Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 23 June 2013

NawatakiaJ'Pili Njema Yenye Amani;Burudani-Bahati Bukuku



Wapendwa ;Muwe na J'Pili yenye Baraka,Amani,Upendo na Shukrani....
Maandalio ya moyo ni ya mwanandamu;Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huzipima roho za watu......

Neno La Leo;Mithali:16:1-20;[3]Mkabidhi BWANA kazi zako,Na mawazo yako yatathibitika....

"Swahili NA Waswahili" Nawapenda Wote.

Saturday 22 June 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Oliver Mutukudzi!!!!




Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo ni Oliver  "TUKU" Mutukudzi;
 Maneno mengi sina Burudika tuu..jee anakubamba/kupenda kazi zake?
Twende Soote sasa....

   "Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday 16 June 2013

Nimatumaini yangu J'Pili imekwenda/Inakwenda vyema;Honngereni Wa BABA wote mnaojua Majukumu Yenu!!!!



Natumaini mmekuwa/Mnaendelea   na J'Pili Yenye Baraka,Upendo,Amani,Furaha na Tumaini..
MUNGU akamwambia Ibrahimu,Sarai mkeo,hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jijna lake litakuwa SARA.

Neno La Leo;Mwanzo:17:15-22.Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka,ambaye  Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao...

Hongereni Kina BABA Wote...Nawe usiyekuwa na mtoto na unapenda/hitaji kuitwa/kuwa na Watoto MUNGU Hajakuacha/kukusahau..Usikate Tamaa Soma hili Neno Uone Abrahamu MUNGU alimtendea....


Wakati wa Home work..hapa hakijaeleweka..

Hapa kuna matumaini....


Hapa urafiki..
Kutembea tembea baada ya yote!!!!!



"Swahili NA Waswahili" MUNGU Awabariki 

Friday 14 June 2013

Kuelekea Siku Ya Mtoto Wa Afrika;Da'Tolly Tolly Anauliza;UNALEA WATOTO AU MAYAI?KESHO YAO ITAKUAJE?




Imeandikwa na da'Tolly .....wa TOLLYZKITCHEN

Kama  Unalolote linalohusu Siku Ya Mtoto wa Afrika na unapenda kushiriki nasi usisite kututumia Email;rasca@hotmail.co.uk

kwa Habari na Mambo Meengi  ya Watoto,Wazazi/Walezi.nifuate huku;http://www.watotonajamii.blogspot.co.uk/

   Pia Usisahau kuungana nasi katika kucheza pamoja na watoto wetu..hapa UK siku hiyo tarehe 16 ni Siku  ya BABA..[FATHER'S DAY] Watoto na Wazazi watakuwa na Mambo meengi..
Basi Tukutane wiki inayofuata  J'Mosi ya tarehe 22/06/2013.


Unalea Watoto au Mayai? si Maneno yangu msome da'Tolly.



