Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Maisha. Show all posts
Showing posts with label Maisha. Show all posts

Monday 7 September 2015

Bin'adam "TENA"....Na maisha KINYUMENYUME. Apumzikaye kusherehekea SIKU YA KAZI


Na Mubelwa Bandio

 Ni SIKU YA KAZI hapa Marekani. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko". NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.

Mmmmmhhh!!! Umeona eeee?


Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?


Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?


Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?


Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.


TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.


Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?" Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia


-Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?


-Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.


-Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.


-Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.
EVER WONDER .......-Why
the sun lightens our hair, but darkens our skin?


-Why can't women put on mascara with their mouth closed?


-Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?


-Why is 'abbreviated' such a long word?


-Why is it that doctors call what they do 'practice'?


-Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?


-Why is the man who invests all your money called a broker?


-Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?


-Why isn't there mouse-flavored cat food?


-Why didn't Noah swat those two mosquitoes?


-Why do they sterilize the needle for lethal injections?


You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!


-Why don't sheep shrink when it rains?


-Why are they called apartments when they are all stuck together?


If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?
HIVI TUNAWAZA NINI?
***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

Friday 20 March 2015

Maisha na Malezi;Mama Mtumwa Wa Mapenzi..!!!


MAMA MALKIA WA UPENDO        💎
                                
💞MAMA MTUMWA WA MAPENZI💞          💎

🌾🍃Mwanadamu ulizaliwa katika hisia za kulia  ukiwa kichanga mwenye uchafu Asili ya upendo ipo kwa mama ulipofumbua macho ulikutana na tabasamu la mama.

🌾🍃Mama alitabasamu wakati unalia mama alijifanya uchizi ili kukufurahisha ghafla ungetokea kuwaona mtoto anapocheza na mama yake ungelidhani wote ni watoto kwa mapenzi ya mama.

🌾🍃Mwanadamu tambua unaweza umizwa na wengi lakini upendo wa mama ukakufanya utulie na hakuna mapenzi ya kweli kwa mtu kama mapenzi ya mama.

🌾🍃Mama juu yako baya likikukuta mama hulia mama yupo tayari kudanganya ulimwengu kukukomboa katika matatizo yako.

🌾🍃Alificha chakula wakati ukicheza udogoni na uliporejea ukamkuta amelala lakini aliacha maagizo utakuta wapo wa kukupashia yote mapenzi.

🌾🍃Mama alipoamka mwanzo alikuulizia ameshakula? Ima umekula atafurahi ima hujala atapita majumba ya watu kukuulizia hata kama atatoka miguu peku yote mapenzi tu.

🌾🍃Ulipoumwa usiku halali atataabika kwa kukaa na wewe ukiwa mikononi mwake huku akilalila ukuta pembeni mwa kitanda huku akitarajia pakikucha shingo limuume kwa kukesha na wewe yote mapenzi hayo.

🌾🍃Mtu yoyote akikupenda watu watamshangaa kwanini anakupenda sana? Lakini mapenzi ya mama hayaulizwi kwanini anampenda yote ni nguvu za hisia za upendo toka kwa mama.

🌾🍃Umekuwa sasa huenda hayupo tena mama amekuacha katika dunia ya mihangaiko na wala tambua hakuna tena kiumbe kitachokupenda kama alivokuwa mama.

🌾🍃Na ukiwa umebarikiwa upendo ulio hai kwako namaanisha uhai wa mama basi huenda amechokaa na anatembea kama mtoto sasa rudisha upendo wako kwa kumfanya nae afurahi japo hutoweza kulipiza yote.

🌾🍃Mama utamkumbuka utapomkosa utatamani kuita mama na hata ukipata wa kuwaita upendo hautatoka moyoni.

🌾🍃Wakati ulipotoka alitabasamu basi na wewe hakikisha wakati anakukimbia duniani mfanye atabasamu hata kama atatokwa na machozi .

🌾🍃Mtumie ujumbe huu Mama na kama hunae tena muombe kwa MOLA upatapo ujumbe huu watumie wenzako huenda wakafufua hisia kwa Mama.

🌾🍃HUYU NDIO MAMA MALIKIA WA UPENDO. 

 🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴


Nimetumiwa na Rafiki Nami nimeileta hapa tujifunze sote.

