Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mahojiano/Burudani. Show all posts
Showing posts with label Mahojiano/Burudani. Show all posts

Tuesday 5 December 2017

Mahojiano Saidi Kanda - sehemu ya 2- NGOMA



Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha 
Kwa kuanzia kama hujawahi kumsikia  Saidi Kanda sikiliza wimbo maarufu "Nasikitika " wa Remmy Ongala. Hizo ngoma kali zinapigwa na nguli huyu mzawa wa Bagamoyo.
Mwezi huu, Desemba 2017,  Saidi Kanda yuko safarini Kenya na Tanzania kushughulikia muziki yake.
 Anahesabiwa kati ya wapiga ngoma stadi ulimwenguni.  Alitunukiwa tuzo ya kwanza ya shirika maarufu la  WOMAD - mwaka 1989. 
Sehemu ya pili ya mazungumzo na Mwanamuziki huyu wa Jadi- Mpiga ngoma mkali - Saidi Kanda- mkazi Uingereza- anazungumzia THAMANI ya Ngoma na vyombo vyetu asilia.




zaidi ingia;
Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha

Tuesday 28 November 2017

Mahojiano Maalum na Mpiga Muziki Stadi- Saidi Kanda- Sehemu ya 1




Mwaka 1989 shirika maarufu la muziki Uingereza , WOMAD, lilimtunuku Mtanzania Saidi Kanda  tuzo la Mpiga Ngoma wa Kimataifa wa Mwaka duniani. Kuanzia hapo mzawa huyu wa Bagamoyo aliyezaliwa 1962, anahesabika mpiga ngoma wa nne kiufundi ulimwenguni chini ya magwiji hatari kama Airto Morreira (Brazil) na Changuito (Cuba) ...
Baada ya kusakata vituz na wanamuziki mbalimbali akiwemo marehemu Remmy Ongala, Kofi Olomide na msanii maarufu wa kimataifa, Grace Jones; leo Kanda anaongoza kikosi chake kikali cha "Mvula Mandondo" kutangaza albam yake ya kwanza, "Ambush".... 
KWA SIMU TOKA LONDON inawaletea sehemu ya kwanza ya Sura Tano za mahojiano kumtathmini mtunzi huyu anayetetea  (na kuhusudisha ), sana muziki wa kiasili wa Kitanzania nje na ndani ya Afrika Mashariki. 







Zaidi;
Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha

Tuesday 11 July 2017

Mahojiano ya Mubelwa Bandio, Viola na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A




Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.

Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.

Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2

Karibu utazame ukisikiliza

Friday 23 January 2015

Mahojiano na JhikoMan kuhusu wimbo wake mpya...Africa Arise


Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania

Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage.

Amezungumza mengi kuuhusu

Karibu usikilize hapa chini



Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja

Wednesday 13 August 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan‏



JhikoMan akitumbuiza kwenye Tamasha la Majahazi 2013
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a
JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Helsinki Finland mwishoni mwa mwezi Julai

Amezungumza
mengi kuhusu ziara yake ya Ulaya iliyoanza mwezi wa nne, maonyesho
aliyofanya, kazi alizorekodi na pia watu aliowashirikisha kwenye albamu
yake mpya ijayo.

Amezungumzia IMANI ya RASTA na pia MUZIKI WA TANZANIA kwa ujumla

Ameongea mengi mema

KARIBU UJIUNGE NASI


Saturday 5 July 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Diamond Platnumz baada ya tuzo za BET‏


Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles
Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Damond Platnumz. Msanii mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Tanzania
Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo.
Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO.
Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi.
SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini 
Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini.
KARIBU