043
Katika maisha si kila unalolifanya unafanya kwasababu unapenda au unafurahia, wakati mwingine maisha yanatulazimu kufanya mambo Fulani au kujua jambo Fulani kwasababu ni muhimu kwetu au kwasababu jamii inatutaka tujue na kuweza.
Kupika ni moja ya hayo. si kila mtu anapenda kupika, lakini ualisia wa maisha unawalazimu  watu kujua kupika.Kwa maisha yetu ya kiafrika kujua kupika ni jambo la lazima kwa mwanamke,hata ivyo ualisia wa mabadiliko ya maisha karne hii ya 21 yanawalazimu hata wanaume kujua kupika.
Kupika ni jambo la kujifunza kwa wazazi na ndugu wanaokuzunguka katika kukua kwake,ni kitu unachojifunza kila siku ya maisha yako na kwakufanya mazoezi ya kupika mara kwa mara kama sehem ya ushiriki wa kazi za nyumbani.
Wazazi wa siku hizi wanawanyima watoto  nafasi ya kujifunza kupika kwa kushiriki kazi za nyumbani.Familia nyingi zina dada au kaka anaefanya kazi zote za ndani na matokeo yake watoto wengi hufanya kazi ya kuangalia Tv siku nzima na kukaa kwenye viti kama mayai  kwenye trei.
Kuwalea watoto wako kama mayai,kutowashirikisha katika kazi za nyumbani na shughuli zako za biashara na mambo mengine ni kosa kubwa sana.Ni kumnyima mtoto nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yampasayo kujua kwenye maisha.
Huku jikoni mtoto anatakiwa kushiki kazi ndugo ndogo tangu anapokua mdogo,aanze kwa kutoan vyombo mezani,kufuta meza,kupanga meza,kufagia jiko,kutwanga vitunguu swaumu na mambo madogo madogo kama hayo kutokana na umri wake.
Hapo nyumbani wapangie watoto zamu na taratibu za kufanya kazi za nyumbani.si kupika tu,bali kazi za nyumbani kwa ujumla.
Tulipokuwa wadogo,mama yetu alitupangia zamu na ratiba ya kazi zote,kutofanya kazi katika wakati husika kuliambatana na adhabu ya kufanya kazi hiyo kwa siku tatu  mfululizo kama kazi ya nyongeza,uku wengine wakipumzika.Ratiba ya kazi hizi ilibandikwa nyuma ya mlango wa kabati  jikoni na ilizingatia umri.Ratiba yetu likua na mambo haya:
1.Ratiba ya kuamka kuandaa chai asubuhi
2.Ratiba ya kupika  mchana na usiku
3.Ratiba ya kuosha vyombo,wadogo wanaosha vyombo vya chai asubuhi
4.Ratiba ya kupanga meza(wadogo)
5.Ratiba ya kufuta meza(wadogo)
6.Ratiba ya kusafisha Sebule na jiko
7.Ratiba ya kusafisha vyumba
8.Ratiba ya kusafisha choo na bafu
9.Ratiba ya kufagia nje
10.Ratiba ya kumwagilizia mauwa
11.Ratiba ya kumsaidia mama kwenye biashara
12.Zamu ya kusali na kuongoza ibada ya jioni
042
Zaidi ya ratiba kulikua na kanuni au sharia ambazo zilikua lazima kufuata na kila moja ilikua na adhabu yake pale unapoivunja.
1.Lazima kuoga kabla ya kwenda mezani kupata kifungua kinywa na kabla ya kwenda kupata chakula cha jioni.Usipooga basi hakuna kwenda mezani,ikimaanisha hautakula.
2.Lazima kufua nguo na kupanga kabati kila jumamosi.Usipofanya hivyo jumapili wengine wakipelekwa kutembea,wewe unabaki nyumbani .
3.Home work zote lazima zifanywe kabla ya saa moja jioni,na umpe mama,baba,mtu mkubwa yoyote akague .Usipofanya hivyo mara nyingi adhabu ilikua kufanya maswali mengine kumi kama hayo au anamwambia mwalimu wako akushugulikie shuleni.
4.Kwenda kanisani ni lazima,hili halikua na mjadala na hakukua na namna ya kulikwepa.
5.Hakuna kuangalia Tv wala sinema kabla ya saa nane mchana.Asubuhi ni walkati wa kazi,mapumziko ni Baada ya  Lunch.Adhabu ya kuvunja hili ilikua ni kupewa kazi za kufanya,kwani kukaa unaangalia Tv maana yake huna kazi.Unaambiwa kashone vifungo vilivyotoka kwenye nguo zako,au kafute na kubrashi viatu vyako.
  • Hizi ni baadhi ya ratiba na sharia au kanuni zilizonilea,na kunifanya niwe hivi nilivyo leo.ratiba hizi zilihusisha watoto wote,wakiume na wakike.Kwa ratiba kama hizi mtoto anajifunza kila kitu  na anajifunza kujitegemea kwa kila kitu.
Ifike mahala muone aibu na mjiulize watoto wenu watakua kina baba au kina mama wanamna gani wakikua.Waswahili husema  Samaki mkunje  angali mbichi.Wewe unaengoja Samaki wako aive ndipo umkunje,utatia aibu na utaumbuka.
Pia ni vyema kujua kuwa,ni katika ufanyaji wa kazi hizi unaanza kuona na kutambua uwezo na vipaji vya watoto.Mpishi mzuri utaanza kumuona mapema,wale wanaopenda kusimamia wenzao ndio vipaji vya uongozi hivyo,kuna wale wa maneno mengi ila hawafanyi kazi nao utawajua na uanze kuwasaidia kubadili tabia hizo zisizofaa.
Hapa jikoni watoto wakija lazima niwape kazi yakufanya,kama hakuna kazi basi nampa kiti akae mlangoni(kukwepa ajali) tuongee mawili matatu wakati napika.Kwani najua anapoangalia niachofanya kula jambo anajifunza,na mara nyingi wanakua na maswali mengi juuu ya lile ninalolifanya.
Yangu ni haya tu kwa leo,yaliyobaki kazi kwako.Ukiamua kulea watoto kama mayai  basi endelea ukijua unamuharibia mtoto maisha.
kwa mambo ya mapishi na malezi ingia hapa;http://tollyzkitchen.wordpress.com/



Jikoni Leo; Na Mswahili Wetu da' Tolly Tolly!!!!!!!!



HUKU JIKONI MAMBO YANAPAMBA MOTO:Sasa tunapatikana ndani ya ……………




008
Leo ni siku ya furaha hapa jikoni na naamini itakua siku ya furaha kwa wanafamilia wote wa jiko hili. katika kufurahi huku basi hata wale ambao si wanafamilia wa jiko hili watavutiwa kujiunga nasi.
Lakini kabla sijakwambia kulikoi ya furaha hii, nachukua nafasi hii kukushukuru wewe mwanafamilia  wa jiko hili kwa kuwa nasi kila siku hapa jikoni. Uwepo wako jikoni hapa ndion chachu ya maendeleo ya jiko hili.
  • Mchango wako ni wathamani sana kwetu , unaposoma makala zetu, unapoandika comment, unapo like page , unapo tu-follow kwenye twitter, Unapotutizama kwenye instagram , unapotutumia barua pepe, unapo tupigia simu au unapowaambia wengine juu ya jiko hili unakua umechangia sana kuliendeleza jiko letu.
Waswahili husema HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA, wenzetu waingereza husema A JURNEY OF A THOUSAND MILES BEGINS WITH A STEP. Jiko letu pia lilianza kama mchicha,na kadri siku zinavyozidi kwenda nasi tunakua  na tunazidi kuongezeka. Ninakila sababu ya kuamini kwamba hapo mebeleni  familia yetu hapa jikoni itakua kubwa sana.
Furaha ya familia ya jiko hili leo inaletwa na hatua moja kubwa ambayo jiko letu limepiga. Kwa mara ya kwanza kabisa jiko hili limeweka VIDEO YAKE YA KWANZA NDANI YA YOUTUBE. Link ni hii, bofya http://www.youtube.com/watch?v=zpTnpAljBd0
Kwa kua ndio video ya kwanza, basi tuliona nivyema iwe video ya kuitambulisha Tollyzkitchen kwako. Tunaamini ukilifaham jiko hili vizuri basi utapata sababu ya kukaribisha na wengine. Na pengine utapenda kuungana nasi katika shughuli mbalimbali za hapa jikoni.
Hapa jikoni tutarusha video za aina  tatu ,
  1. Makala maalum za maongezi tu (kama hii unayotizama leo). Makala hizi zitakua ni mtiririko wa  maongezi au mafundisho juu ya mambo mbalimbali ya  jikoni.
  2. Makala za mapishi kwa vitendo. Hizi ni video ambazo zitafundisha na kuelekeza namna ya kupika vyakula mbalimbali  pamoja na mambo mengine ya jikoni.
  3.  Makala maalum za mahojiano. Haya yatakua ni mahojiano juu ya mambo mbalimbali yanayohusu chakula na yanayokizunguka chakula.Hapa utawasikia watu mbalimbali kama wajasiriamali, wakulima, wanasiasa, masupa staa na wengine wengi.
Makala hizi zote zitakua katika lugha ya Kiswahili. Unapozitafuta ndani ya YOUTUBE pia tumia vichwa vya habari vya Kiswahili,kama utatumia jina basi fatuta TOLLY BEN. Hata hivyo Tutajitahidi sana kuweka link zote kwenye blog ili kukurahisishia .
Nakuomba sana na nakusihi uwakaribishe na wengine jikoni hapa, makala hii yakwanza ikikufurahisha itakua vyema sana uki share link hii na wengine.
Naamini taarifa hizi ni njema kwako na zimekufurahisha kama ambavyo zinatufurahisha sisi hapa jikoni.
TOLLYZKITCHEN  TUNAPORESHA MAPISHI NYUMBANI


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 12 June 2013

Coventry Women Gala ya Tarehe-08/06/2013[Sehemu ya 2]Mgeni Alikuwa Mama Balozi JOYCE KALLAGE!!!


Waungwana;Tunaendelea na Matukio ya Coventry Women Gala...Mama Balozi Joyce Kallage na Da'Rose Kiondo..Wakifurahi Pamoja..ni Raha tuu..
Da'Agness akikaribisha Wageni na kujitambulisha.

Da'Halima akijitambulisha na kuwahakikishia watu Watashiba..

Hawa walisimamia Chakula na Kukaribisha Wageni.

Da'Stella akijitambulisha ..Yeye alikuwa msimamizi mkuu.

