Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 12 March 2011

Wanaume Wanaopigwa na Wake zao!!!!!!!!!!!

Hivi  kuna Wanaume  wanaopigwa  na  kunyanyaswa  na  Wake zao? Je nao wanakitengo cha kuwasaidia kama vile Tamwa na kwingine? Kwanini  kelele nyingi/mashitaka mengi  niyasikiayo  ni ya Wanawake,Au Wanaume ni wavumilivu,wanaona aibu,wanajikaza kiume au wao hawaumizwi na wakiumizwa wanayamaliza wenyewe? Karibu tuelimishane wapendwa!!!!!!!!.

12 comments:

Mija Shija Sayi said...

Mimi nasubiri wanaume wenyewe waseme...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dada Rachel. Wapo wanaume wengi tu wanaokung'utwa na kutiwa kibano kwenye ndoa zao. Kutokana na sababu za kimapokeao, si ajabu wengi wao wanajikaza kiume wakiogopa aibu mbele ya jamii.

Mwaka jana nilisikia kwamba walikuwa katika harakati za kuunda chama chao. Sijui juhudi zao zimefikia wapi. Mwenye habari zaidi atujulishe.

Kwa kuanzia tazama hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/11/leo-ni-siku-ya-wanaume-duniani-chama-wa.html

Goodman Manyanya Phiri said...

Hodi hapa, Rachel!

Naona kweli ntakaribishwa kwa ngumi kweli.

Kupigana siyo kuzuri; lakini mimi nafikiri ni sehemu moja ya kuendeleza POWER PLAY au nani mwenye nguvu (za kifedha) katika ule uhusiano.

Sidhani kabisa mwanaume anathubutu kumpiga mkewe ikiwa mwanamama ndiye mwenye uwezo, si atafukuzwa siku hiyohiyo nyumbani?

Kadiri wanamama wanaposonga mbele kwa kupata uhuru wao wa kiuchumi kote duniani hao MACHOWOMEN kama huyo uliemchora hapa wanazidi kuongezeka na sisi wanaume "tumeipata basi"!

Mimi napendekeza,badala ya kuunda chama chetu, au hata kujinyonga ambao ndio mtindo wetu "maarufu", lazima tunyenyekee tujiunge na vyama vya wanawake. Sidhani watatufukuza kwani wanawake pia ni mama zetu!

Anonymous said...

Hodi Hodi Dada rachel ............Mi mtazamo wangu siwezi kuamini mwanamme anaweza kupigwa na mwanamke ,basi huyo ana uslave wa mapenzi au huba zimemjaa anaogopa asije kukosa mengi na akaachwa kwenye mataa lazima akubali kupigwa na anyanyasike kwa vyovyote ,na wengi wao ni mariooo wanaosubiria kuchuna wake zao.hahahaha

Anonymous said...

Mh Mh JAMANI mbona makubwa hayo..mi nawasikiliza wanaume kwanza watasema nn wazo hilo..

EDNA said...

Wapo sana sema huwa hawasemi wala kulalamika kwa rafiki zao au kushitaki kama ilivyo kwa wanawake.
Wanaona noma kusema.

Yasinta Ngonyani said...

wapo wengi tu kama sio kupigwa kwa magumi basi wanasemwa maana unajua maneno ni kipigo kibaya sana. Kuna wanawake ambao wanawasema waume zao kwa maneno makali sana.

Fita Lutonja said...

WANAUME dada Rachel tunaonewa sana lakini nashindwa kujua kwanini sisi hawatutetei? Kwangu mimi naamini kuwa binadamu wote ni sawa yatupawa kutenda haki kwa kila upande jamani wanaume wanteseka ila wengi wao hawsemi nakumbuka siku moja nilikuwa kambi ya jeshi Sangasanga nilisikitika kumuona askali mmoja sitamtaja akiwa na jeraha baada ya kumuuliza kwa kina akaniambia kapigwa na mke wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! inauma sana jamani tuwe wasawa

chib said...

