Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 31 August 2014

Natumaini JumaPili Inaendelea Vyema;Burudani-Jamaican Gospel...!!!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu Jumapili ilikuwa/inaendelea Vyema,Indelee kuwa na Amani,Upendo,Unyenyekuvu,Furaha na Upole kiasi....Basi ,mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo;mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi,bali nipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu;2;Naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhani ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya kimwili 3; Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4;[Maana silaha za vita vyetu  si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;]
Neno La Leo;2Wakorintho 10:1-18
5;Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukitekanyara kila fikira ipate kumtii Kristo 6;Tena  tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia. 7;Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu.Mtu akijitumainia mwenyewe yakuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake,Ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo,vivyo hivyo sisi 8;Maana, ninapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yenu,[tuliyopewa na Bwana,tupate kuwajenga wala si kuwaangusha],sitatahayarika; 9;Nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa  nyaraka zangu.......................

17;Lakini, yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana. 18;Maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye, bali yeye asifuwaye na Bwana.

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe wote.

Wednesday 27 August 2014

Wanawake Na Mitindo;[Natural Hair]Nywele zisisowekwa dawa[Chukuchuku]

Waungwa;Wanawake na Urembo,Mitindo..Sikuhizi Wanawake/Kinadada wengi wameamua kurudi/kubaki kwenye Nywele zao za Asili... [Chukuchuku]Wengine hawaweki Dawa wala kusukia Nywele Bandia.Na wengine wanaongezea "Madoido"   kidogo ili kupendezesha Nywele hizo, Wengine wanasuka na kuongezea nywele bandia kidogo lakini hawaendi mbali saana na mitindo ya Kizamani/yakina Mama..Lakini wote wanapendeza tuu..

Jee wewe ni mpenzi wa mitindo hii?
Jee ni kuishiwa/kukosa ubunifu wa mitindo mipya?

Jee kuchoshwa na Mitindo hiyo au kuna/ina  Madhara kiafya?kwa mitindo na Urembo zaidi tufuate huku;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/
 "Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima

Sunday 24 August 2014

Tumalizie JumaPili hii Kwa Amani na Baraka;Burudani-Angalia baba,Pamoja na Wewe-Elisha Muliri!!!!!!!

Natumaini Jumjapili hii ilikuwa Njema,Mungu azidi Kuwabariki,Kuwa na Imani,Kusifu,Kuabudu,Kushukuru na Kutukuza...
Akaanza kufundisha tena kando ya bahari.Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno,hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini,mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari.2;Akawafundisha mambo mengi kwa mifano,akawaambia katika mafundisho yake.
Neno La Leo;Marko Mtakatifu4:1-40
3;Sikilizeni;Tazama mpanzi alitoka kwenda kupanda;4;Ikawa alipokuwa akipanda, Mbegu nyingine  ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila.5;Nyingine ikaanguka penye mwamba,Pasipokuwa na udongo mwingi,;Mara ikaota kwakuwa na udongo hapa;6;Hata jua lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina mizizi ikanyauka.7;Nyingine ikaanguka penye miiba;Ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.8;Nyingine zikaanguka penye udongo ulio  mzuri,zikazaa matunda,Zikimea na kukua, na  kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia.9;Akasema, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie.


Mfano Wa Mpanzi:1-9


Shabaha Ya Mifano:10-13[Mat13:10-17[Luka:8:9-10]


Yesu anafafanua mfano wa Mpanzi:13-20[Mat 13:18-23][Luka 8:11-15]

Taa iliyofunikwa:21-25[Luka 8:16-18]

Mfano wa Mbegu inayoota:26-29

Mfano wa Mbegu ya Haradali:30-34[Mat 13:31-32,34][Luka 13:18-19]


Yesu anaamuru dhoruba itulie:35-40[Mat 8:23-27][Luka 8:22-25]
"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Tuesday 19 August 2014

[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV‏


Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano

Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.

Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.

Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014.

Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Mazungumzo na Salma Moshi kuhusu uchaguzi DMV‏
 Salma Moshi akizungumza na Mubelwa Bandio kwenye mahojiano haya


Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.

Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.

