Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 21 June 2012

Watoto na Malezi;Violence Against Children [Ukatili Kwa Watoto]!!!!!!!


Makala hii inaonyesha ukatili dhidi ya watoto na jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakishirikiana na wadau mbalimbali kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

Makala hii imetengenezwa ikiwa ni mwitikio wa hali ya unyanyasaji na ukatili ambayo watoto wanakabiliana nayo. Makala hii imeandaliwa sambamba na uzinduzi wa ripoti ya ukatili kwa watoto ambalo ni agizo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutokomeza ukatili kwa watoto. Ripoti hii ilizinduliwa na Dr. Asha Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Waungwana;Wazazi/Walezi Mnamaoni,Ushaurigani katika haya?


Shime Wazazi/Walezi;"Tutokomeze Ukatili  kwa watoto" Tuungane Pamoja katika kuwapenda,kuwatunza,kuwapa Malezi bora,kuwapatia Elimu na Kuwasikiliza.
"Mtoto wa mwenzio ni wako".
"SWAHILI na WASWAHILI" Pamoja sana!!!!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Dunia ina mambo kweli ,,,,,nimeangalia huku machozi yakinitoka. Mwanako kabisa unamfanyia hivyo kweli hata huruma hakuna...inasikitisha sana... nawatakieni wapiganaji wate kazi njema.