Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 30 November 2013

[AUDIO]: Kuzagaa kwa silaha za moto na kuongezeka kwa mauaji Tanzania‏


Picha kwa hisani ya thehabari.com
Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu.

Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake .

Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.


Ungana
na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia
tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya
waTanzania wengi.



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Wednesday 27 November 2013

Jikoni Leo;[Street food]Chipsi Vumbi Na Hapa kwetu!!!!!!!


Hapa tunapokumbukia Chipsi za Nyumbani, Ma binti zangu hupenda sana Chipsi Mayai[ZEGE]Na sasa wanapika wenyewe kama unavyoona hapo juu,Nyama Choma Baba anawasaidia...

Waungwana;Jikoni Leo Mtaani na Kwa Da'Rachel..
Vipi Chipsi Vumbi/za Mitaani Zina Raha gani? Na Karaha Gani?

Kuna mtu hajawahi kula Chipsi hizi?

Jee wewe uliyekula/Unayekula Wapi KIJIWE bomba Cha Chipsi upendacho?

Pale Dar,Ilala  Kulikuwa kwa Ndago,Barafaa....
Pale Iringa,Kulikuwa kwa Baba Nusa...


Hizi ni Chache tuu nawe Waweza Kuongezea....





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Monday 25 November 2013

Sunday 24 November 2013

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Here I am to Worship[Playlist]!!!!

Wapendwa;Muwe Na J'Pili yenye Baraka,Amani,Upendo na Furaha...
Lakini nafsini mwangu nalikusudia hivi,nisije kwenu tena kwa huzuni...
.Maana mimi nikiwatia huzuni,basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishwaye nami?
Neno La Leo;2Wakorintho:2:1-11.


"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday 23 November 2013

Wa-Africa Na Mitindo Mchanganyiko!!!!!





Mhhhh..Mengi sina..ni Wa-Afrika na Mitindo...mimi naiita Mitindo TATA..
Vipi Inavalika? Si wanasema Wanawake tunavaa mavazi yanayo fanana na Yao..nawao jee?......haya na Nywele za dada kama hivyo.

Kuona Zaidi nifuate;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Miaka 50 tangu kuuawa kwa Rais John F Kennedy‏



 

Ijumaa wiki hii,
Marekani imeadhimisha nusu karne tangu kuuawa kwa Rais wa 35 wa taifa
hilo, John F Kennedy aliyeuawa Novemba 22, 1963 alipokuwa akisafiri kwenye gari la wazi jijini Dallas

Rais John F Kennedy akiwa katika gari la wazi muda mchache kabla hajauawa kwa risasi. Pembeni yake ni mkewe na mbele yake ni aliyekuwa Gavana wa Texas John Bowden Connally, Jr.ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo
Kwa wiki nzima, kumekuwa na shughuli mbalimbali kukumbuka tukio hili lililoshitua wengi nchini humo. Mambo mengi yametendeka. Vitabu vipya vimeandikwa na watu wamezungumzia kuuawa kwa Rais huyo pamoja na ufuasi alioacha kwenye uongozi mpaka sasa. Na kama ilivyotegemewa, Kengele ziligongwa, maua yaliwekwa kwenye kaburi, bendera zilipepea nusu mlingoti na nyimbo mbalimbali ziliimbwa

Rais Barak Obama, aliadhimisha kumbukumbu
hizo Jumatano wiki hii kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais
Kennedy na pia kutoa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali akiwemo Rais
mstaafu Bill Clinton, mwanahabari maarufu Oprah Winfrey na wengine 14.

Rais Barack Obama (wa pili kulia) akiwa na mkewe Michelle, Rais mstaafu Bill Clinton (wa tatu kulia) na mkewe Hillary Clinton wakitoa heshima mbele ya kaburi la JFK jumatano wiki hii.


Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 23, 2013




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Friday 22 November 2013

Jikoni Leo;African Market-Nima Market in Accra, Ghana!!!!




Waungwana;Jikoni Leo, Tupo sokoni  Ghana..haya tuangalie mahitahi...
Kuna vingine wewe huviwezi kula lakini wengine wanaweza.

Nini kimekuvutia?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday 20 November 2013

Ana kwa Ana na Astronaut Dr Donald Thomas‏


Karibu katika mahojiano kamili na Dr Donald Thomas.

Mhandisi na mwanaanga wa Marekani

 Katika mahojiano haya, Dr Thomas anaeleza historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi.

Ilimchukua miaka 9 tangu ajaribu kwa mara ya kwanza mpaka achaguliwe, na katika miaka hiyo, alituma maombi mara nne.

Ili kuongeza nafasi yake kufanikiwa akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo.

Lakini aliamini katika atendalo.

Pia ameeleza maandalizi wanayofanya na mafunzo wanayopitia kuanzia wanapochaguliwa mpaka
wanapoenda kwenye mission hizo, hisia na uoga wake siku ya kwanza alipanda
space shuttle. Amezungumzia safari nzima na shughuli kuanzia
wanavyoondoka mpaka wanavyofika angani pamoja na changamoto za kuishi kwenye
orbit. Kuanzia kupika mpaka kutumia choo. Na pia, namna alivyopokea taarifa za
kulipuka kwa space shuttle Columbia. Shuttle aliyoitumia mara tatu kati ya nne
alizokwenda kwenye orbit.

Baada ya miaka 20 aliyofanya kazi kama mwanasayansi wa NASA, na safari nne kwenye Orbit, akastaafu na sasa ni Mkurugenzi wa Willard Hackerman Academy katika chuo kikuu cha Towson hapa Maryland ambapo anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho

Nilipata fursa ya kuhojiana naye mwaka 2011




Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Monday 18 November 2013

Kipindi Maalum Mazishi ya Bi.Martha Shani Tanzania




Tunawaletea kipindi maalum cha Mazishi ya mpendwa na kipenzi chetu Bi. Martha Shani aliyefariki ghafla nchini Marekani na kuja Kuzikwa nyumbani Tanzania. Katika Kipindi hiki utaona matukio mbalimbali katika safari ya mwisho ya Bi. Martha Shani.

"Swahili Na Waswahili";Mhhh...Pole sana kaka Alex,  Familia,Ndugu,Jamaa na Marafiki.

Ulale kwa Amani da'Martha Shani.


Dr Donald Thomas alipohojiwa na Jamii Production‏


Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE, wiki hii utasikia mahojiano niliyowahi kufanya na Dr Donald Thomas. Mhandisi na mwanaanga wa Marekani.

 Ilimchukua miaka 33 kutimiza ndoto zake za kuelekea kwenye Orbit. Na baada ya kwenda kwenye Orbit mara nne, akastaafu na sasa anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho

Nilipata fursa ya kuhojiana naye ambapo alieleza mengi mema



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 17 November 2013

Tumalizie J'Pili hii Vyema;Burudani-Kutoka,One Nation Gospel Na Gisubizo Choir!!!


Tumalizie J'Pili hii vyema.. Iwe Yenye Neema,Baraka,Upendo na Amani....BWANA asipojenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.........

Neno La Leo;Zaburi:127:1-5





"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana

Saturday 16 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Hatari ya bunduki za kuchapishwa nchini Marekani‏





Bunduki ya plastiki iliyotengenezwa kwa mashine ya 3D ikifyatua risasi wakaati wa majaribio

Photo credits: Screenshot from ATF Video


Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.



Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.

Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha.

Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.


Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)



Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC

Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 16, 2013



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Friday 15 November 2013

Wanawake Na Mitindo Ya Nywele!!!!

Waungwana;Wanawake na Mitindo Ya Nywele...
Hivi ni kweli Nywele ndiyo pambo kubwa kwa Mwanamke?
Kujua/Kuona Zaidi nifuate huku;
http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday 14 November 2013

HUYU NA YULE: Mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.‏


Katika kipengele cha HUYU NA YULE, wiki hii tuliungana na VIJANA WATATU


Liberatus Mwang'ombe, Peter Walden na Ally Badawy kujadili MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.


