Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 30 April 2013

Unazikumbuka hizi?,Mtoto wetu[Everyone's Child],Neria na Nyingine-[kwa Kiswahili]!!!!

Waungwana;Filamu/Hadithi hizi na Nyingine ni zamuda.lakini mimi bado nazipenda na nipatapo muda huwa nazirudia...
Yaani zina mafundisho na Mifano/Yaliyotokea/Yanayoendelea Kutokea katika   Maisha ya kweli katika Jamii.

  Kuna lolote unakumbuka,kukugusa,kukutokea wewe au mtu wa karibu,Kusikia Jee?
       
   
kuona Zaidi ingia;swahiliwood

             "Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.

Monday 29 April 2013

Jikoni Leo;Mchele Mmoja mapishi Tofauti!!!


Waungwana;"Jikoni Leo"Mchele mmoja Mapishi Tofauti...Kazi kwako wewe Mpishi.
   "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 28 April 2013

Muwe Na J'Pili yenye Neema na Imani;Burudani-Rebecca Malope!!!!!!!!

 Wapendwa;Natumaini J'Pili inaendelea vyema...
Muwe na Amani,Baraka,Furaha na Tumaini...

 Upendano wa ndugu na udumu.[2]Msisahau kuwafadhili wageni;maana kwa njia hii wengine wamekaribisha malaika pasipo kujua.
Neno La Leo:Waraka kwa Waebrania:13:1-6..Hata twathubutu kusema BWANA ndiye anisaidiaye,sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?

           "Swahili NA Waswahili" Neema na iwe nanyi Wote.

Saturday 27 April 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Boyz II Men - On Bended Knee,I Swear,Mama na Nyingine!!!!!!!


Waungwana; Chaguo La Mswahili Leo..Mambo ya.. Boyz 2 Men.... Thank you in Advance, On Bended Knee, A song for MAMA ..................... na Nyinginee....
Mhhh palikuwa hapatoshi...Vipi wewe kuna lolote unakumbuka ukisikia/kuangalia nyimbo hizi...Wapi na Nini?

  "Swahili Na Waswahili"  Zilipendwa/Zinapendwa...J'Mosi Njema.

Thursday 25 April 2013

Mitindo Nga'mbo;Fashion Sense TV!!!!!!!Waungwana, Walioko/Wanaoishi Nga'mbo  Baadhi ya Maeneo Jua limeanzaa..watu watapungua uzito kwa Makoti..hahahhaha.. ...
Vipi wewe hapo ulipo? 
haya niwakati wa kuzunguka zunguka Mjini , Nyama Choma, Kupeleka/Kucheza na Watoto Park na Mengine meengi..Raha tupu!!!


 Na Mitindo ndiyo hiyo Madukani..................."Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima

Wanawake na Mitindo Ya Nywele..mitindo inajirudia!!!

Waungwana;Mitindo mingi sasa naona inarudi, kama unavyoona Rasta kubwa sasa zimerudi tena...

Jee kukumbuka zilizopendwa au Tumeishiwa Ubunifu?

Mimi bado nazipenda sanaa tuu..Vipi wewe?


Mitindo zaidi ingia;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk
     "Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 17 April 2013

Ulale kwa Amani Fatuma Binti Baraka -Bi KIDUDE!!!!!

Fatuma Binti Baraka[Bi KIDUDE] Amefariki.

Pole kwa Familia,Ndugu,Jamaa,Wasanii,Wapenzi na Wa TANZANIA Wote...
Na Apumzike kwa Amani bi Kidude.

"Swahili NA Waswahili" pamoja Daima.

Watoto na Vipaji;Botlahle - Winner Of South Africa's Talent!!


Waungwana ;"Watoto na Malezi"Leo tuangalie Vipaji vya watoto Wetu...
Vipi utagundua mtoto wako anakipaji gani?

 Jee Unakubaliana na Mtoto wako nini anapenda kwa Mfano;Michezo,Kushona,Kutengeneza/Ubunifu,Kucheza Ngoma/Muziki,Kusuka,Kuchora na Mingine mingi...
Pasipo kumkatisha Tamaa kwasababu wewe hupendi hicho afanyacho na Ungependa Afanye unacho Penda wewe?

Karibu kwa Maoni/Ushaurina Kuelimishana kwa Upendo.

 Mengi kuhusiana na Watoto ingia;http://watotonajamii.blogspot.co.uk/

    "Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Tuesday 16 April 2013

Yanayo endelea Facebook;Mwalimu Ndondole na Wengine...Jee Wewe Unasemaje?


NAMHOFIA MWANANGU... NAIHOFUA KAZI YANGU... NALIHOFIA TAIFA LANGU...... HASA PALE MBUNGE NA WAZILI WANAPOONA BANGI INAWEZA KUWA HALALI KULIMWA (MAANA YAKE NA MATUMIZI YAKE)

HIVI TANZANIA IMEKOSA VITEGAUCHUMI NA RASLIMALI KIASI CHA KUIFIKILI BANGI KAMA ZAO LA KUONGEZA KIPATO....?

MADHARA YA BANGI YANAPOFANANISHWA NA YALE YA SIGARA KUNA UELEWA HAPO?
HAWA NDIO VIONGOZI WETU WANAOFIKIRI KWA KINA KWA NIABA YETU...?

WANAJUA KWANINI WATU WANAFIKIA HATUA YA KUVUTA BHANGI.....?

BINAFSI NAOGOPA...........................................................?