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Saima.

Tuesday 2 April 2013

Mbegu Za Furaha Na Kaka Said Kamotta!!!!!!!Kila mtu anapenda kuwa na furaha muda wote, Ila kwa bahati mbaya sio wote tunafuraha kwasababu mbalimbali za kimaisha. Wengine wana matatizo ya kiafya, wengine wana matatizo ya kiuchumi na wengine wana matatizo ya kimahusiano na watu muhimu kwao, yote haya ni matatizo tunayokabiliana nayo katika maisha. Licha ya kuwa kila mtu na matatizo yake bado kuna maana na umuhimu wa wewe kuwa na faraja ya kuwa hali za maisha yetu hubadilika kila siku. Hakuna hali isiyobadilika iwe nzuri au mbaya ila tuna matumaini ya kuwa siku zote tuwe wenye furaha na mafanikio katika pilikapilika za maisha yetu. Kwa mantiki hiyo kuna mambo ambayo ukizingatia yatakuza na kuimarisha furaha yako.

Je ni mambo gani hayo?
 

Inaendele..Zaidi ingia;http://kamotta.blogspot.co.uk/


       "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 21 March 2012

Waswahili na Maisha yao!!!!!!!

Hakuna linaloshindikana au?Asante mwanangu Amina kwa kazi nzuri,Joto sasa basi.Kumbe inawezekana!!!!

Friday 25 March 2011

Pozi la leo!!!!

Mpendwa picha na pozi.Unakumbuka picha za zamani za studio imepambwa maua?
Kama si sasa ulipiga ulipokuwa mtoto au wazee/wazazi wako,Je inakukumbusha nini/wapi?.Karibuni sana!!!.

Saturday 12 March 2011

Wanaume Wanaopigwa na Wake zao!!!!!!!!!!!

Hivi  kuna Wanaume  wanaopigwa  na  kunyanyaswa  na  Wake zao? Je nao wanakitengo cha kuwasaidia kama vile Tamwa na kwingine? Kwanini  kelele nyingi/mashitaka mengi  niyasikiayo  ni ya Wanawake,Au Wanaume ni wavumilivu,wanaona aibu,wanajikaza kiume au wao hawaumizwi na wakiumizwa wanayamaliza wenyewe? Karibu tuelimishane wapendwa!!!!!!!!.

Tuesday 8 March 2011

Siku ya Wanawake!!! Mshindi wa Shindano la Wanawake wenye HIV!!!!!!!!!

Mwanamke kutoka Botswana, Anaeishi  na  virusi  vya  Ukimwi. Mashindo hayo ya Wanawake yaliyo fanyika  2007 , Wanawake walijitokeza ili kuifaamisha jamii kwamba  kuwa na Ukimwi siyo mwisho wa Maisha!!!!!!!!Je wewe unamaoni gani katika hili? Tuungane pamoja katika kuelimishana na kusaidia Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI!!!!!!!!.

Monday 21 February 2011

Wanaume na Majukumu!!!!!!!!

Wanaume wanaokaa vijiweni(maskani), wanaocheza bao siku nzima, wanao shinda vilabuni,wapambe na wengine.Je niukosefu wa kazi,mitaji,ubunifu,uvivu,kuchagua kazi au kukimbia Majukumu yao?Wewe msomaji  unamawazo/ushauri gani?.Tuungane pamoja katika kujifunza karibu sana!!!!!!!

Sunday 30 January 2011

Wanawake na majukumu!

Wanawake wa zamani na waleo nani wanamajukumu mazito?.Tulinganishe wa vijijini wa leo na wa zamani,
Pia wa mjini  wa leo na wa zamani. Wa mjini  wa leo wana  wafanyakazi wa ndani,mitandao,Elimu na ujuzi mwingi tu,Pia wa vijijini wa leo wana mashine za kusaga  na huduma nyingine. Je wewe mwenzangu unamtazamo gani?

Wednesday 19 January 2011

Unapokuwa na mawazo faraja yapatikana wapi?Yaweza patikana kwa kusoma  vitabu,  kwenye mikusanyiko,kuwapekeyako au?
Nasubiri kwako msomaji maana kila mtu ana mawazo ila kuna yanayochanganya!!!!!!!!