Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 18 April 2012

Jikoni Leo ni Kakazzz,Burudani-Tmk wanaume family - Dar mpaka moro!!!!!!

Kina kaka walioandaa huu msosi.
Kachumbari

Samaki au dagaa?
vipi hapo ugali utaisha?
Mimi nafikiri mboga za leo mwenzake Nguna/Ugali,Jee mwenzangu?
Mboga ya Majani. Jee ukishiba utashushia na nini?

Waungwana Wanaume Leo ndiyo waliotuandalia Chakula,
Kumbe wakiamua wanaweza,Huko nyuma tulijadili kuhusu ''WANAUME NA JIKO'',Kaka S. [Sam mwana wa  Mbogo]Alielezea vyema sana, Hasa yeye anavyohusika Jikoni.Pia akasema Wanawake wengi wakisaidiwa huwa Wanatabia ya Kujisahau.


Kaka zangu hawa nao wanasema wao hupenda kujipikia zaidi kuliko kupikiwa.


Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?.


Jee wewe Mwenzangu una Maoni,Ushauri Gani? Pamoja sana!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi chitaki bwana ww kila chiku kutamanishana tu..na unajua mie mdhaifu wa chamaki:-(

Mija Shija Sayi said...

Inakuwa vipi hadi leo wanajipikia? Ni swali tu..

emu-three said...

Nasikia njaa kweli kweli....tupo pamoja ndugu wa mimi

Rachel Siwa said...

Ohh pole chana mama Erik mimi nitapikia wewe chamaki nchanga eeh!!!

da'Mija hawana wenza/Wake,sijui bado wapowapo au wanachugua sana!!

Ndugu ya mimi polee si muda maharage yataiva utakula ndugu yangu.Pamoja sana sana.

Mija Shija Sayi said...

Nanukuu..
"Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?."

Nami ngoja niulize kulingana na swali.."Kwani nafasi ya mwanamke ni ipi katika ndoa..Je ni kupika na kufanya kazi za ndani? au kwa maana nyingine ni kwa nini hasa mwanaume huamua kuoa?

Wanaume tungependa majibu yenu zaidi hapa...

Anonymous said...

It's an remarkable article for all the online people; they will get advantage from it I am sure.
Visit my weblog online roulette for money