Mmoja wa wagombea hao, Salma Moshi amaketi nasi kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014 chini ya utayarishaji wa Vijimambo Blog


Karibu uungane nasi kusikia anachopinga

 
 

Wednesday 13 August 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan‏JhikoMan akitumbuiza kwenye Tamasha la Majahazi 2013
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a
JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Helsinki Finland mwishoni mwa mwezi Julai

Amezungumza
mengi kuhusu ziara yake ya Ulaya iliyoanza mwezi wa nne, maonyesho
aliyofanya, kazi alizorekodi na pia watu aliowashirikisha kwenye albamu
yake mpya ijayo.

Amezungumzia IMANI ya RASTA na pia MUZIKI WA TANZANIA kwa ujumla

Ameongea mengi mema

KARIBU UJIUNGE NASI


Tuesday 12 August 2014

Pitapita ya Mswahili mitaani;Mtu Kwao.!!!!!!!Tulikutana na hili bango mitaani hapa UK,kuona Bendera ya Kwetu,"Tanzania" Tukavutiwa..
Nyumbani Kwetu ni Kuzuri,Watu wa Kwetu ni Wakarimu..Karibuni Tanzania Karibuni Mtwara. Mambo Ipo Huko!!!!!!!
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima

Hotuba fupi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank kwa DIASPORA‏


Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Charles Singili alipokuwa akizungumzia huduma za benki yake kwa waTanzania jijini Washington DC
PICHA ZOTE KWA HISANI YA IKULU
Hotuba fupi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Charles Singili alipokutana na waTanzania waishio nchini Marekani usiku wa Agosti 2, 2014.

Hotuba hii ilitolewa kwenye mkutano kati ya waTanzania wa Marekani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Jakaya Kikwete

Karibu umsikilize
Monday 11 August 2014

CITE SUMMER CONFERENCE 2014 COVENTRY WEST MIDLANDS UK WITH MWL.MWAKASEGE.[Tujikumbushe Picha za Mkutano na Mchungaji Daniel Kulola,Uliofanyika Coventry]Picha hizi za chini ni mkutano wa zamani kidogo na Mchungaji Daniel Kulola,Ulifanyika Coventry UK.
Si vibaya tukijikumbusha.....Picha kutoka Maktaba ya Swahili Na Waswahili

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday 10 August 2014

Muendelee na JumaPili hii kwa Amani na Upendo;Burudani-Franck Mulaja,Alleluya,Nzambe malamu..!!!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu Jumapili inaendelea vyema;Iwe yenye Imani,Kuomba pasipo kukoma,Uponyaji,Shukrani na kujitoa kwa wenye kuhitaji.

14.Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao,15. Mara mkutano wote walipomuona walishangaa, Wakamwendea mbio,wakamsalimu.16.Akawauliza, Mnajadiliana nini nao?

Neno La Leo;Marko Mtakatifu:9:1-50

17.Mtu mmoja katika mkutano akaijibu,Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako,ana pepo bubu;18. Na kila  ampagaapo,humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda;Nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.19.Akawajibu,akasema,Enyi kizazi kisichoamini,nikae nanyi hata lini?Nichukuliane nanyi hata lini?Mleteni kwangu.20.Wakamleta kwake;hata alipomwona,mara yule pepo alimtia kifafa;naye akaanguka chini,akagaagaa,akitokwa na povu.

21.Akamuuliza babaye,Amepatwa na haya tangu lini?Akasema tangu utoto.22.Na mara nyingi amemtupa katika moto,na katika maji,amwangamize;Lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia.

23.Yesu akamwambia, Ukiweza!Yote yawezekana kwake aaminie."Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Saturday 9 August 2014

Chaguo La Mswahili Leo;Mary Mary - Shackles,Get Up,In The Morning,Shackles,Haven,Go Get It...!!!!!!!!

Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo; ni Mary Mary..kitambo kidogo na sasa..zipi zinakubamba/kuzipenda..zamani au sasa au zooote?
Nisikuchoshe..Twende Sote sasa......

>


"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima

Thursday 7 August 2014

Hotuba ya Mhe Rais Uhuru Kenyatta kwa waKenya Washington DC. Aug 6, 2014‏


Mhe. Rais Uhuru Kenyatta akihutubia waKenya jijini Washington Aug 6, 2014
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Uhuru Kenyatta alipozungumza na waKenya usiku wa Agosti 6, 2014 kwenye hotel ya Marriott Wardman Park Hotel, jijini Washington DC nchini Marekani.