Ali Badawi (kushoto), Peter Walden (kati(na Liberatus Mwang'ombe (kulia) wakiendelea na mjadala ndani ya studio za Jamii Production

Ulikuwa ni mjadala mrefu na huru ambao ulikuwa na mengi ya kufunzana


Karibu uungane nasi


Wakati tukimalizia mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE, Peter Walden alimuuliza Liberatus Mwang'ombe swali kuhusu kufunguliwa kwa matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi.

Liberatus ni Katibu Mkuu wa Tawi la Chadema hapa Washington DC

Hapo pakawa na ka-mjadala kadoooogo ambako hata Ally Badawy na mwongozaji wa kipindi Mubelwa Bandio wakachangia.

Karibu usikilize



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Tuesday 12 November 2013

Mahojiano na mwanamuziki Dekula Kahanga a.k.a Vumbi‏


Hivi karibuni Jamii Production ilipata nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu katika ucharazaji gitaa nchini Tanzania Dekula Kahanga aliye maarufu kwa jina la Vumbi.
Mahojiano haya "mepesi" yamegusa mambo mbalimbali kuhusu maisha yake kimuziki
Amehojiana na Jamii Production akiwa Sweden yalipo makazi yake ya sasa
KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 10 November 2013

Muendelee na J'Pili hii Vyema;Burudani Mchanganyiko-Hear My Cry Oh Lord,Blessed be the Name of the LORD,Na....!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu  J'Pili inaendeleavyema...
MUNGU ni Pendo.Mimi nakupenda sana wewe uliyepita hapa/Unayepita hapa na Woooote....Muwe na Amani,Furaha na Upendo wa kweli...
Wapenzi na Mpendane;kwakuwa pendo latoka kwa MUNGU, na kila apendaye amezaliwa na MUNGU,naye anamjua MUNGU.

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Yohana:4:7-21











"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Saturday 9 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Athari za vita baada ya kumalizika mapigano‏


Wakati vita ya Congo
ikionekana kuelekea ukingoni, bado tunakumbushwa kuwa athari za vita
katika nchi mbalimbali huendelea kuwaathiri wahusika na hasa wananchi wa
nchi hizo kwa miaka mingi baada ya kumalizika kwa vita hivyo.

Baadhi
ya athari huwa wazi sana. Mfano ni majengo yaliyoharibika wakati wa
mapigano, watu wanaouawa wakati wa mapigano na hata uchumi unaozorota
kutokana na watu kutofanya kazi wakati wa mapigano hayo.

Lakini pia kuna athari ambazo hazionekani ama kutopewa kipaumbele machoni mwa watu wengi baada ya vita hivyo.

Hivi karibuni, waMarekani wamekumbushwa kuhusu hili

Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).



Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 9, 2013



*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

"MISUKOSUKO" KUTOKA KWA NDEGE 3


Jina la Nyimbo ni MISUKOSUKO.
Jina la kundi  ni NDEGE 3
Waimbaji ni Khadija Mnoga (Kimobitel) , Paulyne Zongo na Joan Matovolwa tumefanya featuring na Grayson Semsekwa.

  Audio imeshatoka na sasa VIDEO.




Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joana Matovolwa.Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo linalojulikana kwa jina la NDEGE 3

Friday 8 November 2013

Mapenzi Na Wapenzi; [Love Story]Jee Ulimpata wapi huyo Mwenza wako?


Waungwana;Safari ya maisha huanzia mbali sana mpaka watu Kuchumbiana na  wakaamua Kufunga Ndoa/kuishi Pamoja kama Mke na Mume..Pia kila mtu/watu wanapo walipoanzia.
 Jee wewe ulianzia wapi?
 Hahahah..huyo Mchumba wako,Mkeo/Mumeo ulimtoa/Muona/kutana naye wapi?...
Ulitafutiwa,Mlikutana Njiani,kwenye basi,kazini,Chuoni au....?
Jee Unaushauri gani kwa wanaotafuta Wenza/Wachumba/Mke-Mume?