Da'Mija akijitambulisha..Yeye alisimamia Mitindo

Da'Rachel akijitambulisha..Yeye alisimamia Burudani, ndiye aliyepamba Ukumbi na Mc..
DJ Richie Dee..Yeye ndiyo aliyetuburudisha[Muziki]

Mama Balozi ;JOYCE KALLAGE;
Yeye alitupongeza na kutusisitiza kuendelea na masomo,Kusaidia watoto wengine wa kike Nyumbani wanaohitaji Kuendelea na Masomo lakini hawana uwezo.Kuungana  na kujitoa kwa Moyo na kufanya mambo mengi ya maendeleo.Pia alisisitiza sana tusijisahau Kufuata na kuendeleza mambo mema ya Kwetu..Hategemei mtoto wa mswahili asijue kiswahili ni aibu.Kama tumeshaliachia hili watoto wetu hawajui "KISWAHILI" Tufungue darasa la Kiswahili.
Aliongea Meengi.
Asante sana MAMA,Nasi tutafuata Ushauri wako.
[TEAM MAMA BALOZI]

Wanawake Oyeee!!!!Coventry Women Gala Oyeee!!!!!Waswahili Ughaibuni Juu!!!!!Wanawake na Maendeleo!!!!!
Amesema amefurahi kuona tumeweza kurudia tena!!

Hayo yote kwa furaha na unyenyekevu yalitoka kwa da'MARIAM KILUMANGA;Mwenyekiti wa;Tanzania Women's Association[TAWA UK.]
Alisisitiza Tusikate Tamaa na yupo pamoja nasi wakati wowote..Da'Mariam tulikuwa nae wakati uliopita.
Asante Saaaaana.
Dada/Mama;Hilda..Yeye ni Mfanyabiashara wa siku nyimgi,Amepitia changamoto nyingi sana.
Na sasa amesimama vilivyo..Ametufunza mambo mengi sana..alisema yeye si muongeaji sana..Mzuri sana kwenye Vitendo.

Asante Sana kwa Yote mama.


Dada;ROSE KIONDO,Kutoka Ubalozi wetu wa Tanzania hapa UK.

Da'ROSE KIONDO;Yeye alitusisitiza kujihusisha na Ubalozini kwani pale ni kwetu na tutambue hivyo..kwanini tunakuwa waoga na Nyumbani kwetu?Mtu hujivunia chake na kwako..kwa hapa tulipo Pale ndiyo Nyumbani,Wapo pale kwa sababu yetu pia.Aliongea Meengi yenye Faida kwetu.

Asante sana dada.

Alicheza kwanza..

Alitumia vilivyo uwanja...

Mc..mwenyewe hoii..usimchezee kabisa..Mada zake anazitunza vilivyo..

Ni-Aunty/Mama da'Fay..wewe utakavyo penda kumuita yeye hana shida..Yeye alitusisitiza zaidi,kutumia muda vizuri,kujiendeleza kielimu kwani haina mwisho..atakushangaa eti ukisema sina muda kwasababu nina watoto,mume,kazini,kazi za nyumbani..Ukiamua na kama wewe ni msomaji utasoma tuu..ni wewe utakavyojipanga..kila siku utasema muda huna mpaka lini?Tusipoteze muda kwenye mambo yasiyo na manufaa..hasa  tutumie hii MITANDAO vyema na si kutukanana na kuumizana..Tupendane..
Bila kusahau DIET..Na kutafuta mbinu ya kupunguza mwili..Aliongea meengi saana siwezi kumaliza yote hapa..


EPUKA UZEE USIOKUWA WAKO BIBI EEEEEHH.
.

Da'SUSAN

DA'SUSAN yeye aliongelea MADAWA YA KULEVYA..Utayajuaje,Watumiaji,kuepuka,uuzaji,Madhara yake na kuwalinda watoto wetu,Vijana,Jamii na nasisi wenyewe pia..Na mambo mengii yahusianayo na Madawa ya kulevya..

Asante sana.
Umeona hiyo beji niliyo jibandika hapo? Hawa wanatengeneza keki,beji na mengine meengi..ni wadada wanaojituma..ni AHLAM NA KOIYA..Wape Kazi watoto wa Nyumbani..
Hongereni Sana

Da'TINNA..Yeye ni mwimbaji  mzuri sana sauti MUNGU amemjaalia..usisite kumpa kazi. Dada/Mtoto wa Nyumbani.ni burudani tosha sauti yake.

Mama Balozi,Wageni walipata Nafasi  ya kuona/kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wanawake Wenzao...


Wewe unangoja nini?
Jitoe,Jitambulishe/Tambulisha kazi zako.Ujuzi wako..
Nategemea Kuwaona Wanawake wengi Shughuli ijayo..