Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 7 September 2011

Watoto wa Shule na Tamaa!!!!!

                       Hawa wanandika kwenye ubao na chaki.
                                  Hawa wanamsikiliza mwalimu kwa tabasamu.
                                Hawa wamenyoosha mkono ili wapewe nafasi ya kujibu/kuuliza.
Baadhi ya Shule  zimeshafunguliwa hapa U.k.
watoto wa shule kila kona sasa, lakini baadhi yao walivyo jiremba mmhh,
mpaka  kugundua kama ni mwanafunzi ipo kazi.

Hili pia lipo kwa baadhi ya shule Afrika/Tanzania, hasa hizi shule za kulipia.
Sijui ndiyo kwenda na wakati auu....... Ninawaza tuu!!!!!


Mpendwa unafikiri kwa nini  baadhi ya watoto wa Shule wanakuwa na Tamaa?[1].Ni utoto tuu wakikuwa wataacha,Kutoridhika na maisha yao au...?[2.] Nivyema kwa watoto wa Shule kuvaa sare za shule au kutovaa sare kila mmoja aje na nguo zake?
[3.]Kupata chakula cha aina moja Shule au kila mtu ajitegemee.

Karibuni sana kwa Maoni,Kuelimishana katika malezi ya watoto wetu!!!!!!6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza kabisa nachukua nafasi hii na kusema nimeipenda sana mada hii. Maana hili swala limekuwa likinikera sana hasa kila mara nikilinganisha maisha yangu ya shule na ya wanangu/wanetu.
Nanukuu.."Nivyema kwa watoto wa Shule kuvaa sare za shule au kutovaa sare kila mmoja aje na nguo zake?
[3.]Kupata chakula cha aina moja Shule au kila mtu ajitegemee." mwisho wa kunukuu.....Hakika mimi kama mimi ngependa watoto/wanafunzi wote wavae sare kama ilivyo Tanzania na nafurahi sana sehemu nyingine Tanzania hata wakati watoto wanapopata komnio/kumnyo ya kwanza pia kipaimara wanavaa sare za shule. Unajua kwa nini hii inaletesha unafuu sana kwa wale wenye vipato vidogo..kwani bila ya hivyo hakika wenye mihela wanavalisha watoto mpaka unashangaa...Kwenye chakula ni safi kama wote wakila chakula cha aina moja kama wanapata shuleni. ni mawazo yangu ruksa kuwa tofauti

Goodman Manyanya Phiri said...

"Tamaa" kwa watoto hao sijaelewa maana yake na kwa hiyo sitatoa maoni juu ya hilo.

Kuhusu "sare", ni kitu kwangu cha kushangaza kwamba siku hizi kwa baadhi ya shule kila mtoto atavaa la kwake na watoto maskini kwa matajiri watatofautiana wazi-wazi.


Hapo kweli siwezi nikasema napendelea mfumo upi. Mimi nilimaliza shule tukiwa tunavaa sare hiyo LAKINI NGUO YA NDANI SIKUWA NAYO KAMA WATOTO WENGINE KWA HIYO NILIJITAMBUA TU KAMA MTOTO WA MASKINI.

Labda ni vema tu watoto waelewe kinaganaga wangali bado wadogo kwamba usawa duniani ni ndoto tu ya mwendawazimu....


...kila mmoja avae kiraka chake chenye rangi yake! Vilevile kila mmoja ale kiporo chake kwani kwa watoto wengi vitu kama pipi, chai na uji venye sukari, ayiskrimu na vingine ni fahari wakati mimi binafsi kama mzazi napendelea kulea watoto wangu mbali sana na sukari isipokuwa ni sukari ya matunda!

Simon Kitururu said...

Watoto wa shule na TAMAA!

Ngojea nifikiri ,...
..... kwa kuwa nahisi TAMAA kinamna inatokana na kujua KITU FULANI,...
..... kitu kifanyacho labda tunatumia neno moja TAMAA kwa kumaanisha vitu vingi TOFAUTI .

SI tamaa kwa mkubwa na tamaa kwa mtoto labda kama kiswahili kingekuwa na maneno mengi labda lisingekuwa ni NENO MOJA litumikalo kuwakilisha!

Ntarudi tena-bado nawaza!:-(

Mija Shija Sayi said...

Yasinta na Rachel mlitakiwa mkae pamoja...mmezidi ukali jamani..lol

Haa! haa! haa! Kitururu n'shakupata ila nasubiri urudi ili nihakikishe kama nimekupata vyema...

Kaka manyanya umemaliza yote kaka angu, ni kweli inawezekana kabisa mkavalishwa sare lakini ukweli unabaki moyoni mwako..

Cha msingi ninachodhani mimi ni wazazi kuchukua jukumu la kuwafundisha na kuwaelesha watoto maisha yanaendaje, maana wakielewa kutoka ndani mwao basi hawatataabika kushindana kijinga..

emu-three said...

Unajua nidhamu hujengwa kuanzia utotoni, na hili linatakiwa wazazi kuwa makini, kama tutawaachia watoto wetu wafanye lile walitakalo, wavae watakavyo, ....hii inaweza kuondoa nidhamu...kuna hekima fulani ya kuwa na sare, kuwa na mpangilio fulani, na hili unaweza kujifunza toka kwa wanajeshi...!

Rachel Siwa said...

Da Yasinta hiyo ya Komnio/komnyo,mimi nimeipenda sana kuvaa aina moja,pia kuna watoto ambao wazazi wao wanakipato kidogo, wanafikia hata kutofika kwenye ubarikio kwa mambo kama hayo,

@kaka Manyanya ni kweli usemayo, lakini watoto/wanafunzi wale hawakugundua kama nguo ya ndani huna, kidogo inanafuu, maana watoto/wanafunzi si unawajua wengi wao hawajui shida/maisha ya mtu ni kukucheka tuu mpaka Shule utaiona mbaya, hasa kwasababu nawe ni mtoto unaweza acha shule,

@kaka Kitururu ni kweli neno moja lina maana tofauti, mimi nimeongelea Tamaa za watoto/wanafunzi. Kwa mfano kwanini mimi sina simu, mbona Da Mija anabegi zuri na.... na hizi zinaweza kupelekea Babu Babuaaa maana wazee wengine, mtoto wa mwenzie si wake ni mkubwa mwenzie.

@da'Mija hahahaha yaani itabidi niungane nae nami ananikosha haswa, lakini aniacha sehemu moja tuu unaijua, sana, amebarikiwa/kufanikiwa bila kuwachapa na kina Erik wananivutia mno maana mpaka Ugali unapikwa, Hongera sana dada yangu Yasinta.

Ahsante wapendwa tuendeleee kujuzana/kuelekezana na malezi ya watoto wetu.