Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Afya/Jamii. Show all posts
Showing posts with label Afya/Jamii. Show all posts

Monday 17 June 2019

Afya Na Jamii;Mdau anaomba Ushauri

Wapendwa /Waungwana huyu mwenzetu anaomba Ushauri,

Jamani naombeni msaada ,mwanangu anamwaka sasa ,lkn mpaka sasa hakai,alafu shingo haiko imara sana,,nimeomba ushauri ,wakaniambia nitumie calcium, ambayo ndo nimeanza kutumia,je anaweza akawa na shida gani,maana mwonekano ana afya nzuri na hajawahi kuacha kuongeza kilo. 

Nimetuma kama nilivyotumiwa

Nimatumaini yangu atapata ufanunuzi zaidi

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday 26 January 2016

NesiWangu Show. Rev Kennedy on "OBAMACARE" registration before its deadline Jan 31, 2016


The Affordable Care Act (ACA) or OBAMA CARE is a United States federal
statute signed into law by President Barack Obama on March 23, 2010.
The ACA was enacted to increase the quality and affordability of
health insurance, lower the uninsured rate by expanding public and
private insurance coverage, and reduce the costs of healthcare for
individuals and the government”
This message is brought to you by HELP AFRICA, which is an organization that targets African Communities in abroad and at home.
We
urge you to register so you can access quality health services health
services, avoid penalties and strengthen the health of our communities.

Tuesday 29 December 2015

[VIDEO] NesiWangu Show hosts ChildBirth Survival International

Harriet Shangarai, Stella Mpanda and Tausi Suedi
"Pregnancy is not an illness or disease" say Childbirth Survival International (CSI) Co-founders - Stella Mpanda, CNM and Tausi Suedi, MPH.

It is estimated at least 800 women die every day due to pregnancy, childbirth, and post-childbirth complications, most of which are preventable.

Mama Mpanda and Tausi Suedi have an informative discussion with Harriet Shangarai of Nesiwangu show (click here) and leave no stone unturned as they passionately talked about the challenges, gaps, achievements, opportunities, and shared personal stories.

This video will give you an in-depth picture of Childbirth Survival International, the amazing work the team is doing, and how you can partner to make a difference.

 For more information, visit www.childbirthsurvivalinternational.com

Tuesday 1 September 2015

Mahojiano na Tausi Sued juu ya CSI FUNDRAISING
Dear All,Come join the Embassy of Tanzania and Childbirth
Survival International (CSI) for CSI’s first annual fundraising on
September 12th at 4:30pm to 7pm, at the Embassy of Tanzania, Washington
DC.In Tanzania, many of the lives lost during pregnancy,
childbirth, and immediately after birth, are often 100% preventable. We
are calling upon You to join us and help save lives. This fundraising is
to kickoff CSI’s saving lives at birth project in Biharamulo District
in northwest Tanzania. Biharamulo is one of Tanzania’s poorly performing
Districts that deserves immediate support and attention – We thank you
for answering the call. Visit www.childbirthsurvivalinternational.org for more information.There’s
a registration fee of $100 and it includes a raffle ticket. All
donations are tax deductible and will be used to implement project
activities in Biharamulo. Registration link here.Light Refreshments | Entertainment | Raffle Prizes | NetworkingFor information about the event, please contact

Sandra Kiyonga at sandra.kiyonga@childbirthsurvivalinternational.org or call 202-763-2100.Tuko Pamoja!

Monday 29 December 2014

NesiWangu Show...........Malaria Kit

NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.


Karibu uungane nasi.....

Tuesday 8 April 2014

Maangalizi ya afya Washington DMV...bure‏Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa wale wasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.
Tarehe: 04/12/2014   (Jumamosi)
Saa 3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)  
MAHALA
3621 Campus Drive, 
College Park, MD 20740

Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV. 

Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali


  • Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
  • kuandikisha majina ya wanaokuja
  • kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
  • au kushiriki katika timu ya kitaalam
Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.

Tuesday 20 August 2013

Afya Na Jamii;TATIZO LA MIFUPA AU KUUMWA MIGUU/MAGOTI: OSTEOPOROSIS:


Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi. Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.
Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa. Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi aba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume. Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.
NINI CHA KUFANYA
1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umriu mepiga hatua
2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza
3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani)
4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua)
VIRUTUBISHI
Kwa ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubishi ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu.
Virutubishi vifuatavyo vimewasaidia wengi wenye tatizo hili.
1. Calcium
2. Chitosan
3. LycopenKUKOSEKANA KWA UTE KATIKATI YA VIUNGO (JOINTS) - CARTILAGE

Kajiraba fulani ambako hujulikana kwa jina la kitaalamu kama “Cartilage” (katileji) ambako hupatikana katikati ya mifupa. Kuna kitu fulani huwa kinapatikana katikati ya mifupa miwili ya goti la mnyama (ng’ombe, mbuzi) huwa wengi wanapenda kukila kwenye baada ya kuchemshwa au kupikwa. Kama unaijua hii, basi ndio katileji yenyewe.
Katileji inasaidia kuikinga mifupa isiumie.Vilevile inafanya kazi ya kusaidia kuubeba uzito wakati wa kutembea, kuinama, kunyoosha viungo au kukimbia.
Zaidi ya asilimia 85 (85%) ya katileji ni maji, na jinsi umri unavyosonga mbele, maji hayo huwa yana kawaida ya kupungua. Na asilimia 15 niprotini.
Tatizo hili lipo zaidi kwenye sehemu ya magoti. Endapo katileji inakuwa ina tatizo, husababisha maumivu makali hasa unapotaka kusimama au kutembea, vile vile kwenye mabega, au nyonga. Pia inaweza sababisha uvimbe (goti au nyonga au bega kuvimba).
Mtu ambaye katileji yake ina tatizo aidha imelika au kutokuwepo kabisa, anatakiwa kupatiwa vitu au virutubishi ambayo vitasaidia kuirekebisha katileji au kuijaza kwa upya.
Virutubishi vifuatavyo vimesaidia wengi wenye tatizo hili:
1. Shark Cartilage
2. Calcium
3. Chitosan

