Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 23 April 2012

Siku kama ya leo kaka Twahil Alizaliwa na Siku kama ya Leo Tulimpoteza baba yetu Kipenzi!!!!!!

Siku kama ya leo,Bibi na Bwana M.S.Kiwinga wa Ilala Sharifu Shamba,Dar-es-salaam.Walipata mtoto wa kiume na wakamwita Twahil.Mtoto huyu Siku alipofikisha umri wa miaka 9.Ndiyo Siku ambayo baba yetu, Kipenzi chetu,Muhimili Wetu,Faraja yetu,Rafiki yetu, yaani ni kila kitu Maishani mwetu,Marehemu M.S.KIWINGA.Aliga DUNIA!!! Ohhhhh Siku ambayo Familia hii hatuwezi kuisahau kamweee.

Tunamshuru Mungu kwa kila jambo.Kwani yeye huyu Mungu ndiye alisimamia makuzi yetu mpaka leo hii.


Hongera sana kaka Twahil, Mungu azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo.
Tupo pamoja katika Siku yako hii muhimu japo ni siku ngumu kwetu.


Hongereni Wooote Mliozaliwa Leo na Pia Poleni sana mliopoteza Wapendwa wenu/wetu Leo.
Mungu awabariki na kuwalinda.


Wenu Rachel-siwa[Mwanapenza]hili mwanapenza ni jina la mama wa baba yangu mzazi[BIBI, Asha Penza]. Basi  baba yetu  alikuwa hupenda kutuita watoto wa kikeMAMA.
                       PAMOJA SANA,UPENDO DAIMA!!!!!!

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza HONGERA KAKA Twahil kwa siku hii muhimu kwako. Na pia poleni sana kwa kufiwa na baba. Najua yupo nanyi kiroho ila sio kimwili.

Mija Shija Sayi said...

Poleni sana jamani.... na hongera kaka Twahil. Huyu kaka Twahil inawezekana kabisa ndiye mshika familia yenu... ya Mungu mengi.

Anonymous said...

Kwanza hongera sana kaka Twahil kwa kuzaliwa siku kama ya leo mwenyezi Mungu akujalie maisha yaliyo jaa upendo kaka
Napili Poleni sana wapendwa kwa kumpoteza kipenzi baba,ni ngumu sana kwetu sisi wanaadamu wakati tunapoondokewa lakini tumeambiwa tushukuru kwakila jambo.

Rachel Siwa said...

Amina wapenzi na Ahsanteni sana sana, Mungu atubariki sote.
@dadake kweli ya MUNGU NI MENGI!!!!

emuthree said...

Hongeara kaka Twahili kwa siku yako ya kuzaliwa na poleni kwa huo msiba,....yote ni mapenzi ya mungu...yeye ndiye mpaji na mchukuaji.

EDNA said...

Sijachelewa sana bwanaaa,hongera sana kaka kwa kuongeza mwaka mmoja zaidi na pole kwa kufiwa.

Rachel Siwa said...

Ndugu wa mimi@emu wa 3 na Mwanakwetu da'Edna, Ahsanteni sana sana,Pamoja daima!!!