Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 25 April 2012

Swali kutoka kwa Mwanamke wa Shoka[da'Mija] na Blogger wa Kwanza Mwanamke Mswahili!!!

Kwangu mimi ni Mwanamke wa Shoka huyu dada,Kichwa,mama Vipaji.
Ni Mwanamke wa Kwanza Blogger Mswahili mimi kumfahamu.blog yake http://damija.blogspot.co.uk
Da'Mija na Wanawake wa Shoka.
Swali;wewe Unafikiri Wanawake wa Shoka Wakoje?.

Haya tukiachana na hayo, Shuka Chini uone Swali lake analotaka KuJibiwa,Linatokana na  Mada ya Jikoni leo ni Kakazz.
Mama MM[Jina lake linaanzia na M,Mume wake M, watoto wao M.M]
Kidada zaidi au vipi!!Una mbwembwe wewe dadake.
Nanukuu..
"Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?."


Nami ngoja niulize kulingana na swali.."Kwani nafasi ya mwanamke ni ipi katika ndoa..Je ni kupika na kufanya kazi za ndani? au kwa maana nyingine ni kwa nini hasa mwanaume huamua kuoa?


Wanaume tungependa majibu yenu zaidi hapa...

        

9 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

tunamuoa mwanamke baada ya kujifunza kupika, kusafisha vyombo, kufagia, kutunza watoto na kadhalika. Ukikuta dume halielewi chchote cha ndani ya nyumba utakuwa mjinga kukubali kuolewa na mtu anaetaka mtumwa kwako badala ya msaidizi!!

Mija Shija Sayi said...

Rachel hili la kumwagia watu sifa naona nalo ni kipaji chako kingine, tukiachilia mbali u-MC,

Nashukuru kwa yote...
Ubarikiwe sana muke ya Mubena..

Yasinta Ngonyani said...

Ni swali nzuri sana haya kaka zetu mpo wapi jitokezeni...Mija umetoka chicha dadangu:-)

emuthree said...

Kweli tunamtunuku kama dada wa blog. Lakini wahenga husema wavumao baharini papa kumbe wapo wengine kama wewe ndugu wa mimi

sam mbogo said...

Kiukweli,kama mwanaume na baba bilakusahau ni mume wa mtu(roho yangu my wife). sikumbuki kama niliwahi kuwaza naoa kwa ajili ya hayo yote ulio bainisha hapo juu. I la ninacho kumbuka nilijiambia mwenyewe kuwa sasa muda wa kuoa umefika ila sikujuwa ni yupi angekuwa my wife japo kulikuwa na nilio kuwa nawakubali kwa maumbile yao na muonekanao wao kuwa wanaweza kuwa chaguo langu.swala la kupika halikuwa tatizo kwangu. hivyo haya mengine ya kupika nimatokeo tu ,ila kimsingi mimi ni mpikaji,na mazingira ninayo ishi sasa mimi ndo mpishi mkuu.mke kwangu ni muhimu kutokana na taratibu na mifumo ya maisha,japo ndoa ni kiboko,bonge la shule. kaka s.

emu-three said...

Nilikuwa sijajibu swali maana mtandao no unashida zake,....swali lilijificha:

Kwanini wanaume wanaoa,pia unaweza kuigeuza hivi, kwanini wanawake wanaolewa:
Kwanza wote tunamuamini mungu, au sio hata kama unaamini kwa kupitia njia nyingine, lakini hatima yake ni huyo muumba. Tunaoa kwa sababu mwenyezimungu katuambia tuoane ili tukaijaze dunia....!
Mambo mengine ni kusaidiana tu, kwasababu huwezi ukazaa peke yako, lazima kuwa na mwenzako, kuwa na mume na mke,...unaweza kuweka unavyoweza.
Swali linakuja baadaye ndio tumeambiwa tuoane ili tukaujaze ulimwengu, kwa vipi, hapi ndipo zinakuja sheria, jinsi gani ya kuoana,na mengineyo.
Je mkishaona itakuwaje,...tukarahisishiwa kuwa kuna muoaji na muolewaji, na ukiangalia hapo,utaona taratibu nyingi, muoaji ni mwanaume,na muolewaji ni mwanamke,hata kama kuna wengine wanaotoa mahari ni wanawake,....lakini anayeolewa ni mwanamke.
Kiasili,wanadamu tumeumbwa na vipaji , kuna vipaji vya asili, mwanamke, kajaliwa kupika ....na mwanaume kajaliwa kufanya kazi za nguvu....hata ukiangalia maumbile...ingawaje inaweza ikatokea vinginevyo.
Kiutaratibu lazima mnapokutana zaidi ya mmoja, kuna takiwa kuwe na kiongozi, kunatakiwa kuwe na taratibu za kikazi, sasa itakuwaje kati ya wanandoa hawo, haina shida, tunakwenda moja kwa moja kweney vipaji vya asili....
Ni mlolongo mrefu tunaweza tukatunga kisa hapa, ila kifupi, ndoa ni taratibu ambazo zimebarikiwa na mungu, mke namume waishi pamoja kama aivyoishi Adam na Hawa,...
Ili tukaijaze dunia, mengine ni kusaidiana NA KUWEZESHA WANANDOA HAWA WAISHI KWA AMANI NA UPENDO. Sijui wenzangu mnasemaje.

Interestedtips said...

Da'Mija ni mwanamke wa shoka hiyo hujakosea, kwakweli mwanaume akiwa anajua kazi zote za ndani anaweza kuoa haraka au akachelewa, ila akioa mwanamke ujipange utakosolewa kila mara ila faida utapata kubwa atakusaidia kwa vingi sana

Rachel Siwa said...

Waungwana Ahsante sana sana kwa michango,Maoni na Ushirikiano wenu katika kijibu swali hili.Kwaniaba ya da'Mija[Mwanamke wa Shoka] Tunawashukuru mnoo!!!!Mbariwe wooote na Pamoja sana.

Pia kama unalolote au wewe bado hujasema chochote ukijuacho, hatuja funga mlango, unaweza kutoa maoni yako,JIMWAGE TUU MUUNGWANA!!!

Rachel Siwa said...

Ameeeeeeeeen dada Mija!!!!!!