Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Habari/Matukio. Show all posts
Showing posts with label Habari/Matukio. Show all posts

Tuesday 22 April 2014

Mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu Bunge maalum la Katiba‏





Karibu katika mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.
Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania.
Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Saturday 12 April 2014

[AUDIO]. DAKIKA 90 ZA DUNIA: Maadhimisho ya Kwibuka20, Washington DC‏


 Wiki
kama hii, miaka 20 iliyopita, nchi ya Rwanda ilishuhudia kuanza kwa
mauaji ambayo kwa siku 99 zilizofuata, yaliacha historia mbaya na ambayo
itaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Ndani ya siku 100, watu wanaokadiriwa kufika milioni 1 waliuawa katika mauaji ya kimbari.
Miaka
20 baadaye (mwaka huu), dunia nzima imeungana na Rwanda kukumbuka kile
ambacho wengi wanaona kuwa kilitokea na kuachwa kuendelea kutokana na
Jumuiya ya kimataifa kutoingilia kati na kutoa msaada muafaka kwa wakati
muafaka.
Kumekuwa na matukio mbalimbali kukumbuka mauaji ya kimbari
ya Rwanda ambayo yamefanyika duniani kote, Kutoka Kigali Rwanda mpaka
hapa Dar-Es Salaam na hata huko Washington DC.



Hii ni sehemu ya
ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Monday 7 April 2014

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Mauaji kwenye kambi ya jeshi Fort Hood‏

Jenerali Mark Milley, Kamanda wa Fort Hood akizungumza na waandishi wa habari  
Wiki iliyopita, nchi ya Marekani ilikumbwa na mauaji mengine yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi huko Fort Hood, Texas.

Jumatano Aprili 2, askari mmoja wa Jeshi la nchi hiyo, Ivan Lopez ambaye
inasemekana alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo, aliwafyatulia
risasi na kuwaua wanajeshi wenzake 3, kujeruhi 16 kabla hajajigeuzia
bastola na kujiua

Mauaji haya, yanarejesha kumbukumbu ya mauaji
makubwa kabisa kutokea kwenye kambi za jeshi nchini humo, yaliyotokea
kwenye kambi hiyohiyo takriban miaka 5 iliyopita.



Hii ni sehemu ya
ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Saturday 22 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90: Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani‏

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011.
Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za
kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi
na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu
kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua
macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama
miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.


Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network
ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya
dunia.



Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea
tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana
wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.


Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90
ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es
Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30
AM).

Saturday 15 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Mfungwa aliyekuwa akisubiria KIFO aachiwa huru‏


Picha iliyopigwa na mwanasheria wake, ikimuonyesha Bwn Ford, siku ya kwanza kama mtu huru baada ya miaka 30 jela kwa kosa ambalo hakufanya. Photo Credits: theatlantic.com
Wiki hii, mmoja wa wafungwa nchini Marekani, ambaye alikuwa kwenye orodha ya wanaosubiri kunyongwa kutokana na kuhukumiwa kifo kwa mauaji  aliyotuhumiwa kufanya mwaka 1984 aliachiwa huru baada ya Jaji kukubali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa ni yeye aliyeshiriki mauaji hayo.

Sasa, mfungwa huyu atalipwa dola 25,000 kwa kila mwaka aliotumikia kifungo hicho, lakini, kwa mujibu wa sheria ya Louisiana, kiwango cha juu anachoweza kulipwa ni dola 250,000

Ina maana, atalipwa kwa miaka 10 tu kati ya 30 aliyokaa gerezani

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Saturday 22 February 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?‏


Photo: Mobile88.com

Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya
WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu
bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi
kifupi tu.

Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano
ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni
19 kununua WhatsApp.

Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Tuesday 3 December 2013

Kifuatacho Jamii Production...Fatuma Matulanga na Evans Mhando‏



Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE  wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa
wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga
aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja
tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana

Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo

1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA

2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?

3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?

4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?

5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?

6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)

Na mengine mengi

Usikose kutembelea mtandao huu siku ya Jumatano ili kusikiliza mahojiano kamili

Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma
Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la
Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China

Saturday 30 November 2013

[AUDIO]: Kuzagaa kwa silaha za moto na kuongezeka kwa mauaji Tanzania‏


Picha kwa hisani ya thehabari.com
Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu.

Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake .

Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.


Ungana
na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia
tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya
waTanzania wengi.



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Saturday 23 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Miaka 50 tangu kuuawa kwa Rais John F Kennedy‏



 

Ijumaa wiki hii,
Marekani imeadhimisha nusu karne tangu kuuawa kwa Rais wa 35 wa taifa
hilo, John F Kennedy aliyeuawa Novemba 22, 1963 alipokuwa akisafiri kwenye gari la wazi jijini Dallas

Rais John F Kennedy akiwa katika gari la wazi muda mchache kabla hajauawa kwa risasi. Pembeni yake ni mkewe na mbele yake ni aliyekuwa Gavana wa Texas John Bowden Connally, Jr.ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo
Kwa wiki nzima, kumekuwa na shughuli mbalimbali kukumbuka tukio hili lililoshitua wengi nchini humo. Mambo mengi yametendeka. Vitabu vipya vimeandikwa na watu wamezungumzia kuuawa kwa Rais huyo pamoja na ufuasi alioacha kwenye uongozi mpaka sasa. Na kama ilivyotegemewa, Kengele ziligongwa, maua yaliwekwa kwenye kaburi, bendera zilipepea nusu mlingoti na nyimbo mbalimbali ziliimbwa

Rais Barak Obama, aliadhimisha kumbukumbu
hizo Jumatano wiki hii kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais
Kennedy na pia kutoa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali akiwemo Rais
mstaafu Bill Clinton, mwanahabari maarufu Oprah Winfrey na wengine 14.

Rais Barack Obama (wa pili kulia) akiwa na mkewe Michelle, Rais mstaafu Bill Clinton (wa tatu kulia) na mkewe Hillary Clinton wakitoa heshima mbele ya kaburi la JFK jumatano wiki hii.


Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 23, 2013




--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Saturday 16 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Hatari ya bunduki za kuchapishwa nchini Marekani‏





Bunduki ya plastiki iliyotengenezwa kwa mashine ya 3D ikifyatua risasi wakaati wa majaribio

Photo credits: Screenshot from ATF Video


Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.



Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.

Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha.

Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.


Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)



Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC

Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 16, 2013



Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Saturday 9 November 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Athari za vita baada ya kumalizika mapigano‏


Wakati vita ya Congo
ikionekana kuelekea ukingoni, bado tunakumbushwa kuwa athari za vita
katika nchi mbalimbali huendelea kuwaathiri wahusika na hasa wananchi wa
nchi hizo kwa miaka mingi baada ya kumalizika kwa vita hivyo.

Baadhi
ya athari huwa wazi sana. Mfano ni majengo yaliyoharibika wakati wa
mapigano, watu wanaouawa wakati wa mapigano na hata uchumi unaozorota
kutokana na watu kutofanya kazi wakati wa mapigano hayo.

Lakini pia kuna athari ambazo hazionekani ama kutopewa kipaumbele machoni mwa watu wengi baada ya vita hivyo.

Hivi karibuni, waMarekani wamekumbushwa kuhusu hili

Hii
ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA
DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).



Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 9, 2013



*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"