Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 30 April 2012

Wimbo Mpya "Uhuru wa Habari" kutoka Ngoma Africa band aka FFU

                  FFU wa Ngoma Africa Band wameachia Jipya "Uhuru wa Habari"
                  Unasikika at www.ngoma-africa.com


Kwa kawaida wanahabari na vyombo vyao ndio wanarusha hewani habari za
matukio mbali mbali pamoja wasanii na burudani zao kwa jamii,
Lakini bendi maarufu Ngoma Africa aka FFU imewageuzia kibao !!
Kuliweka hewani song jipya "Uhuru wa habari" wimbo huo mpya
utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na
kijana Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye pia ni mpiga
gitaa la solo(mtutu) wa kikosi kazi iko.
Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye makao yake kule ujerumani,
miezi michache tu iliachia hewani CD ya "Miaka 50 ya Uhuru" na sasa
wanarusha hewani "Uhuru wa habari" ,
Taarifa za kuhaminika zinaeleza kuwa Remix ya wimbo huo pia itakua
hewani siku za usoni,katika Remix hiyo kutakua na majina mengi ya wa
dau wa habari ambao wanachangia kuijulisha jamii habari mbali mbali.
Sikiliza na pata burudani ya bure katika ffu camp at www.ngoma-africa.com
au http://www.ngoma-africa.com


No comments: