Saturday 31 March 2012
Chaguo la Mswahili Leo,mambo ya Taarab-Utalijua Jiji!
Friday 30 March 2012
Thursday 29 March 2012
MAZISHI YA MAREHEMU DENIS OSWALD KAPINGA
Ndg. Joseph Oswald Kapinga
Ndugu Joseph Kapinga pichani hapo juu anapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwa Ratiba ya mazishi ya mpendwa mdogo wetu Denis O. Kapinga yatafanyika leo Tarehe 29/03/2012 katika makaburi ya Sinza karibu na ukumbi wa mwika.
Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:
Mwili wa marehemu utafika Nyumbani maeneo ya Sinza karibu na New White Inn Bar bara bara ya Sinza uzuri mnamo saa 6.00 Mchana kutoka Hospitali ya Mwananyamala.
Mwili utaagwa nyumbani saa 7.00 Mchana na baadae utapelekwa kanisa la Roman Catholic Sinza kwa Ibada.
Baada ya hapo Saa 8.30 Mchana mwili wa marehemu utapelekwa Makaburi ya Sinza kwenye nyumba yake ya milele.
"BWANA ALITOA NA BWANA
Poleni sana Familia ya Kapinga.
Swahili na Waswahili tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu kwenu.
Mungu awatie Nguvu.
Ulale kwa Amani kaka Denis.O.Kapinga.
Poleni sana Familia ya Kapinga.
Swahili na Waswahili tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu kwenu.
Mungu awatie Nguvu.
Ulale kwa Amani kaka Denis.O.Kapinga.
Tuesday 27 March 2012
Jikoni Leo-Ni kwa Mama Mwakitalu!!!Pata na Burudani ya Ngoma!!!!![Mwanamke jiko au Mwaume Jiko?]
Da'Masika/mama Mwakitalu |
Mboga za Majani Mchanganyiko,Majani ya Kunde na Majani ya Maboga |
Mchuzi wa Samaki Umeungwa/wekwa Nazi na nyanyachungu |
Maandaziiiiii na hapo chini ni Mahindi ya Kuchemsha.
Kwani Utamu/Radha ya chakula wewe unaweza kupendezwa nacho na mwingine asipendezwe nacho.
Jee Kazi/Ujuzi wa Kupika ni kwa Wanawake tuu?Kwani mara nyingi utasikia Mwanamke jiko na si Mwanaume Jiko,Hasa kwa Maisha ya Leo,
kwa Maisha ya Zamani wengi wao Mama/Dada kazi yao kubwa ni Upishi na Baba wengi ndiyo walikuwa wanafanya Kazi hasa Mijini, Kwa Vijijini Woote BABA na MAMA Wanaenda shambani lakini Kupika ni MAMA.Jee Leo Tunaweza Thubutu kusema MWANAUME JIKO? AU TUTAKUA TUMEWADHALILISHA?Kwani wapo Wanakarangiza haswaaaa kutushinda au Hamjakutana nao?.
Karibuni Waumgwana kwa Mawazo na Kuelimisha na Kwa upendo.
MWAKILISHI WA UNOPS NCHINI SIERA LEONE NDUGU OMARY MJENGA AKISALIMIANA NA RAIS KIKWETE WAKATI WA MAZISHI YA MKUU WA WILAYA YA LIWALE MAREHEMU VICTOR P. CHIWILE JANA KIBAHA.
Mmoja wa waombolezaji akimsalimia Rais Kikwete kwa kuibusi Pete yake, kulia ni Ndugu Omary Mjenga akishuhudia tukio hilo.
Rais akisalimiana na Ndugu Omary Mjenga jana walipokutana kwenye mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale.
Ndugu Mjenga alikuwa Personal Secretary wa Rais Kikwete wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje kabla hajawa Rais.
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante Sana.
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante Sana.
Sunday 25 March 2012
Saturday 24 March 2012
Chaguo la Mswahili Leo-Twanga Pepeta - Mtu Pesa na nyingine nyingi!!!
Wednesday 21 March 2012
Waswahili na Maisha Yao - Zanzibar na Mwaka Kogwa Festiva-Burudani Marashi ya Pemba!!
Karibuni sana Waungwa!!
Sunday 18 March 2012
J'Pili ya leo ni Maombi kwa Wajane,Yatima , Wenye shida na Tabu; Kabula anasema Dhihirisha na Upendo anasema Hapa Nilipo!!!!!!!
Neno la leo;Matendo ya Mitume:9;36-43.Na Mwanafunzi mmoja alikuwa Yafa Jina lake Tabitha,Tafsiri yake ni Dorkasi[yaani Paa];Mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.Endelea na Uwe na wakati mwema.
Saturday 17 March 2012
Thursday 15 March 2012
Mswahili Wetu Leo; DR. SHABANI KACHUA MTANZANIA ANAEIPEPERUSHA VEMA BENDERA YA TANZANIA NCHINI CANADA
Dr. Engineer Shabani G Kachua akijiandaa kuingia kwenye Professional Engineer Induction Ceremony nchini Canada
Hapa Dr. Kachua akionyesha moja ya Nishani aliyotunukiwa siku hiyo
Dr Kachua akiwa amesimama kwa nyuma na Mainjinia wenzake
Akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu na mainjinia wenzake.
