Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 25 August 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU.


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015



Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015


Monday 24 August 2015

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHE, WILSON MASILINGI AWASILI WASHINGTON DC.


    Balozi mpya atakayeiwakilisha Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi akiwa amefuatana  na Mkewe  Marystella Masilingi pamoja na mwanae Nelson Masilingi wawasili kituoni kwake Washington DC, awali ya hapo Mhe Wilson Masilingi alikua Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kutua Washington DC akisalimiana na atakayekua dereva wake Virgilio Paz maarufu kama Bong.
Safari ya Mheshimiwa Balozi pamoja na mama ikianza kuelekea Hotelini kwake ambapo atapumzika kwa muda kabla ya kuingia nyumbani kwake Bethesda ,Maryland.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kufika Hotelini kwake akisaidiwa mlango na Afisa wa Ubalozi Swahiba Habib Mndeme.
Mhe Balozi Wilson Masilingi akisalimiana na baadhi ya Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki pichani ni mmoja wa Maafisa Andrew Mugendi Zoka.
Mama Marystella Masilingi naye hakua nyuma kusalimiana na baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.
Mhe Wilson Masilingi akiwa na bashasha tele kuona kwa jinsi gani Tanzania House walivyo na upendo na kuonyesha ushirikiano wao wa dhati kwenye tukio hilo muhimu.
Mhe Wilson Masilingi alifuatana na Mtoto wake Nelson Masilingi.
Maafisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme pamoja na Alfred Swere wakiteta jambo kidogo.
Mhe Balozi Wilson Masilingi pamoja na Familia yake kwenye picha  ya pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta.
Mhe Wilson Masilingi alipata fursa kidogo kutembelea mitaa ya jijini akiwa ameongozana na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta

Baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Tanzania House wakiwa Hotelini alipofikia Mhe Wilson Masilingi.

   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI KWA PICHA ZAIDI UNGANA NASI PUNDE.


Sunday 23 August 2015

Muendelee vyema na Jumapili hii;Burudani-Kinondoni Revival Choir Twalilia Tanzania,Solomon Mukubwa Mfalme Wa Amani na nyingine.....

Nimatumaini yangu wote mpo salama wasalimini na Mungu yu pamoja nanyi
Muwe na wakati mwema......
1Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama isingekuwa hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi. 3Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi.4Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda.”

Neno La Leo;Yohana 14:1-31

Yesu njia ya kwenda kwa Baba

5Thoma akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda, tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?” 6Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu. 7Ikiwa mnanijua mimi, mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua, tena mmekwisha mwona.”
8Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, nasi tutatosheka.” 9Yesu akamwambia, “Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: ‘Tuoneshe Baba?’ 10Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambieni siyasemi kwa mamlaka yangu; Baba aliye ndani yangu anafanya kazi yake. 11Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya. 12Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi, kwani ninakwenda kwa Baba. 13Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.

Roho Mtakatifu
15“Mkinipenda mtazishika amri zangu. 16Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele. 17Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.
18“Sitawaacha nyinyi yatima; nitakuja tena kwenu.19Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona tena, lakini nyinyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai. 20Siku ile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu. 21Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
22Yuda (si yule Iskarioti) akamwambia, “Bwana, itawezekanaje wewe kujidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” 23Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye. 24Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
25“Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi, 26lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni.
27“Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike. 28Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi. 29Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini. 30Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana mtawala wa ulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu; 31lakini ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampenda Baba, na ndiyo maana nafanya kila kitu kama Baba alivyoniamuru. Simameni, tutoke hapa!
Bible Society of Tanzania










"Swahili Na Swahili" Mungu ibariki Tanzania/Watanzania,Africa. 

MISS TANZANIA USA: MAJAJI WAMPOKONYA USHINDI DOREEN PANGA NA KUMVIKA TAJI AEESHA KAMARA NJE YA UKUMBI


Aeesha Kamara sasa ndiye mshindi wa Miss Tanzania USA pageant
  Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Doreen Panga baada
ya kuvikwa taji la Miss Tanzania USA 
Miss Africa 2014-15 akipata picha ya
pamoja na Aeesha Kamara baada kuvikwa taji na maamuzi ya majaji ambao
hawakukubaliana na mshindi aliyetangazwa kwanza.