Wednesday 2 July 2014

Mahojiano na Kwanza Production na NURU THE LIGHT‏


Photo Credits: Bongo Celebrity 
Karibu katika mahojiano kamini kati ya Kwanza Production na NURU THE LIGHT.
Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi moja kwa moja kutoka Stockholm Sweden
Kazungumza mengi ikiwa ni pamoja na alivyoanza muziki
Kisha akagusia kuhusu onyesho lake la kwanza kabisa jukwaani.
Na kama nilivyokuja kumtambua, ni mtu mwenye misimamo na anayejitambua, utamsikia msimamo wake awapo studio
Nikataka kujua pia, nini anaona kama tatizo kubwa kwenye muziki wetu?
Haya ni machache kati ya mengi aliyozungumza nami
JIUNGE NASI



Wednesday 25 June 2014

Katika "HUYU NA YULE" ya NJE-NDANI wiki hii......‏


Photo Credits: Bongo Celebrity 
Katika NJE NDANI wiki hii, mbali na habari kutoka Afrika, utasikia mahojiano yangu na NURU THE LIGHT.

Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nami kutoka Stockholm Sweden

Kazungumza mengi mema

Jiunge nami, MUBELWA BANDIO Jumamosi (June 28) katika NJE NDANI ya Kwanza Production na Border Radio kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana kwa saa za Marekani ya mashariki kupitia www.kwanzaproduction.com ama www.bordermediagroup.com


Tuesday 17 June 2014

Mahojiano ya moja kwa moja na msanii Anna Mwalagho kuhusu Tamasha lijalo‏


Anna Mwalagho.
Photo Credits Anna Mwalagho Facebook page
 Karibu katika mahojiano mafupi na ya moja kwa moja kati ya msanii Anna Mwalagho na Kwanza Production kwenye kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi Juni 14, 2014

Amezungumzia tamasha kubwa linaloendelea ambalo atatumbuiza pamoja na kikundi chake kwa siku tatu

Tamasha hilo linaandaliwa kwa ushirikiano wa watu wa Oman na maktaba ya sanaa za waAfrika hapa Washington DC
Karibu usikilize

Monday 9 June 2014

Kuelekea Kombe la Dunia...Mahojiano na Halifa Ramadhan kutoka Brazil‏



Photo Credits: EyesOnNews.com 
Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Brazil, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
Kuna malalamiko na maandamano nchini humo ambavyo kwa hakika vinaleta taswira isiyo njema kuhusu maandalizi ya michuano hiyo
Kutaka kujua mengi, Kwanza Production imefanya mahojiano na Halifa Ramadhan.

Mtanzania mwenye maskani yake nchini Brazil ambaye amezungumzia mengi kuhusu maandalizi ya fainali za kombe la dunia na pia maisha ya nchini humo kwa ujumla.
KARIBU UUNGANE NASI
Kwa maoni ama ushauri tuandikie kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Saturday 7 June 2014

Mahojiano ya Dekula Kahanga "Vumbi" na Kwanza Production‏


Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Dekula Kahanga "Vumbi"
Vumbi ambaye anamiliki Dekula Band nchini Sweden

Amezungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa albamu yake mpya ya Shujaa Mamadou Ndala iliyozinduliwa Aprili 23 na 24 huko Sweden.

Pia, ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaotaka kufanya muziki nchi za Scandinavia

KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni na ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Tuesday 12 November 2013

Mahojiano na mwanamuziki Dekula Kahanga a.k.a Vumbi‏


Hivi karibuni Jamii Production ilipata nafasi ya kuhojiana na mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu katika ucharazaji gitaa nchini Tanzania Dekula Kahanga aliye maarufu kwa jina la Vumbi.
Mahojiano haya "mepesi" yamegusa mambo mbalimbali kuhusu maisha yake kimuziki
Amehojiana na Jamii Production akiwa Sweden yalipo makazi yake ya sasa
KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Tuesday 5 November 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Dj Luke Joe‏


Dj Luke akiwa studio na Mubelwa Bandio wa Jamii Production
Karibu katika mahojiano na Dj mkongwe kutoka Tanzania na
mmiliki wa blog ya Vijimambo Lucas Mkami a.k.a Dj Luke Joe


Dj Luke ambaye makazi yake kwa sasa ni Maryland nchini Marekani ameeleza mengi kuhusu kazi zake hizi.