Kwa niaba ya Watanzania ninapenda kukupongeza kwa kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania.
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.http://kapingaz.blogspot.com/
Ahsante sana.
Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.http://kapingaz.blogspot.com/
Ahsante sana.
Wednesday 14 March 2012
Watoto na Urembo,Wanapaka Shedoooooo!!!!!!
Wazazi/Walezi hapo vipi?Kuna msemo sikuhizi; Aku babu najiremba mie napishana na Uzee!Nao Watoto sasa;Aku bibi nakufuata hukohuko!!Mambo ya kileo hayo, Zamani ulikuwa huruhusiwi kupaka,Wanja,Poda na vipodozi vingine, mpaka siku ya KUOLEWA!!Eti ukipaka kabla,Siku ya Arusi hautapendeza!!Na walikuwa Wakisuka Nywele Ufunge kilemba mpaka MUMEO kwanza Aone!!''Hizi hadithi mie nazisikia''.Hahahahahha Ohiiii Leo hii nani umfungishe Kilemba?Tena ukienda salon ndiyo unafunga kilemba kama nywele zimeharibika, ukimaliza tuu kilemba kuleeee,Wataanza kuona kina baba/mama John,Juma,Neema,Pili na mnaopishana Njiani, hee dada wewe Umependeza, Umetoka Chicha na..Nani kakusuka dada mmoja anaitwa YASINTA NGONYANI!!!Muwe na Wakati Mwema Waungwa, Karibu Sana sana.
Tuesday 13 March 2012
Wanawake na Mitindo ya Nywele,Pata na kideo Jinsi ya kuweka Nywele Bandia!!!!!!
Haya Waungwana Mitindo ya Nywele kwa Wanawake, Mmmh lakini kwa sasa hakuna cha Wanaume wala cha Wanawake, kila mmoja anajaribu kuingilia Mitindo ya Jinsia nyingine,Au labda mimi ndiyo sielewi, kwamba hakuna Mitindo ya Wanawake na Wanaume Wote ni Sawa!!!!Wewe uliyepita hapa unaonaje?
Swali ;Wanaume wengi Wanaofanya Kazi SALON zA Wanawake Wengi wao/Baadhi yao ni MASHOGA?
Swali ;Wanaume wengi Wanaofanya Kazi SALON zA Wanawake Wengi wao/Baadhi yao ni MASHOGA?
Monday 12 March 2012
Sunday 11 March 2012
Nawatakia j'Pili Njema Wapendwa,Burudani,Rose Muhando-Tamalaki''Na nyingine Mpya!!
Saturday 10 March 2012
Wanawake na Mitindo-da'Levina na Rafiki zake!! Chaguo la Mswahili-Yvonne Chaka - Mamaland na Umgombothi
Dadazzz mmependeza mnoo,Asanteni sana kwa kutuwakilisha.Siku ya Wanawake ,Wao walijumuika na wenzao kwa Shamim.Duuhh kivazi cha kanga kikitengenezwa, kinapendeza haswaaa.Wanawatakia Wanawake Woote Duniani ,Baraka, Amani,Upendo na Umoja.WANAWAKE JUU!!!
Friday 9 March 2012
Thursday 8 March 2012
Nawatakia kheri na Baraka, Wanawake wote!!Burudani,Vicky Kamata - Wanawake Maendeleo
Tuesday 6 March 2012
Kaka Farid atimiza miaka 14-Ona mambo yake!!!
Poziii
Mpirani
Shughulika baba!!!!
Vituko
Mapenzi kwa mama.
Hongera sana kaka Faridi kwa kutimiza miaka 14,Mungu akubariki na kukulinda wakati wote.
Uwe baraka kwa wazazi na watu wote.
Hongera pia Wazazi na Mungu awape Maarifa, Usimamizi na Mema Yote kwenye Malezi.
Waungwana; Eti watoto Wengi wa Kiume ni rafiki/wapo karibu sana na MAMA kuliko BABA?
Pamoja Wapendwa!!
Mpirani
Shughulika baba!!!!
Vituko
Mapenzi kwa mama.
Hongera sana kaka Faridi kwa kutimiza miaka 14,Mungu akubariki na kukulinda wakati wote.
Uwe baraka kwa wazazi na watu wote.
Hongera pia Wazazi na Mungu awape Maarifa, Usimamizi na Mema Yote kwenye Malezi.
Waungwana; Eti watoto Wengi wa Kiume ni rafiki/wapo karibu sana na MAMA kuliko BABA?
Pamoja Wapendwa!!
Monday 5 March 2012
Wanawake na Mitindo Leo-Da'SUBIRA WAHURE DESIGNS!!!!!!
Da'Subira anaomba wenye mapenzi mema,wamsaidie kufikisha Ujumbe huu.
Hizo ndizo kazi afanyazo.
Ukitaka kumfahamu zaidi ingia.http://www.subirawahure.blogspot
Ukitaka kumfahamu zaidi ingia.http://www.subirawahure.blogspot
Hongera sana da'Subira,Kazi nzuri na Mungu akubariki kwa kazi zaMikono yako!!
Sunday 4 March 2012
Saturday 3 March 2012
Chaguo la Mswahili Leo-Ngoma & Kidumbak na Ahmada Umelewaaaa!!
Subscribe to:
Posts (Atom)