Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 8 March 2012

Nawatakia kheri na Baraka, Wanawake wote!!Burudani,Vicky Kamata - Wanawake Maendeleo


Namshukuru Mungu kwa kuniumba  Mwanamke,Najivunia kuwa Mwanamke!Nawatakia Wanawake wenzangu woote Kheri,Baraka,Upendo,Utuwema,Fadhili na Yootee yanayostahili.Wanawake Tujiheshimu na Kuheshimu Wengine,Tupendane na Tujipende,Tushirikianae na Kuelimishana,Tusamehe nasi Tusamehewe.Wanawake wa Zamani hata akiwa mama wa Nyumbani lakini alikuwa anakitu kidogo cha kufanya,kama, Kusuka ukili,Kufuma vitambaa,Biashara ndogo ndogo,Kushona na mambo meengi ili kuongezea kipato.Hata Wanawake wa sasa hatuja chelewa, kama hakuna Ajira basi Tunaweza Kusjishughulisha,hakuna asiyeweza kufanya lolote na hakuna aliye zaliwa anaweza.Japo masoko yamekuwa magumu,lakini Tusikate Tamaa.Pale tunapokwama tusisite kutafuta Ushauri na maelekezo, Kwani kuuliza si Ujinga.Mungu awabariki sana,WANAWAKE JUUU!!!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo, tena kabisa wanawake tunaweza. Hongera sana nawe pia na mimi na yule au nisema woteeeeeee..Wanawake na maendelee tufanya kazi tusonge mbele ..yeleee yeeellee haya hapo eeehh ehee..mmhh mpaka jasho wakati kunabaridi hapa leo:-)

Simon Kitururu said...

Hongereni sana yani!Na nimependa picha yako!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongereni wanawake popote mlipo. Bila ninyi kusingekuwa na jamii. Mbarikiwe sana !!!

emuthree said...

Hongereni sana, lakini nauliza hivi ipo siku ya wanaume duniani, au TZ....Au siku nyingine zote zilizobaki ndizo za wanaume, mbona kupendelea...wanawake siku moja, sita wanaume au?

Mija Shija Sayi said...

Hahahahahahahhhh EMU-3 tangu nikujue leo umeongea neno!!

Haya bwana Rachel naona unazidi kuwa kimodo. Umependeza ile mbaya.

Hongera mwanamke.

Rachel Siwa said...

Ahsante sana kwa niaba ya Wanawake wote!@ ndugu wa mimi emu-3 tehtehteh.
@ da'Mija asante tunajaribu kupishana na Uzee!!!