Kipigo cha maneno!! Kwa mtindo huo, wengi watanyamaa tu!

Rachel Siwa said...

wapendwa asanteni sana kwa mawazo yenu/michango yenu!

@kaka Matondo nimeona pale kwako je chama kinaendelea? wenye kujua wajuze!
Pia na hiyo uliyoweka Mwanaume kapigwa sasa waliokuwa wajiuliza hivi kweli.Ingia,www.matondo.blogspot.com utapata ukweli na zaidi kuhusu Tanzania waliamua kuanzisha chama [ccwwt] ingia hapo utapata habari kamili.

@kaka Goodmana hahaha usjali kaka hapigwi mtu hapa! na KARIBU SANA!

@Kaka Lutonja usjali kaka chama kipo sasa sijapata uhakika kama kipo hai!.

Haya tuendelee wapendwa je Wanawake ukikuta kaka yako ndiyo anadundwa ytafanya nini?

Simon Kitururu said...

Hii kitu ipo sana!

Na unajua wanaume wengine tumefunzwa kutopiga wanawake.

Mimi yalinikuta siku moja ambayo hata ugomvi ulipoanzia sijui ingawa nahisi ni maswala ya wivu tu na Tequila shots!

Basi ghafla msichana mmoja aliyekuwa ananisaidi urafiki wa kike akaanzisha bwana kasheshe yani lile la fulu kunirukia halafu niko na washikaji hapo ambao nao kwake ilikuwa ni moja la tatizo.

Basi mimi kwa kujaribu kuepusha dhali nikapiga simu Polisi kuwaita kuhusu kasheshe lenyewe.

Cha kushangaza Polisi walipofika wakamuita mwanamke pembeni na kuanza kumuhoji kuwa kama anataka kunifungulia kesi. Na kwa bahati nzuri nilikuwa na mashahidi ambao wote wakashangaa ni kwanini niliyepiga simu ndio sisikilizwi na asikilizwaye ndiye aliye kuwa analeta vurumai na bila ushahidi wao labda ningewekwa ndani ingawa ni mie nimewaita.


Mimi moja kwa moja nikaanza kuamini labda ni ubaguzi wa rangi kwa kuwa mdada alikuwa mzungu. Na ni mpaka baadaye nilipostukia ni kwamba wale Mapolisi hawakuamini kabisa kuwa yule msichana ndio mwenye kasheshe kwa kuwa ni MSICHANA . Hasa kwa kuwa hawaamini mvulana anaweza kuita polisi kwa kasheshe la mwanamke!

Na haki ya nani tokea siku hiyo nahisi ni vigumu sana hata kwangu kumripoti mwanamke kuwa ananishushia varangati kwa kuwa kwanza huaminiki ukiripoti hilo .


Na wapo wanaume wengi watesekao kwa kuwa atawakisema haitaaminika, watajishusha kwenye jamii na kwa ujumla inaaminika sio jambo la kidume kubwengwa na demu ingawa upo ukweli kuwa wapo wanaume wengi wabwengwao kwa kuwa tu hawarudishii mapigo kwa sababu zao binafsi ikiwa ni pamoja na kulelewa kwa staili ya kuwa mwanamke hapigwi, matatizo ya kiuchumi ambayo yanaweza kuzaa kidume kufukuzwa nyumbani kwa mwanamke au kutalikiwa kitu ambacho kitamkosti au tu ukweli tuko vidume tupendao MIBONGE ya MIDADA ambalo likikukalia sikumoja hufurukuti.


Mnakumbuka gazeti la Sani kuhusiana na MIDADA gani kiukubwa ambayo PIMBI alikuwa naifukuzia?

Rachel Siwa said...

Pole @kaka Kitururu kwa yaliyokukuta!
basi huyo dada akijiona yeye mshindi kamtwanga mwaume!

pia nakubaliana nawe wengine wanabwengwa na kuwaachia tuu!!!.