Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 10 September 2011

Poleni sana Wapendwa wetu Zanzibar,Mungu awatie nguvu kwa wakati huu Mgumu!!!

MELI YA LCT SPICE ISLANDERS YAZAMA KATIKA BAHARI YA HINDI PWANI YA NUNGWI LEO USIKU.Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.
Naibu Waziri huyo amesema meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima,lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unahitajika.Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helkopta yake kwenye eneo la tukio

Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

Habari kwa msaada wa Kapingaz.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mwenyezi Mungu aweape nguvu wafiwa na pia azilaze Roho za marehemu mahala pema peponi Amina.