Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 21 February 2011

Wanaume na Majukumu!!!!!!!!

Wanaume wanaokaa vijiweni(maskani), wanaocheza bao siku nzima, wanao shinda vilabuni,wapambe na wengine.Je niukosefu wa kazi,mitaji,ubunifu,uvivu,kuchagua kazi au kukimbia Majukumu yao?Wewe msomaji  unamawazo/ushauri gani?.Tuungane pamoja katika kujifunza karibu sana!!!!!!!

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

wengi wanachagua kazi wanasahau kuwa mwanzo ni mgumu.

Mzee wa Changamoto said...

Tatizo la kwanza ni kuwa UNATENGENISHA UMOJA.
Nadhani jibu ni "mchanyato" wa haya uliyoyataja.
"Je niukosefu wa kazi,mitaji,ubunifu,uvivu,kuchagua kazi au kukimbia Majukumu yao?"

Mija Shija Sayi said...

Mzee wa changamoto umemaliza yote, hawa wazee ni wavivu, wanakimbia majukumu, wanachagua kazi na vyote da Rachel ulivyovisema...

emu-three said...

Ukikimbia kazi `unategemea nini' kama sio kumtegemea ndugu! Ni kweli wapo vijana wengu, nguvu kazi, lakini waambie kukaa kijiweni, kujifanya `bongo fleva' ikifika muda wa kula mbio kwa ndugu!
Inasikitisha!

Simon Kitururu said...

Kwanza majukumu ya wanaume ni yapi?

Na kama majukumu ya wanaume ni kuwa tu dume la mbegu tu ndani ya nyumba USIKU,..
..labda yote yaliyotajwa hapa sio uthibitisho wakaao vijiweni..nk., hawafanyi kazi zao za kiume- na labda ni ubunifu wa wafanye nini mchana upelekao WASHINDE WASHINDAVYO kitu kifanyacho waaminio kazi za mwanaume hazina uhusiano na KUONEKANA TU VIJIWENI waone kama kuna mapungufu katika LIFESTYLE zao.

BINADAMU mara nyingi hufanya yanayowezekana maishani na kama kwa kucheza bao siku nzima na rafiki zao bado watakula , watalala na watavaa - huku wana wake nyumbani watimizao MILA na DESTURI ya kuwa walezi wa watoto kama ilivyokuwa kawaida kwenye MILA ZAO -labda ni taratibu tu hizo za siku ya maisha ya watu-hata kama ni utaratibu ambao twautilia mashaka kwa kuwa sio utaratibu wa MILA na DESTURI zetu.

Kwani wajulikanao kwa KUFANYA KAZI kwa bidii KISA WANASHINDA MAKAZINI ndio maana yake wanatimiza MAJUKUMU majumbani mwao na MAISHA yao ndio yamenyoka na yenye furaha?

Na labda malengo tu ya ninini muhimu maishani ndio yafanyayo watu wanyosheane vidole ingawa labda kuna wenye malengo ya kuwa tu na furaha maishani na kuna wagunduao furaha kwa kuishi tu simple bila malengo makubwa wakati bao linachezwa wakati wanasubiria tu siku ya kufa ifike.


Samahani natoka kidogo....

Simon Kitururu said...

Tuendelee...

DESTURI na MILA za watu pia huchangia mirindimo ya nini chaonekana ni kawaida kufanyika ndani ya siku ya mtu.
Na kama umetokea kwenye tamaduni ambazo MWANAMKE kazi yake ni kujiremba tu na kufungiwa ndani ili asije kutana na wanaume wengine unaweza kukuta ni wanawake wenyewe wanaweza kukusuta UKIJIFANYA UNAINGILIA MAISHA YAO na kudai waende kazini au sokoni na kuacha kushinda tu nyumbani - kama tu wanawake wajulikanao kwa kutetea ukeketwaji wa wanawake uendelee kwa kuwa ndio chanzo cha IDENTITY yao ya wao ni nani na wanathamani gani katika jamii na kwa kutokeketwa kidude wanageuka WANAWAKE WASIOFAA KUOA katika jamii.

KUJITAMBUA kwa watu ndio kusababishako kuna waridhikao na yale tudhaniayo WANAKOSEA kwa kuwa kwa KUTAMBUA KWETU kivyetu yetu tunadhani katika maisha ya mwanadamu ndio yanamchango mkubwa ingawa labda ni mchango mkubwa katika kubomoa kuliko hata wa hao waonekanao kama wavivu.

Kwa hiyo WANAUME wanaokaa vijiweni wanaweza kuwa wanaonekana waajabu zaidi kwa WAGENI wa mila hizo.

