Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 29 March 2015

Tumalizie Jumapili Hii kwa Amani na Imani;Burudani-Mama Jusi Choir, Moshi-Pendo Kuu,Ee Bwana nimesikia,Bwana nina haja nawe...!!!!!!


Wapendwa;Tumalizie Jumapi hii kwa Amani,Imani,Upendo na Kweli.
 13Basi, ndugu zangu, msishangae kama ulimwengu unawachukia nyinyi.
18Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.
Neno La Leo:1 Yohana 3:1-24
Watoto wa Mungu
1Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.2Wapenzi wangu, sisi ni watoto wa Mungu sasa, lakini bado haijaonekana wazi jinsi tutakavyokuwa. Lakini tunajua kwamba, wakati Kristo atakapotokea, tutafanana naye kwani tutamwona vile alivyo. 3Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa.
 4Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria. 5Mnajua kwamba Kristo alikuja kuziondoa dhambi zetu, na kwamba kwake hamna dhambi yoyote. 6Basi, kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi dhambi; lakini kila mtu atendaye dhambi hakupata kamwe kumwona wala kumjua Kristo.7Basi, watoto wangu, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Mtu atendaye matendo maadilifu ni mwadilifu kama vile Kristo alivyo mwadilifu kabisa. 8Lakini atendaye dhambi ni wa Ibilisi, maana Ibilisi ametenda dhambi tangu mwanzo. Lakini Mwana wa Mungu alikuja duniani kuiharibu kazi ya Ibilisi.
 9Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu. 10Lakini yeyote asiyetenda mambo maadilifu, au asiyempenda ndugu yake, huyo si mtoto wa Mungu. Hiyo ndiyo tofauti iliyoko kati ya watoto wa Mungu na watoto wa Ibilisi.

Pendaneni
11Na, ujumbe mliousikia tangu mwanzo ndio huu: Tunapaswa kupendana! 12Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!
 13Basi, ndugu zangu, msishangae kama ulimwengu unawachukia nyinyi.14Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uhai kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo. 15Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake. 16Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu. 17Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma, anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu? 18Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.
Uthabiti wetu mbele ya Mungu
19Hivyo ndivyo tuwezavyo kuwa na hakika kwamba sisi ni watu wa ukweli; na hatutakuwa na wasiwasi mbele ya Mungu. 20Kwa maana, hata kama dhamiri zetu zatuhukumu, twajua kwamba Mungu ni mkuu kuliko dhamiri, na kwamba yeye ajua kila kitu. 21Wapenzi wangu, kama dhamiri zetu hazina lawama juu yetu, basi, twaweza kuwa na uthabiti mbele ya Mungu, 22na kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza. 23Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Yesu Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.24Anayezitii amri za Mungu anaishi katika muungano na Mungu na Mungu anaishi katika muungano naye. Kwa njia ya Roho ambaye Mungu ametujalia, sisi twajua kwamba Mungu anaishi katika muungano nasi.

Bible Society of Tanzania








"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Sunday 22 March 2015

Tuendelee na Jumapili Hii vyema;Burudani-Kinondoni Revival Choir Mtafuteni Bwana,Ayubu,Chukua Hatua..!!!!!!







Wapendwa;Nawatakia kila lililo Jema,Baraka,Amani,Furaha,Upendo,Unyenyekevu,Busara, Hekima na Shukrani.
MUNGU akawaguse na Kuwabariki- Yatima,Wajane,Wagonjwa walio Hospitalini/Nyumbani,Walio Magerezani pasipo na Hatia,Wenyeshida/Tabu.
MUNGU atuongoze katika kunene na Kutenda.





29Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.
Umoja katika jumuiya

Neno La Leo;Waefeso4:1-32

Umoja katika jumuiya
1Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. 2Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni nyinyi kwa nyinyi kwa mapendo. 3Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu. 4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja. 5Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja; 6kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote. 7Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na Kristo. 8 Kama yasemavyo Maandiko:
“Alipopaa mbinguni juu kabisa,
alichukua mateka;
aliwapa watu zawadi.”
9Basi, inaposemwa: “Alipaa juu,” ina maana gani? Maana yake ni kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani. 10Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu. 11Ndiye aliyewapa watu zawadi: Wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Injili, wengine wachungaji na waalimu. 12Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, 13na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe. 14Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila. 15Kama tukiuzingatia ukweli kwa moyo wa mapendo tutakua katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; 16chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo.

