Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Shida na Raha. Show all posts
Showing posts with label Shida na Raha. Show all posts

Monday 23 April 2012

Siku kama ya leo kaka Twahil Alizaliwa na Siku kama ya Leo Tulimpoteza baba yetu Kipenzi!!!!!!

Siku kama ya leo,Bibi na Bwana M.S.Kiwinga wa Ilala Sharifu Shamba,Dar-es-salaam.Walipata mtoto wa kiume na wakamwita Twahil.Mtoto huyu Siku alipofikisha umri wa miaka 9.Ndiyo Siku ambayo baba yetu, Kipenzi chetu,Muhimili Wetu,Faraja yetu,Rafiki yetu, yaani ni kila kitu Maishani mwetu,Marehemu M.S.KIWINGA.Aliga DUNIA!!! Ohhhhh Siku ambayo Familia hii hatuwezi kuisahau kamweee.

Tunamshuru Mungu kwa kila jambo.Kwani yeye huyu Mungu ndiye alisimamia makuzi yetu mpaka leo hii.


Hongera sana kaka Twahil, Mungu azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo.
Tupo pamoja katika Siku yako hii muhimu japo ni siku ngumu kwetu.


Hongereni Wooote Mliozaliwa Leo na Pia Poleni sana mliopoteza Wapendwa wenu/wetu Leo.
Mungu awabariki na kuwalinda.


Wenu Rachel-siwa[Mwanapenza]hili mwanapenza ni jina la mama wa baba yangu mzazi[BIBI, Asha Penza]. Basi  baba yetu  alikuwa hupenda kutuita watoto wa kikeMAMA.
                       PAMOJA SANA,UPENDO DAIMA!!!!!!

Monday 13 February 2012

Hongera Mange/U-Turn Blog. Tunapo kula na kunywa,Tusisahau na Wenye Shida!!!!!
Hongera Mange/U-Turn Blog na Wooote mlioshiriki/Kufanikisha jambo hili,Mungu awabariki sana.
Nijambo jema tena lenye maana na Mfano mzuri.Watoto Yatima,Wasiojiweza,Wenye hali/Maisha magumu ni Jukumu letu sote,kuwasaidia na kuwanao pamoja na kuwapa Upendo.
Mungu ni Pendo Apenda Watu!!!!!!Pamoja.

Kuona/Kujua zaidi, Ingia. hptt://www.U-turn.co.tz.

Saturday 24 September 2011

Mshumaa uliozimika.Leo ni BRENDA FASSIE, Sikiliza (Vul'indlela / ...!!!

Mungu wape Faraja  Yatima ,Wajane na  wote walioondokewa na wapendwa wao.

Thursday 7 July 2011

Baba wa Blogger Evarist Chahali Apata Ajali Mbaya!!!!

Mzee Philemon Chahali,Amepeta Ajali mbaya asubuhi ya leo huko Ifakara Tanzania.
Tuungane pamoja katika kipindi hiki kigumu kwake Mzee wetu Chahali na familia yote ya Chahali kwa Maombi,Sala/Dua.

Kaka Chahali pole sana  Mungu akupe nguvu na Tupo pamoja nawe.

Kwamaelezo zaidi unaweza kuyapata.  http://www.chahali.com [Kulikoni Ughaibuni].

Wednesday 16 March 2011

Kuna Wanaojikondesha na Wanaokonda si kwa Kupenda!!!!!!!!!!!!!

Wapo  wanaotamani  hata Uji wa chumvi na hawapati,Wapo wanaoweza kupata chakula chochote watakacho,lakini hawali kwa sababu wanafanya Diet. Wapo wafujaji, waharibifu na wachoyo.Wapo wanaopenda kusaidia waliokosa lakini wana vichache.Binadamu tujenge tabia ya kusaidiana / Kutoa ni Moyo si Utajili!!!!! Wewe unamawazo/mchango  gani katika hili? Karibu tuelimishane Wapendwa!!!!