Na kwenye vilabu kuna VILABU kwa kuwa kuna MTENGENEZA pombe aliyeko kazini , muuzaji pombe aliyeko kazini, malaya kadhaa walioko kazini , mchoma nyama nk. Kwa hiyo kwa kukaa vilabuni twajua ni kitendo kiwapacho watu wengi kazi na kama viuzwavyo ni BIA , Konyagi, SIGARA na nk.- basi na SERIKALI inakula kodi zake humo kwa wakaa vilabuni ambacho ni chanzo kingine cha kodi za serikali zichangiazo uwezekano wa safari za nje za Kikwete.

Na hapa sigusii mchango wa wapambe katika kuhakikisha Dr Slaa maarufu, mchango wa wacheza bao ambao wanajulikana kwa kunywa kahawa na kashata katika zao la kahawa na kipato cha watengeneza kashata na karanga za kukaanga.

Hapo ndipo naweza kuingiza tetesi kuwa wote wafanyayo yadhaniwayo ni UVIVU wanafanya kama tu inawezekana kwa kuwa kama huwezi kuafodi pombe kila siku huwezi kuwa kila siku vilabuni - wakati tukikumbuka washinda kilabuni sio wote wako hapo kunywa NA KUPIGA SOGA TU kwa kuwa kuna wengine wapo hapo kuhudumia wasenge kisenge , malaya , vibaka mpaka wahubiri wa dini .:-(

HITIMISHO kimtazamo wangu:

Wanaume wanaokaa vijiweni , wanaocheza bao siku nzima, wanaoshinda vilabunni, wapambe na wengine - sinauhakika kwao ni ukosefu wa kazi kwa kuwa sina uhakika uwepo wao hapo sio aina ya kazi kwa kuwa kazi inaweza kuwa ni kuwa kibaka wa simu za walevi, naa mini lazima kuna kaubunifu fulani wanako ambako utagundua kama utajaribu kuwaiga kukaa vilabuni kila siku ushuhudie jinsi isivyokuwa rahisi kuongea na walevi kila siku ambao wengine wakilewa kidogo tu huanza kulia, sina uhakika ni wavivu kwa kuwa naamini moja ya shughuli nzito hapa duniani ni kuwa ombaomba na pia naamini kubweteka sio shughuli rahisi kwa kila mtu, ila naamini wanachagua kazi ingawa sina uhakika wanakimbia majukumu yao.

Wakati sikatai kuwa kuna wavivu,...
... hivi UVIVU ni nini?

NI MTAZAMO wangu tu!:-(

Rachel Siwa said...

Ahsante ni sana kwa mawazo/michango yenu,tuendelee kujifunza!
@kaka Kitururu hapa naona mila na Desturi pia zinachangia!

Tuendelee!

Simon Kitururu said...

Mila na DESTURI zinachangia sana! Ingawa BABA yangu anaamini kuna kosa NYERERE alilifanya baada ya UHURU kwa kuwa katika sera za mwanzo hakutilia sana mkazo kazi na hata wasimamizi wa kazi walikuwa wanalinganishwa na MAKABAILA wa kikoloni.


Ilikuwa ni kawaida baada ya uhuru kwa watu kulalamikia wasimamizi wa kazi kuwa ni MAKABAILA. Na majina kama WANYAMPARA na kadhalika yalibobea sana na kwa sehemu za Tanzania ambazo zilizoea kuwa na wafanyakazi wa bidi lakini wahitajio usimamizi ziliathirika sana kwa mitazamo fulani. Kwa hiyo alipoondoka Mkoloni aliyeweza kukuchapa viboko ukikaakaa tu basi huendi tena kazini. Kule UPARENI ambako hata kabla ya UHURU machifu walichimba barabara kwa kusimamia watu wao mpaka huko juu milimani kabisa , watu wakaanza kukaakaa tu nako na ni mpaka MBUNGE aaahidi siku hizi hata zahanati ambavyo zamani ilikuwa watu wanafanya wenyewe.

Nachojaribu kusema ni kuwa MILA na DESTURI na pia kukosa uongozi ambao una DIRA na MALENGO ya nini watu wafanye na unaosimamia watu kuhusu nini cha kufanya waweza kuwa umeongezea tatizo pia.

Hili ni nyongeza kwa niliyobwabwaja hapo kwenye komenti ya juu

Mzee wa Changamoto said...

Kitururu wa Mkodo

DUH!!!!!!!!!!

Rachel Siwa said...

@kaka Kitururu hii sasa ndiyo ya punda haendi bila kiboko!
@kaka Mubelwa naona umeguswa!.
Tuendelee!!!!!!!!!