Maisha mapya katika Kristo
17Basi, kwa jina la Bwana, nawaonyeni: Msiishi tena kama watu wasiomjua Mungu, ambao fikira zao zimekuwa upuuzi mtupu, 18na akili zao zimo gizani. Wako mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya upumbavu ulio ndani yao na ukaidi wao. 19Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu. 20Lakini nyinyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo. 21Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu. 22Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu. 23Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu. 24Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu. 25Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo. 26 Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima. 27Msimpe Ibilisi nafasi. 28Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini. 29Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu. 30Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni. 31Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu! 32Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.
Bible Society of Tanzania








"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

TANZANIA CHILDREN'S PROJECT YAFANYA HARAMBEE KUSAIDIA WATOTO TANZANIA COLUMBIA, MARYLAND


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Switebert Mkama(pichani kushoto)
Rais wa Tanzania Children's Project Bwn. Timothy Lynch katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani.
 
picha ya pamoja
Picha ya pamoja
 
Kikundi cha muziki kikitoa burudani.

Friday 20 March 2015

Maisha na Malezi;Mama Mtumwa Wa Mapenzi..!!!


MAMA MALKIA WA UPENDO        💎
                                
💞MAMA MTUMWA WA MAPENZI💞          💎

🌾🍃Mwanadamu ulizaliwa katika hisia za kulia  ukiwa kichanga mwenye uchafu Asili ya upendo ipo kwa mama ulipofumbua macho ulikutana na tabasamu la mama.

🌾🍃Mama alitabasamu wakati unalia mama alijifanya uchizi ili kukufurahisha ghafla ungetokea kuwaona mtoto anapocheza na mama yake ungelidhani wote ni watoto kwa mapenzi ya mama.

🌾🍃Mwanadamu tambua unaweza umizwa na wengi lakini upendo wa mama ukakufanya utulie na hakuna mapenzi ya kweli kwa mtu kama mapenzi ya mama.

🌾🍃Mama juu yako baya likikukuta mama hulia mama yupo tayari kudanganya ulimwengu kukukomboa katika matatizo yako.

🌾🍃Alificha chakula wakati ukicheza udogoni na uliporejea ukamkuta amelala lakini aliacha maagizo utakuta wapo wa kukupashia yote mapenzi.

🌾🍃Mama alipoamka mwanzo alikuulizia ameshakula? Ima umekula atafurahi ima hujala atapita majumba ya watu kukuulizia hata kama atatoka miguu peku yote mapenzi tu.

🌾🍃Ulipoumwa usiku halali atataabika kwa kukaa na wewe ukiwa mikononi mwake huku akilalila ukuta pembeni mwa kitanda huku akitarajia pakikucha shingo limuume kwa kukesha na wewe yote mapenzi hayo.

🌾🍃Mtu yoyote akikupenda watu watamshangaa kwanini anakupenda sana? Lakini mapenzi ya mama hayaulizwi kwanini anampenda yote ni nguvu za hisia za upendo toka kwa mama.

🌾🍃Umekuwa sasa huenda hayupo tena mama amekuacha katika dunia ya mihangaiko na wala tambua hakuna tena kiumbe kitachokupenda kama alivokuwa mama.

🌾🍃Na ukiwa umebarikiwa upendo ulio hai kwako namaanisha uhai wa mama basi huenda amechokaa na anatembea kama mtoto sasa rudisha upendo wako kwa kumfanya nae afurahi japo hutoweza kulipiza yote.

🌾🍃Mama utamkumbuka utapomkosa utatamani kuita mama na hata ukipata wa kuwaita upendo hautatoka moyoni.

🌾🍃Wakati ulipotoka alitabasamu basi na wewe hakikisha wakati anakukimbia duniani mfanye atabasamu hata kama atatokwa na machozi .

🌾🍃Mtumie ujumbe huu Mama na kama hunae tena muombe kwa MOLA upatapo ujumbe huu watumie wenzako huenda wakafufua hisia kwa Mama.

🌾🍃HUYU NDIO MAMA MALIKIA WA UPENDO. 

 🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴


Nimetumiwa na Rafiki Nami nimeileta hapa tujifunze sote.

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Saima.

Wednesday 18 March 2015

Niambie Live Show....Ep1‏


Omby Nyongole, Salma Moshi na Queen Mkelemi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.

Ni Niambie Live....

KARIBU

Tuesday 17 March 2015

Monday 16 March 2015

NesiWangu Show...Albinism


Karibu katika kipindi cha NesiWangu.

Katika kipindi hiki, Harriet Shangarai amezungumza na wanaharakati wa masuala ya Albinism. Sehemu ya kwanza ni mazungumzo na Daisy Makwaia wa Albino Charity Organization na sehemu ya pili ni mazungumzo yao na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare wa Afrobino Ltd

Karibu


Sunday 15 March 2015

Tumalizie Jumapili hii vyema;"Happy Mother's Day"Burudani-Upendo NkoneUpendo wa Yesu..!!!!

Wapendwa;Tumalizie Jumapili hii vyema.
"Happy Mother's Day" mama Rachel-siwa[mama'k]
 na Wamama wote wanao jua majukumu yao kama MAMA.
Mungu awape Busara,Hemakima,Maarifa,Upendo,Furaha,Amani na Maisha marefu.
Pole kwa wenzetu waliopoteza/kufiwa na MAMA ..MUNGU awape uvumilivu ,msiache kufuata  yale yote mema MAMA aliyo waachia.
Wale wanaotafuta Watoto MUNGU akaonekane na awabariki nanyi mpate watoto.
MUNGU azidi kutubariki katika malezi.


1Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi? 2Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.

Neno La Leo;Wafilipi 2:1-30

Unyenyekevu na ukuu wa Kristo

1Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi? 2Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja. 3Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.4Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake. 5Muwe na msimamo uleule aliokuwa nao Kristo Yesu:  6Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu;lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Munguni kitu cha kungangania kwa nguvu.7Bali, kwa hiari yake mwenyewe,aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi,akawa sawa na wanadamu,akaonekana kama wanadamu.8Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa,hata kufa msalabani.9Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa,akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.10Ili kwa heshima ya jina la Yesu,viumbe vyote mbinguni, duniani na kuzimu,vipige magoti mbele yake,11na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana,kwa utukufu wa Mungu Baba.




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday 14 March 2015

PAZI REUNION HOUSTON, TEXAS LEO KUWAKA MOTO WACHEZAJI WENGI NDANI YA NYUMBA‏



 Timu ya Pazi wanaume wakipata picha ya pamoja na mashabiki wao walipokua nyumbani kwa madikodiko ambaye pia ni mmoja wa waratimu wa tamasha hili la kumbukumbu ya timu hiyo iliyowika miaka mingi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Tamasha hili lililobeba jina la Pazi Reunion litafikia tamati leo Jumamosi March 14, 2015 kwa mechi kadhaa na kuakumbuka na kuaenzi viongozi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki.
 Pazi Queens wakiwa katika picha ya pamoja leo patakua hapatoshi.
Patrick Mwigula kutoka South Carolina na Atiki Matata kutoka Uingereza wachezaji wa Pazi waliowika miaka ya nyuma wakijadili mchezo wa leo kama walivyokutwa na kamera ya Vijimambo.
 Atiki Matata na Richard Kasesela wakipata picha ya pamoja.
Kulia ni Masawe shabiki wa Pazi wa miaka mingi si mazoezi si mechi alikua hakosekani uwanjani hapa akisalimiana na Richard Kasesela mara tu walipoonana baada ya kupoteana kwa miaka mingi.
Kutoka kushoto ni Emmanuel, Patrick na Kasesela wakikumbushana enzi zao za Pazi.
Wachezaji wa Pazi toka shoto ni Vitalis Gunda toka Maryland, Richard Kasesela toka Tanzania na Willy Crrusa toka Houston, Texas wakikumbushana enzi zao.
Kwa picha zaidi Bofya HAPA