Mahojiano na mgombea urais wa jumuia DMV, Liberatus Mwang'ombe‏


Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Liberatus Mwang'ombe.
Mgombea uRais wa Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia
Uchaguzi unategemewa kufanyika Agosti 9, 2014

Wednesday 6 August 2014

Kipindi cha Maswali na Majibu kati ya Rais Kikwete na waTanzania, Washington DC‏


Mhe. Rais Dk Jakaya Kikwete akijibu maswali ya waTanzania
Usiku wa Agosti 2, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete alikutana na waTanzania katika hoteli ya Marriot jijini Washington DC

Baada ya hotuba yake, Mhe. Rais aliruhusu maswali kutoka kwa waTanzania hao

Na haya, ndiyo yaliyoulizwa kwake.

Karibu


Tuesday 5 August 2014

Hotuba Ya Mhe Rais Jakaya Kikwete Kwa WaTanzania Washington DC. Aug 2, 2014‏
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani.
Monday 4 August 2014

Ujumbe wa Leo; kutoka kwa kaka Boniface Ole Precious "Msakatonge"


MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA..


1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhari mwanangu usimuache huyo!

2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!

3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!

4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa!

5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!

6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!

7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!

8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!

9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.

10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.

11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.

12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.

13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.

14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga kama wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.

15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!

16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.

17. Mwanangu, nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.

18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.

19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!

20. NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU. NAKUPENDA!

Ujumbe huu umeandaliwa na Boniface Ole Precious "Msakatonge" Ametoa ruhusa ya ku-share na marafiki.

Shukrani;https://www.facebook.com/SautiYaMwanamke/timeline

Sunday 3 August 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani-Living Water Worship Team Yesu U Mwema,Sifa ni kwako,Yehova Mwenye Nguvu Zote..!!!!!!!!


Wapendwa;Nawatakia Jumapili Njema Yenye Kusifu,Kuabudu,Kutukuza,Kushukuru,Kuwa na Matumaini na Kupendana......
5.Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,6.Na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7. Na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.....


Neno La Leo;Waraka Wa Pili Wa Petro;1:1-21

19.Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vema, mpaka kutakapo pambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.20.Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu furani tu.21.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa MUNGU,Wakiongozwa na roho mtakatifu.


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima

Friday 1 August 2014

Siku Kama Ya Leo da'Rachelsiwa Alizaliwa;[Happy birthday]Namshukuru MUNGU kwa kila Jambo!!!!!!!

Wapendwa/Waungwana,Siku Kama Ya Leo mimi "Rachel siwa"Nilizaliwa.Namshukuru sana MUNGU wangu kwa yote aliyonitendea/anayonitendea...Yeye ni mwingi wa Rehema,Neema,Baraka,Upendo.Yeye ni kila kitu maishani mwangu..
Nawashukuru Sana Wazazi/Walezi wangu kwa malezi na yote mliyonitendea kulingana na uwezo wenu,Nathamini sana mchango wenu,Kwani malezi yenu hayana mwisho kwangu.
Namshukuru sana Mume wangu katika yote,Tangu pale tulipokutana/tulipotoka mpaka sasa tulipo na tunapoelekea ni kwa Uwezo wa MUNGU tutafika salama.
Niwashukuru sana Watoto wangu wote,wale wa kuwazaa na wakurithi , kwa Faraja,Heshima,Upendo na mengineyo..Najivunia kuwa MAMA.
Nawashukuru sana Dada,Kaka,Mawifi,Mashemeji,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu wote wanaonifahamu kwa namnamoja au nyingine..Nawapenda Wote.MUNGU azidi kuwabariki na kuwaongezea kila lililo jema.
Asante sana kwa wote walioniletea zawadi,wanaoniombea,walionitumia ujumbe na mnaondelea kuniombea...MUNGUazidi kuwa Bariki na kuwatendea....Asanteni Sana kwa kunisoma  na MUNGU awabariki Sana.

"Swahili Na Swahili" Pamoja Sana.