Doreen Panga kutoka New York usiku wa Aug 22, 2015, alivuliwa taji la Miss
Tanzania USA na majaji wa shindano hilo nje ya ukumbi taji alilolivaa kwa
dakika 45 na kumvika Aeesha Kamara wa Maryland kwa madai kwamba Doreen
Panga hakua chaguo lao.

Majaji hao Peter Walden, Elaine Roecklein, Tee Thompson, Bertini Huemegni,
Tina Semiti Magembe, Mayor Mlima, Uche Ibezzue wakiongozwa na Michael Lewis
McBride kwa pamoja walikataa kukubaliana na mshindi aliyetangazwa na
kufanya kikao nje ya ukumbi wakati watu wakiondoka ondoka nao
wakisikitishwa na maamuzi ya kutangazwa mshindi huku na kama majaji
wangekaa kimya basi masahabiki wa shindano hilo wangepelekea lawama kwa
majaji.Jaji Dr. Secelela Malecela japo kwamba alipingana na Doreen Panga
kutangazwa mshindi lakini hakukubaliana na majaji wenzake Doreen avuliwe
taji na apewe Aeesha Kamara aliyekua chagua la majaji wengine, yeye
alipendekeza kwa kua kosa lishafanyika waachane nalo wahakikishe mwakani
halitokei tena. Wazo lake lilipingwa na majaji wenzake pale pale.

Shindano hilo lilianza vizuri kwa nyimbo za Taifa za Marekani na Tanzania
zilizoongozwa na watoto Brian akiwa kwenye kinanda na dada yake Briana
akiwa kwenye kipza sauti,

Baadae walitambulishwa ma miss wa
kesho watoto wa DMV wenye umri wa miaka 9 na 12 na baada ya hapo waliingia
malikia wenyewe huku wakisindikizwa na wimbo wa Diamond wa mdogo mdogo na
baadae kujitambulisha kwa majaji.

Washiriki wa miss Tanzania USA
walikua Rechel Mujaya kutoka Atlanta, Joyce Mkapa toka New York, Doreen
Panga toka New York, Aeesha Kamara toka Maryland, Aziza Gama toka Maryland
na Brenda Panga toka New York. Washiriki walianza shindano kwa kujielezea
wakifuatia na shindano la vipaji na baadae kujibu maswali ya majaji.

Pia katika shindano hilo kulikua na burudani mbalimbali akiwemo Mr Tz
ambaye aliitambulisha singo ya wimbo wake mpya uliotoka mwei uliopita,
Wasanii wengine walikua kutoka Ivory Coast na Jamaica.

Baada ya hapo ndipo kulitangazwa mshindi kuwa ni Doreen Panga ushindi ambao
waliowengi hawakukubaliana nao wakiwemo majaji na mkurugenzi na mwanzilishi
wa Miss Africa USA ambao walisikika wakinong'ona huku wakiulizana imekuaje
bila kupata majibu.

Wakati majaji wakiwa nje ya ukumbi wakitafakali imekuaje tumeacha shughuli
zetu tumekuja hapa tunatoa maamuzi sasahihi halafu mtu anatuzarau maamuzi
yetu. Mashabiki walianza kuondoka baada ya shindano hilo kufikia ukingoni
na wengine wakimtupia lawama wandaaji kwa kuvurunda shindano.

Majaji walipokua wakijadiliana wafanye nini walikuja na kuazimia kwa kauli
moja  lazima wampe ukweli mwandaaji kwamba hawakufurahika na
kilichotokea ndani ya ukumbi. Mwandaaji wa Miss Tanzania USA aliitwa ndipo
majaji wakatoa dukuduku lao na mwandaaji akajitetea kwamba mshindi amesema
hataweza kushiriki mashindano hayo na ameamua kumpa taji mshindi wa pili
ambaye alikua Aziza Gama, baada ya kusikia hayo majaji walimwita Doreen
Panga na kumuuliza sababu yake ya kutaka kumvisha taji mshindi wa pili ni
nini yeye akawajibu ni kutokana na kazi zangu ninazofanya hospitali
sitaweza kupata muda wa ushiriki kwa hiyo badala yake nitampa taji mshindi
wa pili.