Friday 13 March 2015

Pazi ReUnion USA. Mambo yazidi kupamba moto Houston Texas








 Watatu toka kushoto ni Richard Kasesela alipokua akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa George  Bush Intercontinental uliopo Houston, Texas nchini Marekani kwa ajili ya Pazi Reunion itakayofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 katika uwanja wa mpira wa kikapu wa Pilgrim uliopo katika kanisa la Lutheran lililopo Houston. Wengine katika picha ni wenyeji wake waliompokea,  kutoka kushoto ni Willy Crrusa, Aika na Flora Mochiwa maarufu kama Madikodiko. Mchezaji mwingine anayekuja kwenye maadhimisho hayo ya Pazi toka nje ya Marekani ni Atiki Matata anayekuja siku ya Ijumaa March 13, 2015 akitokea Uingereza. Picha na VIJIMAMBO
 Richard Kasesela akitest uwanja wa mpira wa kikapu mara tu alipowasili uwanjani hapo mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege kushoto ni Davis mchezaji mwingine wa mchezo huo, Flora Mochiwa na Willy Crrusa wakiangalia kama bado wamo. Richard Kasesela richa ya kuwa mchezaji wa Pazi pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania.
 Wachezaji wa mpira wa kikapu wakipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.
 Mdau toka Columbus, Ohio akiwa tayari kushuhudia Pazi Reunion itayaofanyika siku ya Jumamosi March 14, 2015 ndani ya jiji la H-Town.
 Willy Crrusa katika picha ya pamoja na Andrew wakati wakiwa ndani ya madikodiko.
 Wageni wakipata chakula huku maongezi yakiendelea.
Andrew akipata picha ya pamoja na Richard Kasesela.

WaTanzania wa Houston Texas kurekodi kipindi kuhusu mauaji ya Albino Tanzania‏





Wadau kutoka New York katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa.



Wadau wa North Carolina wakiwa kwenye kipindi kilichopata kurekodiwa.


Timu ya Vijimambo ikishiriana na Kwanza Production inapenda kwanza kutoa pongezi kwa Watanzania Houston kwa jitihada zao za kupambana na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi
Pia inaandaa kipindi cha video kuongelea hili swala kwa mapana zaidi na kuangalia jinsi gani ya kukomesha mauaji haya ambayo yanaleta fedheha na aibu  ikiwemo ukiukaji wa haki za binadamu.

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumampili saa 8 mchana (2pm) mahali ni Extended Stay America chumba namba 224 anuani ni 2424 West Sam Houston Prkway, Houston, TX 77042. 

Kwa maelezo zaidi wasiana na 301 335 6383 asante


Ujumbe kutoka kwa ndugu zetu hapo chini.

Monday 9 March 2015

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta......Wizara na Kugombea Urais


Karibu katika sehemu hii ya pili ya mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

Aliketi nasi kuzungumzia kuhusu kazi zake kama Waziri wa Uchukuzi na pia nia yake ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015)

Karibu


Sunday 8 March 2015

Nawatakia Jumapili njema Na Happy Women's Day;that's my king-.!!!Burudani-Your Name Brings Healing To Me - Planetshakers (Worship song with Lyrics)


Wapendwa;Natumaini Jumapili inaendelea Vyema..
Mungu andelee kuwa Bariki na Kuwalinda kila iitwapo Leo..

"Happy Women's Day"


That's My King..!!!!!!



"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.

Saturday 7 March 2015

Stara T aachia wimbo wa Siku ya Wanawake Duniani



Msanii Stara T, ametoa wimbo mpya UWEZESHWAJI WA MWANAMKE ambao ni maalum kwa ajili ya siku ya kinamama dunia inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.


Wednesday 4 March 2015

Jikoni Leo;Kenyan Mukimo Recipe How to make Mukimo - Jikoni Magic

Waungwana;"Jikoni Leo"Tujifunze kupika "Mukimo" chakula hiki kinapikwa/kuliwa sana na Ndugu zetu waKenya...
Mimi ni mmoja wa wapenzi wa chakula hiki,lakini sijawahi kupika huwa napikiwa na Rafiki yangu.
Vipi wewe Mpendwa/Muungwana umeshawahi kula/kupika Mukimo?
Kama bado jaribu natumai utakipenda.....


Twende wote sasa..


Shukarani/Thanks;Jikonimagic

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Monday 2 March 2015

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta (Pt I).......KATIBA


Karibu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.
Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata
Karibu