"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Tuesday 5 November 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Dj Luke Joe‏


Dj Luke akiwa studio na Mubelwa Bandio wa Jamii Production
Karibu katika mahojiano na Dj mkongwe kutoka Tanzania na
mmiliki wa blog ya Vijimambo Lucas Mkami a.k.a Dj Luke Joe


Dj Luke ambaye makazi yake kwa sasa ni Maryland nchini Marekani ameeleza mengi kuhusu kazi zake hizi.

Katika mahojiano haya, ameeleza historia yake katika kuchezesha muziki, aliyemvutia kuingia katika kazi ya uDj, mafanikio ya Dj, changamoto zake, ku-blogu na mengine mengi.


Karibu Uuungane nasi



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Monday 4 November 2013

Kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production......FAMILIA ZA KAMBO (sehemu ya mwisho)‏





Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema
Moja ya sababu zilizotusukuma kujadili masuala kuhusu FAMILIA ZA KAMBO ni takwimu zilizopo hivi sasa kuhusu familia hizi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.blendedandbonded.com, hapa Marekani
• 41% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka
• 60% ya ndoa za pili huishia kwenye talaka
• 73% ya ndoa za tatu huishia kwenye talaka
• 45% ya wanawake na 50% ya wanaume wataoa tena ndani ya miaka mitano ijayo
• 50% ya ndoa za marudio huhusisha watoto wa mahusiano yaliyopita walio chini ya miaka 18
•Ndoa 2100 huanzishwa kila siku nchini Marekani
• 42% ya watu wazima wana uhusiano wa kambo. Hii inajumuisha mzazi wa kambo / mtoto wa kambo ama ndugu wa kambo
Kwa idadi ya Marekani, takwimu hizi zinamaanisha kuwa familia za kufikia zinahusisha watu wazima wapatao milioni 95.5
•Kuna baba wa kambo milioni 16.5
•Kuna Mama wa kambo milioni 14.
•Wataalamu
wa mahusiano wanasema kuwa ndoa za kufikia ndio zitakuwa ndoa zenye
umaarufu na nyingi zaidi nchini Marekani na kuwa, kutokana na kukosekana
kwa taarifa sahihi kuhusu familia za kufikia, familia hizi mara nyingi
zimejikuta kwenye migogoro na mafarakano.
Nasi tuko hapa kujaribu kuepusha hilo kwa kushirikiana nanyi katika kile tunachoweza kuelimisha kudumisha ndoa hizo.
Ungana nasi katika sehemu hii ya mwisho ya MADA hii.




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 3 November 2013

Nawatakia J'Pili Njema yenye Amani;Burudani-bado tupo ,Kijitonyama Choir,Ee Baba,Jehova Baba wa Upendo na...!!!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili hii iwe njema..Na usikate tamaa MUNGU yupo na Anatenda/Ametenda/Atatendaaa.. Jehova Baba wa Upendo..Eeee Baba kama si wewe Ningekuwa/Tungekuwa/Ungekuwa Wapi?...Mhhh Acheni MUNGU aitwe MUNGU Bwaana!!!!!

Watulizeni mioyo,Watulizeni mioyo,Watu wangu asema MUNGU wetu....
Neno La Leo;Isaya:40:1-31;

Bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai;watapiga mbio,wala hawata choka;watakwenda kwa miguu,wala hawatazimia.






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Saaana.

Saturday 2 November 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Oliver N'goma-Bane na Nyimgine..!!!






Waungwana "Chaguo La Mswahili Leo" Ni Oliver N'goma...
Mhh..wewe unakumbuka wapi na ilikuwaje/ulikuwa wapi wakati huo?
Maneno Meengi sina nasikiliza kutoka kwako..

Twende Sote sasaaa......





Swahili Na Waswahili Pamoja Sana.