Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 20 August 2013

Afya Na Jamii;TATIZO LA MIFUPA AU KUUMWA MIGUU/MAGOTI: OSTEOPOROSIS:


Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi. Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.
Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa. Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi aba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume. Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.
NINI CHA KUFANYA
1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umriu mepiga hatua
2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza
3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani)
4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua)
VIRUTUBISHI
Kwa ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubishi ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu.
Virutubishi vifuatavyo vimewasaidia wengi wenye tatizo hili.
1. Calcium
2. Chitosan
3. Lycopen



KUKOSEKANA KWA UTE KATIKATI YA VIUNGO (JOINTS) - CARTILAGE

Kajiraba fulani ambako hujulikana kwa jina la kitaalamu kama “Cartilage” (katileji) ambako hupatikana katikati ya mifupa. Kuna kitu fulani huwa kinapatikana katikati ya mifupa miwili ya goti la mnyama (ng’ombe, mbuzi) huwa wengi wanapenda kukila kwenye baada ya kuchemshwa au kupikwa. Kama unaijua hii, basi ndio katileji yenyewe.
Katileji inasaidia kuikinga mifupa isiumie.Vilevile inafanya kazi ya kusaidia kuubeba uzito wakati wa kutembea, kuinama, kunyoosha viungo au kukimbia.
Zaidi ya asilimia 85 (85%) ya katileji ni maji, na jinsi umri unavyosonga mbele, maji hayo huwa yana kawaida ya kupungua. Na asilimia 15 niprotini.
Tatizo hili lipo zaidi kwenye sehemu ya magoti. Endapo katileji inakuwa ina tatizo, husababisha maumivu makali hasa unapotaka kusimama au kutembea, vile vile kwenye mabega, au nyonga. Pia inaweza sababisha uvimbe (goti au nyonga au bega kuvimba).
Mtu ambaye katileji yake ina tatizo aidha imelika au kutokuwepo kabisa, anatakiwa kupatiwa vitu au virutubishi ambayo vitasaidia kuirekebisha katileji au kuijaza kwa upya.
Virutubishi vifuatavyo vimesaidia wengi wenye tatizo hili:
1. Shark Cartilage
2. Calcium
3. Chitosan

OFISI ZETU ZIPO karibu na huduma zifuatazo:
1. Ofisiya TRA, au karibu na
2. Afya Dispensary, au karibu na
3. Mjasiriamali kwanza, au karibu na
4. Kanisa la Sabato au karibu na
5. Kanisa la Lutherani au karibu na
6. Uwanja wa mpira wa Mwenge.

Anaye hitaji ufafanuzi zaidi tuwasiliane: 0715 594 564 au 0756 594 564

Au tembelea website yetu www.1000ufahamu.com

12 comments:

Interestedtips said...

Asante kwa elimu hii, afya njema na muhimu sana kwenye maisha yetu

Rachel Siwa said...

Nikweli kabisa da'Ester.Karibu.

Unknown said...

Asante, lkn mimi nina miaka 31 na miguu inaniuma kwenye kisigino, itakua ninini?

Rachel Siwa said...

pole sana si uhakika ni nini lakini jaribu kuvaa viatu vyenye kisigino kidogo..
epuka kuvaa high heels na p
flat zili kama unakanyaga chini kabisa..

Unknown said...

Habari zenu humu. Naomba msaada wenu miye nimekuwa nasumbuliwa na matatizo ya mifupa tangu mdogo.nikiambiwa na sickle cell.baadae nimekuja kupima tena na vipimo vyote vya matatizo ya mifupa naonekana sina kitu lakini silali vizuri kutembeya kwangu naumiya miguu magoti mgongo nishida kwangu naombeni ushauri wenu nini nifanye

Rachel Siwa said...

salama mpendwa,
pole sana ,
unaweza kuwasiliana nao kupitia hizo namba hapo juu.

Unknown said...

Habari? Mimi nipo Arusha. Nikihitaji huduma yenu naweza kuwapata huku?


Anonymous said...

Kiukweli mm ninatatizo hilo nahitaji msaada

Unknown said...

Jamani naombeni msaada ,mwanangu anamwaka sasa ,lkn mpaka sasa hakai,alafu shingo haiko imara sana,,nimeomba ushauri ,wakaniambia nitumie calcium, ambayo ndo nimeanza kutumia,je anaweza akawa na shida gani,maana mwonekano ana afya nzuri na hajawahi kuacha kuongeza kilo.

Unknown said...

Naomba msaada wenu,goti linauma hasa wakati wakuchuchumaa na nikikaa chini kuinuka linuuma

Unknown said...

Naomba msaada wenu,goti linauma hasa wakati wakuchuchumaa na nikikaa chini kuinuka linuuma

Unknown said...

naomba ushauri wenu mtoto wangu anaumwa magoti sana na visigino hadi kutembelea amebadilisha kutembea pia ana umri wa miaka 11 tu