Katika mahojiano haya, ameeleza historia yake katika kuchezesha muziki, aliyemvutia kuingia katika kazi ya uDj, mafanikio ya Dj, changamoto zake, ku-blogu na mengine mengi.


Karibu Uuungane nasi



--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Thursday 10 January 2013

Mfululizo wa Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics:Dully Sykes (4)!!!!!!


Muendelezo wa 147 Critics;leo tunamsikiliza mdau na mwanamuziki muhimu kwenye Tasnia ya Muziki  wa kizazi kipya Dully Sykes.Ufahamu wake kuhusiana na marekebisho  ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147  yanayogusa Muziki na Filamu.

 Tumsikilize  Critics 147: Dully Sykes  (4) Akiwa ni mtu wa  nne kuelezea maoni yake kupitia Video;





 

Muendelezo wa mahojiano na wadau mbalimbalikuhusiana namabadiliko ya sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 
147,uelewa wao na nini mitazamo yao!

kwa maelezo zaidi ingia;TheImageProfession


                                                   "Swahili NA Waswahili" Pamoja sana. 


Mfululizo wa Mahojianao ya Wadau wa Filamu na Muziki;Critics 147:Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee (3)!!!!!!


Muendelezo wa 147 Critics.leo tunamsikiliza mdau na mwanamuziki muhimu kwenye Tasnia ya Muziki 
wa kizazi kipya Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee,Ufahamu wake kuhusiana na marekebisho 
ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147,yanayogusa Muziki na Filamu.

 Tusikilize 147:Judith D.M Wambura a.k.a Lady Jay Dee Akiwa ni mtu wa tatu  kuelezea maoni yake kupitia Video;





Judith Daines Wambura Mbibo akielezea mitazamombali mbali kuhusiana na uwekaji STAMP kwenye kazi za sanaa ya Muziki na Filamu. Huu ukiwa ni muendelezo wa kuwahoji  wadau mbalimbali kuhusiana na mabadiliko hayo ya sheria ya ushuru wa bidhaa.



Kwa maelezo zaidi ingia;TheImageProfession


                    "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 26 December 2012

Mfululizo wa Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics:John F Kitime (2)!!!


 Muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tunamsikiliza mdau muhimu na makini kwenye Muziki wa Dansi na kwa 
upande mwingine kwenye Filamu akielezea kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147 
yanayogusa Muziki na Filamu.

Tusikilize 147 Critics:John F Kitime (2)  akiwa ni mtu wa pili kuelezea maoni yake.


Msikilize vyema John F Kitime uweze kufahamu vyema yale anayoyajuwa na anayodhani ni muhimu kuwa sawa katika mabadiliko ya sheria hii!






Mahojiano haya na Ndg John F Kitime yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.

kwa Maelezo zaidi ingia;TheImageProfession 

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Saturday 22 December 2012

Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)


 Mfululizo wa 147 Critics ambayo ni  mahojiano ya wadau wa Filamu na Muziki yaliyofanywa na TFCA-
Tanzania Film Critics Association(On line Platform) kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
ambayo yatapelekea kuanzia mwezi wa January 2013 bidhaa zote za Filamu na Muziki zilizopo hapa Tanzania kuwekewa 
Stamp/Sticker kwa ajili ya Kurasimisha,Kumpatia kipato halali msanii na Kukusanya mapato ya serikali yanayotokana na 
uuzaji wa kazi husika.
Sheria hii ina changamoto nyingi ambazo kama hazitatatuliwa zinaweza kuifanya sheria husiaka isfikie malengo yake,Je 
wadau wanasemaje kuhusiana na hilo?

Tusikilize 147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)  akiwa ni mtu wa kwanza kutupa maoni yake kupitia Video hii;


Mahojiano haya yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda
mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na
kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo
hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.
80
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.

Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.
           

 Kujua Zaidi Ungana na mwenzangu;TheImageProfession
              
  "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.