Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 29 September 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 28 2015 (FULL)


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hiki ni kipindi kilichosikika Septemba 28, 2015

Kutoka Tanzania tuliungana na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea ubunge jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA

Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, na kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani

KARIBU

Sunday 27 September 2015

Muwe na Jumapili Njema;Burudani-2015 Ambassadors of Christ Choir-Siku zakilio zimepita,Nimekupata Yesu,kesheni kaombeni,Yanatisha sana na ....(New video 2015)

Wapendwa;Muendelee vyema na jumapili hii,
Amani,Busara,Hekima,Heshima na Utu vikatawale siku zote!!


(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yoh 6:1-14)
13Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini. 14Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.
15Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.” 16Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni nyinyi chakula.” 17Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.” 18Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.” 19Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Neno La Leo;Mathayo14;1-36

Kifo cha Yohane Mbatizaji
(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9
)
Yesu anawapa chakula watu zaidi ya elfu tano
(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yoh 6:1-14)

Yesu anatembea juu ya maji
(Marko 6:45-52; Yoh 6:15-21)
Yesu anaponya wagonjwa kule Genesareti
(Marko 6:53-56)
Bible Society of TanzaniaShukrani;Rwanda Tube
"Swahili na Waswahili"Mbarikiwe sana.

Wednesday 23 September 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Sep 21 2015


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hii
ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo
mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo
Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York.

Kutoka Tanzania tuliungana na Richard Kasesela

Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York.
Kutoka Tanzania tuliungana na Blogger Mr Verbs wa www.habarika24.blogspot.com, pia kulikuwa na Dr Patrick Nhigula, Hajji Khamis na Emil Mutta na Kennedy

Monday 21 September 2015

SWAHILI FEST COMMUNITY PICNIC YAFANA DMV


Mshereheshaji Tuma akielekeza jambo kwenye tamasha la Swhili Fest lililofanyika siku ya Jumapili Septemba 20, 2015 Bladensburg, Water Front iliyopo jimbo la Maryland nchini Marekani. Picha na Vijimambo Blog/ Kwanza Production.
Patrick Kajale mmoja ya waratibu wa swahili fest akipata picha ya pamoja na mmoja ya watoto walioshinda kucheza wimbo wa Bongo Flava. Waratibu wengine ni Amri Maliyatabu, Seif Ndossa na Frank Kajale.
Patrick Kajale mmoja ya waratibu wa swahili fest akipata picha ya pamoja na mmoja ya watoto walioshinda kucheza wimbo wa Bongo Flava.
Patrick Kajale mmoja ya waratibu wa swahili fest akipata picha ya pamoja na mmoja ya watoto walioshinda kucheza wimbo wa Bongo Flava.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV bwn. Iddi Sandaly akiongea machache kwa wageni waliohudhuria tamasha la Swahili Fest.
Mwalimu wa darasa la Kiswahili DMV na mdau wa CHAUKIDU Bi. Asha Nyang'anyi akiongea machache.
Mdau wa CHAUKIDU Bwn. Elius Magembe akilonga machache.
Wageni waliohudhuria tamasha hilo katika picha