Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 30 January 2011

Wanawake na majukumu!

Wanawake wa zamani na waleo nani wanamajukumu mazito?.Tulinganishe wa vijijini wa leo na wa zamani,
Pia wa mjini  wa leo na wa zamani. Wa mjini  wa leo wana  wafanyakazi wa ndani,mitandao,Elimu na ujuzi mwingi tu,Pia wa vijijini wa leo wana mashine za kusaga  na huduma nyingine. Je wewe mwenzangu unamtazamo gani?

10 comments:

Simon Kitururu said...

Mimi nafikiri ugumu wa kitu mara nyingi uko KISAIKOLOJIA zaidi ndio maana UGUMU mara nyingi hutegemea mtu na mtu.


Labda ndio maana aonekanaye ana kila kitu bado ndiye atafutaye kitu,...
... na kwa kua anapikiwa bado kwake ni ujanja kupikia mtu na kama habebi mizigo labda bado anaenda GYM kubeba vitu ,...
....na labda MAJUKUMU ACTUALLY sio kitu kibaya hasa kama wajio na majukumu utakuta wengine mpaka wanafikiri kujiua kisa maisha hayana MAANA!:-(

NI mtazamo tu!

Rachel Siwa said...

Ni kweli@kaka Kitururu kupikiwa na kubebewa anaona ujanja naye anakubeba vingine Gym hahahha nimekupata kaka majukumu yanaweza kupelekea kifo!!!!.

EDNA said...

Binafsi nafikiri wa vijijini wanafanya kazi kwa bidii tena katika mazingiara magumu,Ebu fikiria Mama na mtoto mgongoni anafuata maji umbali wa kiliometa 10...Akirudi aende porini kutafuta kuni, na hapo shamba linamsubiri....

Simon Kitururu said...

@Da EDNA:

UGUMU wa kitu nafikiri unategemea na mtu na mtu na katika ukuaji mtu kajifunza nini na KAZOEA nini!

Naamini kabsa kama umekulia samba na uazoea KILIMO sio adhab kihivy . Na unaweza kuja mjini ukaona mahangaiko ya DAR es salaamu labda ni fadhali ujikalie tu KIJIJINI kwa kuwa hujazoea.

Nakumbuka BIBI yangu ilikuwa hawezi kukaa sana mbali na kijini kwake MBAGA Manka huko upareni. Watoto wake walikuwa wanajaribu kumfanya akae nao mabali na UPARENI na ilikuwa haichukui muda atadai tu nirudisheni kwangu na kwake yeye ndio alikuwa mtu wa shughuli sana tu kuanzia kukamua ng'ombe maziwa , KUSHUGHULIKIA KAHAWA , unajua tena babu alikuwa na shamba la KAHAWA kwahiyo kahawa ilikuwa inatengenezewa nyumbani na shughuli nyingine kibao kiasi kwamba ungefikiri angefurahia kukaa na wanae mjini ambapo asingehitajika kufanya chochote kile.

Na BABA yangu kwa mfano huwezi kumfanya akae zaidi ya wiki mbili nje ya TANZANIA ,..
... ataanzatu kutafuta sababu kwanini arudi MOROGORO.Kwa hiyo nachotaka kusema ,...
... naamini ni vigumu kufananisha sana maisha ya VIJIJINI na MJINI kwa kuwa yanaendana pia na hisia na mazoea. Kuna mtu kufanya kazi kwa bidii ni kawaida tu na yaonekanayo ni mazingira magumu ndio mazingira yake tu hata ingawa kuna ukweli kubeba kuni na mtoto mgongoni labda sio juisi kwa kila mtu.

Lakini kuna watu hayo ndio mazoea na ukimleta mjini UGUMU wa MAISHA unazidi kwa kuwa ghafala labda hata aidia kuwa inabidi akodi nyumba tu ya kuishi ni BUGHUDHA TUPU kwa kuwa kazoea angalau hata kama ni KIBANDA cha nyasi lakini ni chake kijijini!:-(

Ni mtazamo tu!

emu-three said...

Sawa kabisa na ugumu wa jambo ni kulitenda...wapo watu wanawalaumu watu masikini kuwa wamejitakia, au maisha ya kijijini wanajitakuwa kuwa na shida, kwasababu gani, HAWAJAWAHI KUKUTANA NA HALI ...WAMEZALIWA MJINI, WAMEKULIA KATIKA MAZINGIRA YA KITAJIRI...Sasa mtu kama huyu utamwambia nini!

Mija Shija Sayi said...

Waishio vijijini wana majukumu zaidi.

mumyhery said...

mimi nafikiri wanawake wa kijijini wana majukumu zaidi asubuhi shamba mchana kupika chakula na akiwa anarudi shamba na mzigo wa kuni labada na ndoo ya maji kichwani bado hajakamua ng'ombe maziwa nk!!!

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana wapendwa kwa kuelimishana!
@ kaka Kitururu bibi bado yupo?nampa hongera zake na wakati anafanya yote hayo babu anakuwa wapi na anafanya nini?

Simon Kitururu said...

Bibi mzaa BABA bado yupo! Babu alifariki hivi karibuni akiwa na miaka 105. Upande wa mama BABU sikuwahi kumuona aliuawa huko Musoma kabla sijazaliwa na Bibi alifia hukohuko MUSOMA miaka ya themanini ingawa yeye nilimuona.

Babu alikuwa kwa sana maswala ya USHONAJI , duka vyama vya ushirika nk. Na alimpata BIBI mtoto wa CHIFU kisa BIBI alienda kupimwanaye gauni la KRISMASI enzi hizo!

SI unajua mafundi cherehan wawezavyo kuwa wanampima kifuani msicha aliyekuja kushonesha sketi isiyo nauhusianao na maeneo yenye nyonyo?:-)

Rachel Siwa said...

hahahhah kaka Kitururu !!umenifurahisha sana, yani hapa sina mbavu hahaha!!najua mafundi kaka. Da Mija naye sijui anapimaje wateja wake!!!!!!

Turudi kwa mada yetu, sasa nimekupata ilivyo kaka, nimefurahi kuona hata babu naye hakuwa mwinyi kama wale wanaocheza bao tuu chakula kikiiva anatumwa mtoto kamwite babu!
pole kwa waliotangulia kwani sote tunapita tuu katika dunia hii,lakini babu ameula wangu miaka 105,si mchezo.Nawe utaridhi kama babu tena utapita miaka hiyo!.

Ahsante sana kaka yangu kwa kutumia muda wako kwangu!!tupo pamoja!!.