Majaji walishindwa kuafikiana na Doreen na kuamua kupiga kura upya ndipo
wote kwa pamoja kasolo Dr Secelea Malexela walimchagua Aeesha Kamara kwamba
ndiye aliyestahiki kuvigwa taji na ndio aliyekua chaguo lao.

Doreen Panga akavuliwa taji na kuvikwa Aeesha Kamara huku Doreen akionesha
kutokubaliana na majaji lakini wao ndio waamuzi wa mwisho na kitendo
walichokifanya ni kulinda heshima yao.

Sasa Miss Tanzania USA ni Aeesha Kamara.






Saturday 22 August 2015

Mshumaa wa wiki.....Barry White


 Mshumaa wa wiki ni kipengele kinachozungumzia kuhusu msanii ama kundi la muziki wa zamani katika kipindi cha Mishumaa ya Kale

Kipindi hiki hukujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka 1 usiku kwa saa za Marekani ya Mashariki

Kinatayarishwa na kurushwa na Vijimambo Radio na Kwanza Production, kwa ushirikiano na NesiWangu Media

Tuesday 18 August 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Agosti 17 2015


Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Katika kipindi hiki utasikia mjadala wetu na wageni Jeff Msangi toka Toronto Canada na Darmatus Nambai aliyehudhuria studio kuhusu DEMOKRASIA na MABADILIKO kuelekea uchaguzi nchini Tanzania

KARIBU

Tuesday 11 August 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu wiki hii (Aug 10, 2015)


Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tulijadili kuhusu kung'atuka uongozi kwa Prof Ibrahimu Lipumba na pia kukua kwa ufuasi kwa mgombea uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa.

Pia, hotuba ya Zitto Kabwe huko Iringa, na mengine mengi

Ungana na Dj Luke Joe (wa hapa), Rose Chitallah, Shamis Abdul (wa hapa) na Mubelwa Bandio (wa hapa) toka Kilimanjaro Studio, Beltsville Maryland na Jeff Msangi (msome hapa) kutoka Toronto Canada kujadili haya.

Pia, kulikuwa na simu za wasikilizaji kadhaa

KARIBU

Monday 10 August 2015

MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY


Na Mubelwa T Bandio

MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa. Na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.

Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.

Na...

Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.

Leo, Agosti 10,  ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.

UKWELI ni huu...

Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako.

Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.

Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa. Tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.

Kama nilivyowahi kuandika, kuwa UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO (rejea hapa)

Maishani, nimehudhuria BIRTHDAY(s) na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia TAMATI yetu.

Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika HAPA Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.

Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali.

Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.

Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana. Si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.

Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada. Na naamini katika hilo.

Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai. Siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni HII

Lakini leo wasoma niandikalo.

NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"

Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.

Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo. Na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.

Na ndio maana nikasema, MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY

Anyway!

Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.

Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa.

Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.

Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)

Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa

Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani)

Hahahaaaaaaaaaaaaaa

Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.



Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.

 

Sunday 9 August 2015

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA NEW YORK NCHINI MAREKANI.


Mchungaji Butiku akiongoza misa ya shukurani na arubaini ya
marehemu Mzee Samuel Luangisa iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 8,
2015 Mount Vernon, New York na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki
kutoka kila pembe ya Marekani.
Mrs Luangisa, mke wa marehemu akifuatilia misa.


Wanafamilia wakifuatilia misa.


Wajukuu wa marehemu wakifanya onesho la kumenzi babu yao.


Mtoto wa marehemu Mao Luangisa akitoa salamu za shukurani.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York Hajji Khamis akiongea
machache huku akisisitiza upendo na mshikmano kwenye Jumuiya za
Watanzania hususani zile zilizopo nje ya Tanzania kwani kwa kufanya
hivyo Jumuiya zitakua imara.


Mchungaji Butiku akiongoza misa.


Wakati wa maakuli.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Thursday 6 August 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AONDOKA RASMI MAREKANI KURUDI TANZANIA.


 Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.




                               Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.

 Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.

 Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.

               Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa  pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.

                        Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika hatua za mwisho za usajili.

                           Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika

Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.

Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.

 Kwa pamoja tunasema Safari Njema na Ubarikiwe Sana Balozi Mulamula daima tutakukumbuka.

                    PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

Tuesday 4 August 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATINGA NDANI YA STUDIO YA KILIMANJARO


 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik

 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa