Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 26 February 2015

MAWAZIRI WA NCHI TANO AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON,DC NCHINI MAREKANI


Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo  uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  Balozi   Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu  MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi, 

Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James  Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi  Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi  MFA & IT Kenya, Bi.  Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir  PA to CS MEACT Kenya.

Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred  Nwam na Stilson  Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.


Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika siku ya Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.


Ujumbe wa Tanzania


Ujumbe wa Burundi


Ujumbe wa Kenya


Ujumbe wa Uganda na Rwanda


Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Wednesday 25 February 2015

Maisha;Ndoa Na Wanandoa-Majuto ni Mjukuu.!!!!!


Kijana Joseph ambaye sasa ni
marehemu,enzi za uhai wake
alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla
ya kuoa.
Baada ya kuoa miaka mitano ya
kwanza akabahatika kuwa na watoto
mapacha wa kike na wa kiume na
mke wake aliishi kwa furaha
akifurahia baraka ambazo Mungu
aliwapa familia ile.
Mke hakuwa na kazi na mme akaona
ni vyema amsaidie kwa kumsajilia
kampuni na mama yule akawa na
kampuni ya mitindo na ikafana sana
na kupata umaarufu katika eneo lile.
Miaka michache baadae baadae mme
akapatwa na matatizo kazini na
kusimamishwa kazi na kwa kuwa
alikuwa daktari basi na leseni yake
ya udaktari ikafungiwa na
hakutakiwa kufanya kazi yoyote.
Mpango huo ulisukwa na wenzake
pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana
kwa utendaji wa kazi zake na
kupinga vitendo vya rushwa.
Maisha yakazidi kuwa mabaya pale
nyumbani kwani miaka ilivyosogea
hakupata tena wala kuliona lile
penzi la mkewe, kwani mke akawa ni
mtu wa kumchukia mmewe mara
mme akihitaji fedha apewe kwa
masimango na mbaya zaidi hata
watoto wakaanza kufundishwa na
mama yao kumchukia baba yao.
Hali ile ilimpa mzee yule wakati
mgumu na ikafikia kipindi akaanza
kudhohofika mwili kwa mawazo
ingawa akajitahidi sana
kutoyaonesha hayo machoni pa
watu na majirani.
Baada ya muda akapatwa na homa
na akawa akijiuguza lakini baada ya
muda akashauriwa aende akapimwe
na kugundulika kuwa alikuwa na
tatizo katika moyo wake
lililosababishwa na msongamano wa
mawazo.
Akamfuata mkewe ofisini kwake na
kumwambia anatatizo la moyo na
ilihitajika apate msaada wa fedha
kiasi cha laki tano (500,000) ili
afanyiwe upasuaji wa haraka na
kujiokoa katika hali hiyo hatarishi
kwa maisha yake.
Mke alimjibu, " Sidhani kama nina
hela ya kuchezea kwa kukupa
mwanaume usiye na faida kwa
familia yako... yaani mpaka chupi
nikununulie mimi?Wanaume
wenzako wanafanya kazi na sio kama
wewe ulivyo sasa"
Baba alinyanyuka na kuufuata
mlango bila ya kusema neno machozi
yakimtoka na akikumbuka jinsi
alivyoijenga familia yake kwa upendo
na amani akiwapa mahitaji yote na
jinsi alivyotumia mpaka tone lake la
mwisho la fedha, muda na hata
jasho kuinyanyua biashara ya mkewe
ambayo ni kwa ajili ya familia.
Akawasha gari na kuondoka kuelekea
nyumbani akiwa na mawazo huku
akiona jinsi mtu umpendaye
anayoweza kubadilika kiasi cha
kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa
huna kazi na kumfananisha na wale
wote.
Huku nyuma mke akaingiwa na roho
ya ubinadamu na na kujilaumu kwa
kauli ile na kuanza kuumia kisha
akajaribu kumpigia simu mzee ikawa
haipokelewi na kumka kuliwasha gari
na kuanza kumfuata mzee
Kilomita chache mbele akaona kuna
mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki
gari na kuuliza kuna nini?
wakamwambia kuna ajali ya gari
kuna mzee alikuwa anataka kuingia
upande wa kushoto bila kuona kama
kuna gari.
Kusogea pale hakuamini kuona mwili
wa mme wake ukiwa umefunikwa
alianza kutokwa na machozi kabla
ya kuingia kwenye gari na kuona
kuna kadi nzuri ikiwa kwenye
bahasha akaifungua na kuisoma.
Kilio kikubwa kilimtoka baada ya
kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni
siku za kuzaliwa ya baba huyo na
hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye
mzee kununua kadi iliyoandkiwa "
NAKUSHUKURU MUNGU KWA
KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA
PAMOJA NA CHANGAMOTO
NINAZOZIPITIA NAAMINI KUNA SOMO
WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI.
UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH
DAY TO ME"
Mama yule aliomboleza na mpaka
sasa anazidi kuomboleza na hana
amani tena hata faida ya ile
biashara haioni tena na hajui nani
atamsamehe.
Je, unapitia mapito gani sasa katika
mahusiano yako?
Je, unayamudu vipi matatizo ya
mahusiano yako?
Je, unafikiria nini kama siku ukiamka
na kuona wewe ndio chanzo cha
kifo, kilema au chanzo msongamano
wa mawazo kwa mwenza wako
kutokana na tabia zako za ubinafsi?
Ndugu una kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa kukupa
mwenza huyo na kuamini kuwa
katika kila mnalolipitia ni jaribu la
kuwafanya muwe na sababu ya
kuonyeshana upendo vyema zaidi ya
ule wa mwanzo;
Nimeumia sana mpaka nimefikiria
sana mahusiano yangu na watu
wanaonizunguka,
kupitia stori hii nimepata somo la
upendo na uvumilivu na kuzishinda
stress za dunia.