 • Edgar Joel Naunga mkono hoja tunapoteza mapato mengi sana wakati watu wengi wanatumia na ina soko kubwa sana tungepata mapato mengi endapo ingetozwa kodi .
 • Leon Mhongole uwezo wa kufikiri wa wabunge wetu umeshuka sana inatishia maisha ya vizazi vijavyo..
 • Lusungu Ndondole Natamani watoto wa yule mbunge, waziri na Edgar Joel wawe wa kwanza kuanza kutumia hii kitu. Lakini nawaswas na UZALENDO WAO na KAMA WANA WATOTO........ Najiridhisha kwa KAZI ZAO haziwapi fursa ya KUTAFAKARI zaidi ya KUFIKIRI....
 • Lusungu Ndondole Bwana Leon Mhongole, sie wenye WATOTO, UZALENDO na IMANI............ ndio TUNAOTAFAKARI mpaka kufikia tulikofikia. Usiogope ni KAZI zao na MAKUZI yao yanawapotosha...
 • Edgar Joel Mi nilimwelewa sana Mbunge Lusungu Ndondole unajua tumbaku ina madhara makubwa sana na ni sumu lakini imeruhusiwa kwanini bangi nayo isiruhusiwe tafakari na jua kuwa inatumika sana sasa na watu wa rika lote sasa jiulize je tumepoteza vipi mapato..
 • Edwin Mvanda Nadhani watawala washalichoka taifa hili. Wanataka baadae tuwe na taifa lenye vichaa watupu.
 • Kukaye Moto hiyo ndio dawa ya vifua vikuu hamkujua nini hahahaahaha hapa ulaya inauzwa bei sana, karibu nchi zote zimeruhusu ..watu wananunua hapa madukani..Usiogope..acha watu wapate ajila zao kama zao lina kubali ..hiyo sio hatari kama kodi itakusanywa vizuri..Rushwa ni hatari kupita kajani hako
  16 hours ago · Edited · Like · 1
 • Jane Mkini Acha mbwembwe wewe mbona tumbaku inalimwa akat mshaambiwa ni hatari kwa afya zenu!!!!!!!!! Acha tu iruhusiwe hiyo bange ili kama kutatokea nginjanginja basi wajingawajinga wote tufe wabaki wenye akili zao labda kutajengwa taifa lenye usawa na haki.......
  7 hours ago · Like · 1
 • Lusungu Ndondole Dada Jane Mkini Hujaisoma POST sawasawa, kwa uwezo wako wa kutafakari watakaokufa ni wajinga au wavutabangi? Ndio maana nimeuliza UNAFANANISHA MADHARA YA BANGE NA YALE YA SIGARA? Fikiri tena na UTAFAKARI.
 • Lusungu Ndondole Shemeji yangu Kukaye Moto, najua we ni ADIKT WA UZUNGU ndio maana sishangai mchango wako.
 • Lusungu Ndondole Nina maswali muhimu kwa Kukaye Moto, UNAFANANISHA ULAYA NA TANZANIA? We umetokea pale Ipogoro, najua fika unaijua TZ vizuri, UNADIRIKI KUITAFAKARI TANZANIA KWA KUILINGANISHA NA UINGEREZA AU UJERUMANI? Vijana wa kitanzania wapo sawa KIELIMU, KIPATO, UTA...See More
 • Edwin Mvanda Watu hawajui, unapokua na vichaa na mateja wengi ndipo hata wewe uliye na kazi yako unakua katika risk zaidi. Vibaka wakizidi utapolwa na wala hutakua salama. Kwa sasa wafanyakazi wote wanalipa kodi pamoja na ya wote wasio na kazi. Yaani wewe uliyeajil...See More
  15 minutes ago · Like · 1
 • Lusungu Ndondole Kwa maswali yangu hayo kama UNAWATAKIA MEMA wanyalukolo wenzio huku utafikiri UPYA na KUTAFAKARI shemeji yangu Kukaye Moto. Huo UZUNGU ndio ULIOWAHARIBU hata viongozi wetu wakienda ulaya wanarudi wanafikiri na KUWAZA KIULAYA wakidhani watu wote wa TZ wameshafikia kiwango cha
 • Edwin Mvanda Ubinafsi utatuua. Huyu anayetetea bangi ananikumbusha hasira za popo anapokua mtini kalala. Popo anaposikia kishindo cha kitu kinapita chini hupatwa na hasira na hatua ambayo huchukua ni kutoa kinyesi ili kimfikie aliye chini ambaye anahisi ni adui yake, sasa anasahau kua kalala miguu juu kichwa chini ndipo hapo mwili mzima huloa mavi yake mwenyewe. Hivi ndivo tunataka kufanya tunapotetea bangi. Watch out guys.
 • Lusungu Ndondole Sawa kabisa kaka Edwin Mvanda. Tatizo la kuathiriwa na UZUNGU ndilo linalowatesa hata viongozi wetu wengi wakienda semina ULAYA na AMERIKA wakirudi WANAFIKIRI KIZUNGU na KUWAZA KIZUNGU ndio maana wanalopoka tuu wakidhani wote wamefikia MAENDELEO, MAHITAJI, MTAZAMO na MALENGO ya KIMAREKANI wamesahau kama wao wanawaongoza WAFRIKA ambao wengi bado HAWAJAFIKIA KIWANGO WANACHOWAFIKIRIA badala yake walitakiwa WATAFAKARI kwanza.

Like ·              Maoni/Ushauri,Nyongeza......
 Karibuni Sana na Tuelimishane Kwa Upendo.
                                                      "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
 ·