Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 8 March 2011

Siku ya Wanawake!!! Mshindi wa Shindano la Wanawake wenye HIV!!!!!!!!!

Mwanamke kutoka Botswana, Anaeishi  na  virusi  vya  Ukimwi. Mashindo hayo ya Wanawake yaliyo fanyika  2007 , Wanawake walijitokeza ili kuifaamisha jamii kwamba  kuwa na Ukimwi siyo mwisho wa Maisha!!!!!!!!Je wewe unamaoni gani katika hili? Tuungane pamoja katika kuelimishana na kusaidia Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI!!!!!!!!.

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa siku yetu ya wanawake dunia nzima!!

Mija Shija Sayi said...

Maisha ni mtazamo. Hakuna kitu kigumu au chepesi hapa duniani, yote yanategemea na mtazamo wako juu ya jambo hilo. Ni kweli kuwa na ukimwi si mwisho maisha ila ni ngumu sana kuamini na kulikubali hilo pindi unapoukwaa...

Anyway bado twahitaji kuzishinda hizi dhana za kudidimiza mitazamo yetu..

Hongereni kina mama kwa siku hii.

Simon Kitururu said...

Nanukuu:``Tuungane pamoja katika kuelimishana na kusaidia Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI!!!!!!!!´´-mwisho wa nukuu.


Nakubaliana kabisa na hilo!

Anonymous said...

kuugua si mwisho wa kuishi duniani,kifo si cha mgonjwa alie kitandani,kifo cha wote binadam tutembeao mitaani,ugonjwa si kufanya mtu akate tamaa maishani,mwenyezi mungu awe pamoja nasi na wote wenye kuumwa walio kitandani,watembeao barabarani,ameen

Anonymous said...

mwanzo kabisa si kuelimisha tu kusaidiwa kimaisha,wengi wao wanakata tamaa kwajili ya hali ngumu ya maisha,kutafuta lishe ya kila siku,hali mbaya ya maradhi bora,wanashindwa kuepukika na maleria,maji safi,na umasikini ufuqara uliyojaa wanazidi kujikuta wanafeli ata kuwa kujiangalia afya kwa ufanisi zaid, utafutaji mgumu wa mahitaji mhim ya kila siku,tuwache ubinafsi,wenye upeo wakusoma tuwasomeshe,wenye watoto tuwasaidie kuwaelimisha ili mgonjwa mama,au baba asijikute na mawazo mengi ya ulezi,wakutafuta maisha bora yao binafsi,tujitokeze pindi tuisikiapo wenye matatizo kama hayo.walio karibu katika familia,na walio mbali ya nje ya familia,MOLA ATUPE IMANI NA ZAID KUWEZA KUWASAIDIA WENZETU,AMIN

emu-three said...

Hawa walijitolea kuhamasasha, na ni kielelezo cha akina mama wengi wanaoishia kufa na kukata tamaa bila misaada yoyote.
Siku kama hii ilitakiwa kuwa na harambee, na hata kuwatembelea akina mama vijijini

EDNA said...

Kuugua si mwisho ya maisha,Ukimwi ni kama yalivyo magonjwa mengine.Cha msingi ni kutowanyanyapaa walioathirika bali kuwaonyesha upendo na kuelimisha wengine.

MissPosh said...

congrats to her she's a super woman god bless hatuna guarantee to survive the next 10mins proud of her

Mel said...

Ni vizuri sana ndugu zetu wanapokuwa huru kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali jamii inawatazamaje kutokana na matatizo ya kiafya waliyonayo, jamii kwa ujumla ina wajibu mkubwa kuwafanya wenzetu wajisikie huru kushiriki, kwanza kuonyesha upendo kwao vilevile kuwaheshimu na kuwaonyesha kuwa nao ni sehemu ya jamii. Kwa kufanya hivyo ndugu zetu wataishi kwa amani bila hofu kuwa jamii inawatazamaje.

Rachel Siwa said...

Asanteni sana wapendwa kwa mawazo na michango yenu! Mungu atupe mapenzi mema ya vitendo zaidi!!!!!!!

Tuendeleeee!!!!!.