hajj Khamis 347-623-8965

Ukitaka kutoa rambirambi yako unaweza kutumia number hizi hapa chini.
Luangisa na Kwame Luangisa. Bank ni Bank of America. Account# 9504210977. Routing# 021000322. Swift code ni BOFAUS3N. 

Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake la Bwana litukuzwe. Amen!

Monday 25 May 2015

UPENDO NKONE, MIKE KALAMBAY WANOGESHA TAMASHA LA GOSPEL COLUMBUS, OHIO


Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Columbus, Ohio Enock Mwamba(kati) akiimba moja ya nyimbo za injili huku akiwashirikisha Mike Kalambay aliyekuja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Upendo Nkone aliyekuja toka Tanzania maalum kunogesha tamasha la Gospel lililofanyika siku Jumapili May 24, 2015 na kuhitimisha tamasha hilo lililokua la siku 3 mjini humo lililoanzia siku ya Ijumaa May 22, 2015.
Mike Kalambay akiimba huku akitoa neno la Mungu kwa Kifaransa kilichochanganyika na lingala huku mchungaji Fayes (kulia) akitafsiri kwa kiingereza na Kiswahili.
Mike Kalambay akiimba moja ya nyimbo za injili kwenye tamasha la gospel lililofanyika siku ya Jumapili May 24, 2015 mjini Columbus, Ohio.
Mike Kalambay toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akishambulia jukwaa na nyimbo za injili.
Mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake kwenye tamasha hilo.
Upendo Nkone na mchungaji Donis Nkone wakifuatilia tamasha Mike Kalambay (hayupo pichani).
Mchungaji Donis Nkone na mke wake Nnunu Nkone wakiwa wamepiga magoti wakati Mike Kalambay akiwashukuru kwa kufanikisha ujio wake ikiwa ndio mara ya kwanza kwa yeye kufika mjini humo.
Mike Kalambay(kati) akipata picha ya pamoja na mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone mara tu baada ya kumalizika kwa tamasha hilo lililovuta watu mbalimbali wa mataifa tofauti mjini Columbus, Ohio.