Hawa wanandika kwenye ubao na chaki.
Hawa wanamsikiliza mwalimu kwa tabasamu.
Hawa wamenyoosha mkono ili wapewe nafasi ya kujibu/kuuliza.
Baadhi ya Shule zimeshafunguliwa hapa U.k.
watoto wa shule kila kona sasa, lakini baadhi yao walivyo jiremba mmhh,
mpaka kugundua kama ni mwanafunzi ipo kazi.
Hili pia lipo kwa baadhi ya shule Afrika/Tanzania, hasa hizi shule za kulipia.
Sijui ndiyo kwenda na wakati auu....... Ninawaza tuu!!!!!
Mpendwa unafikiri kwa nini baadhi ya watoto wa Shule wanakuwa na Tamaa?[1].Ni utoto tuu wakikuwa wataacha,Kutoridhika na maisha yao au...?[2.] Nivyema kwa watoto wa Shule kuvaa sare za shule au kutovaa sare kila mmoja aje na nguo zake?
[3.]Kupata chakula cha aina moja Shule au kila mtu ajitegemee.
Karibuni sana kwa Maoni,Kuelimishana katika malezi ya watoto wetu!!!!!!