"Nimetumiwa na Rafiki nami nikaona ni vyema tusome wote"
 "Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Monday 23 February 2015

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi....Sehemu ya mwisho


Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE

Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi

Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha

Na katika sehemu hii ya nne na ya mwisho ya mazungumzo yetu, Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea

1:Tukio la ugaidi la Septemba 11, 2001  - walivyopata taarifa (kama wanadiplomasia), na kilichofuata

2: Jukumu la kukuza mwanya wa biashara kati ya Marekani na Afrika, ambalo lilisababisha kupitishwa kwa muswada wa sheria wa AGOA

3: Siku yake ya kawaida kama Balozi inavyokuwa na alizimudu vipi?

4: Kituo chake kipya cha kazi huko Abu Dhabi Julai 2002

5: Utata juu ya wajibu wa ofisi za ubalozi kwa wananchi wake

6: Maisha baada ya kustaafu

7: Kazi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC)

8: Nani alioshirikiana  na kuhusiana nao kwa urahisi zaidi

9: Maisha yake ya kisiasa na BUSARA ZAKE

KARIBU

Kama ulikosa sehemu za awali, unaweza kuangalia Sehemu ya kwanza hapa, sehemu ya pili hapa na sehemu ya tatu hapa

Sunday 15 February 2015

Wapendwa natumai Jumapili inaendelea vyema;Tumshukuru/nina mshukuru sana Mungu;Burudani-Kijitonyama,Amenitendea na...!!!!!!


Wapendwa/Waungwana, Nimatumaini yangu Jumapili hii inaendelea/Imekuwa njema kwenu..
Bila shaka mmemaliza juma/ wiki hii vyema na mmejiandaa vyema kwa Juma/wiki lijalo.
Mimi nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa mengi sana aliyonitendea na anayoendelea kunitendea,
Mungu amekuwa nami katika yote...
Sina budi ya kuzidi kumtukuza na kumrudishia utukufu kwake..
Ndugu yangu Mungu anatenda Bwana..usikate tamaa wala usife moyo..kama si leo kesho utapokea tuu..
Tena kwa Mungu hakuna Rangi,Kabila,Mfupi/Mrefu,Haijalishi umetokea wapi/Taifa gani,Kila kitu kina sababu yake.
Yeye akisema ndiyo nani aseme hapana/siyo?
Anaweza kukuweka sehemu ambayo hukutegemea akakuchanganya na watu usiowajua vyema mila/Tamaduni zao.
Lakini yeye akiona panakufaa basi mtaelewana/kuendana/vyema.
 Mtaishi kwa Upendo,Furaha,Amani,Umoja na kuheshimiana.
Na hapo kuna mengi ya kujifunza,kila mmoja atajifunza ya mwingine.
Sasa utabeba unaloliona linafaa kwako na lisilo na manufaa/faida,Ulazima utayaacha hapohapo....
Mungu amempa kila mtu karama yake...Tumuombe sana Mungu azidi kutupa maono/ndoto.
Asante pia kwa siku hii...nilikuwa nina kibarua/nafanya kazi sehemu...
wakati/muda aliyonipa Mungu kufanya kazi/kuwa na wapendwa hawa umekwisha..
Nikasema kwaherini..ilikuwa ni vigumu sana kusema kwaherini...lakini kila jambo lina mwanzo na mwisho
Mwisho wake ulifika.Maisha lazima yaendelee..
Niliwapenda/Nitaendelea kuwapenda..
Kuna mengi nimejifunza kupitia wapendwa/waungwana hawa...
japo nilikuwa mweusi/mwafrika peke yangu lakini sikuwa mpweke.
Nina imani Mungu aliniweka hapo kwa sababu zake.
Ninamshukuru sana Mungu wangu nanimeuona utukufu wake..
G.H.Mkae salama na Mungu azidi kuwabariki.


Thank god for this day i was working somewhere, 
the  time god has given me to work with these lovely people has come to and end 
it was hard for me  to say goodbye 
but everything has a begging and an end 
i loved them and i always will 
i have learned lots from them 
i was the only one from africa, however  i was not alone becuse they showed me such love that ive never witnessed before
i know god put me there for a reason 
i thank God  i have seen the amazing things he can do, 
and i would like to say thank you so much to these amazing people from GH
Stay safe and ppeaceful may God bless you !! 

 3Je, huyu si yule seremala, mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?” Basi, wakawa na mashaka naye.







Neno La Leo;Marko:6:1-53
Yesu anakataliwa huko Nazareti
(Mat 13:53-58; Luka 4:16-30)
1Yesu aliondoka hapo akaenda katika kijiji chake, akifuatwa na wanafunzi wake. 2Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya? 3Je, huyu si yule seremala, mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?” Basi, wakawa na mashaka naye. 4Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.” 5Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya. 6Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao.

Bible Society of Tanzania





"Swahili Na Waswahili"Nawapenda wote.

Friday 13 February 2015

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi Pt II


Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE

Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi

Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha

Tunaendelea na sehemu ya pili ya mazungumzo yetu, ambapo Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea namna

1: Alivyoingia kwenye siasa (ubunge mwaka 1970)

2: Alivyopata taarifa za kwanza za uteuzi wake serikalini. Hapa napo pana mvuto wake kusikiliza.

3: Nafasi alizoshika kama naibu waziri na waziri kamili

4: Nafasi ya ukuu wa mkoa

5: Na hata harakati zake na pia alivyopata nafasi ya kuja kusoma Chuo Kikuu Havard

KARIBU

Kama ulikosa sehemu ya kwanza ya mazungumzo yetu, bonyeza READ MORE



Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Tuesday 10 February 2015

Tanzanian Dentist Dr. Talib Ali on the TOP Doctors Interviews - Sedation Dentistry


Dr. Talib Ali, a top dentist from Avatar Dental Care in Leesburg, Virginia, discusses the benefits of Sedation Dentistry on the TOP Doctors Interviews which are seen on CNN Headline News, CNBC, FOX News and other networks. Call Avatar Dental Care Today and set your consultation with Dr. Talib Ali at 703-669-8600 or visit http://www.avatardental.com/ or his office at:

Avatar Dental Care

545 G. East Market Street

Leesburg, VA 20176

Wednesday 4 February 2015

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi (Pt 1)


Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE

Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha

Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea

1: Historia yake.

 2: Aliposoma na alivyosoma.

 3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)

 4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.

 KARIBU

Sunday 1 February 2015

Muendelee na Jumapili hii Vyema;Burudani Na Dan Em-Halleluyah,Tunakuabudu na...!!!


Wapendwa/Waungwana Muendelee na Jumapili hii vyema,Muwe na Amani,Baraka,Upendo,Tumaini,Hekima na Busara..
Tusifu na Kuabudu..!!!!

1Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma. 2Katika vita walivyokuwa wakipigana na Israeli, Waaramu walikuwa wamemchukua msichana mmoja mdogo kutoka Israeli, naye akawa anamtumikia mke wa Naamani. 
Neno La Leo 2Wafalme:5:1-27
Naamani aponywa

 3Siku moja akamwambia bibi yake, mke wa Naamani, “Laiti bwana wangu angekwenda na kumwona yule nabii aliyeko Samaria! Angemponya ugonjwa wake.” 4Naamani alipopata habari hizi, akaenda kwa mfalme na kumweleza habari za mtoto huyu. 5Mfalme wa Aramu akamwambia, “Chukua barua hii umpelekee mfalme wa Israeli.”Hivyo Naamani akaondoka, huku amechukua vipande 30,000 vya fedha, vipande 6,000 vya dhahabu na mavazi kumi ya sikukuu. 6Barua yenyewe iliandikwa hivi,
“Barua hii ni ya kumtambulisha kwako ofisa wangu Naamani. Nataka umtibu huu ugonjwa wake.”
7Mfalme wa Israeli aliposoma barua hii alirarua mavazi yake na kusema, “Mbona mfalme wa Aramu anataka nimtibu mtu huyu ukoma wake? Kwani anafikiri mimi ni Mungu aliye na uwezo wa kuua au kufufua? Fahamuni basi, mwone ya kwamba mtu huyu anataka kuniletea mzozo.” 8Elisha, nabii wa Mungu, alipopata habari kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, alituma ujumbe kwa mfalme, akamwuliza, “Mbona umeyararua mavazi yako? Mlete mtu huyo kwangu, ili apate kujua kwamba kuna nabii katika Israeli?” 9Naamani akaenda na farasi wake na gari lake mpaka mlangoni mwa Elisha. 10Elisha akamtuma mtumishi wake amwambie, “Nenda ukaoge mara saba mtoni Yordani, nawe utapona kabisa.” 11Lakini Naamani alikasirika sana, akaenda zake akisema, “Nilidhani kwamba hakika atanijia na kumwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya mahali ninapougua na kuniponya! 12Isitoshe, je, mito Abana na Farpari ya huko Damasko si bora kuliko mito yote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga humo na kupona?” Akaondoka na kurudi nyumbani, huku amekasirika sana. 13Watumishi wake wakamwendea na kumwambia, “Baba yetu kama nabii angekuambia ufanye jambo fulani gumu, je, hungelifanya? Sasa, aliyokuambia tu ni: ‘Jioshe, ili upone!’” 14Basi, Naamani akateremka mtoni Yordani akajitumbukiza humo mara saba, kama alivyoagizwa na Elisha mtu wa Mungu, naye akapona kabisa. Ngozi yake ikawa imara na yenye afya kama ya mtoto mdogo. 15Ndipo akarudi kwa mtu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu yeyote ila tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafadhali sasa upokee zawadi za mtumishi wako.” 16Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.”Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa. 
Bible Society of Tanzania




"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.