OFISI ZETU ZIPO karibu na huduma zifuatazo:
1. Ofisiya TRA, au karibu na
2. Afya Dispensary, au karibu na
3. Mjasiriamali kwanza, au karibu na
4. Kanisa la Sabato au karibu na
5. Kanisa la Lutherani au karibu na
6. Uwanja wa mpira wa Mwenge.

Anaye hitaji ufafanuzi zaidi tuwasiliane: 0715 594 564 au 0756 594 564

Au tembelea website yetu www.1000ufahamu.com

Friday 11 January 2013

Afya na Jamii;Na Mswahili John Haule- Nyama tamu, Inaua!


Historia yake:
Kwa miaka mingi sana nyama imekuwa chakula cha asili kabisa katika nchi yetu. Nyama imekuwa ikiliwa na inaendelea kuliwa na vyakula vya wanga, na hapo ndipo nyama ilikutana na jina jipya la kitoweo. Lakini pia nyama hailiwi tu kwa staili hiyo, nyama pia ilijikuta ikipata jina lingine kwenye mabaa na vilabu vya pombe iliposhushiwa na mafunda ya pombe na kuitwa asusa.
Nyama ni tamu sana. Kuna uhakika wa kitaalamu kabisa unasema nyama ikipikwa au kuchomwa basi utamu na mahitaji yake kiafya mwilini huongezeka mara dufu. Lakini nyama ukiikuta mezani itakutatiza sana kujua hii ni ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, au sungura. Vilevile inawezekana pia hata hisia zako zikawa tena mbali na ukweli maana nyama ipo pia ya porini kama vile pofu, nyati, mbuni, swala, digidigi na wengineo wengi tu, hivyo kuuliza kabla ya kula nyama ni muhimu sana hasa kwa wale wenye miiko na baadhi ya vyakula na waislamu ambao baadhi ya nyama kwao zimeharamishwa. Ila mimi nawaongezea jicho la tatu ndugu zangu hao kuwa IMEHARAMISHWA tu lakini HAIKUKATAZWA kuila kama hutakuwa na jazba kunielewa utagundua hivyo. Na mimi nafikiri leo naziharamisha nyama za aina zote hapa kwa ushahidi wa madhara ya kiafya na kiroho pia.
Mungu pia hapendi nyama:
Kama mtakumbuka mliosoma Biblia, Wajukuu wa Mungu Kaini na Abeli walijikuta siku moja wakimtolea babu yao sadaka. Kaini akiwa kama mfugaji alichinja akamletea Mungu nyama. Mungu alikataa na sadaka yake haikuteketea! Lakini Abeli akiwa kama mkulima yeye alileta mazao ya shamba lake. Mungu alipokea! Ikawa Kaini akamwuua nduguye Abeli na kizazi cha wafugaji kikajimegea dhambi ile mpaka leo.
Nyama inajenga matabaka:
Enzi zetu za kujisomea hapa nchini kila nyumba ilikuwa na “Book Shelf” Leo zipo wapi? Sisi tulisoma kitabu kilichoitwa UPUMBAVU WA MWAFRIKA na ndani kulikuwa na hadithi nyingi tamu ikiwemo “Uchu wa Mzee Mikidadi” ambayo tulipoisoma tulielewa kuwa nyama ina nguvu ya kuwagawa watu kimatabaka kwa uchu tu wa wenye madaraka, ukiachilia mbali madhara makubwa zaidi ya kiafya.
Uharamu wa nyama umeifanya jamii iwatenge wanyonge na kuwakweza wenye nguvu na mamlaka katika kila Nyanja ya maisha. Angalia, Katika vitoweo vyote nchini na duniani hakuna ambacho ni ghali kama nyama. Wanakula wenye pesa tu. Wapo akina mama wa kambo walioripotiwa kuwalisha nyama watoto wao na kuwalisha maharage wale watoto wa kambo. Katika jamii yoyote wenye mamlaka na nguvu ndio wanao faidi nyama huku wengine wakiambulia mchuzi na mifupa. Ukiandaa sherehe usipoleta nyama watu watakuwa hawakuelewi kabisa toka miguuni hadi utosini. Nyumba Fulani Fulani nyama hupakuliwa na mama. Mboga za aina nyingine ni ruksa yeyote kujipakulia. Wengine wameripotiwa kuwahesabia finyango za nyama wake zao. Wapo pia wanawake waliopewa nyama kilo moja wapike ikafika mezani robo kilo tu, lakini watu watakuambia wapo wanaume wanaokula kilo ya nyama wakiwa baa na huku mke na watoto wanalalia uji. Huku utasikia mtoto kachomwa mikono kisa eti kadokoa nyama, na mikasa kadha wa kadha inayotutahadharisha kuwa nyama itatutoa roho!
Nyama inaua:
Lakini umeona jinsi tulivyoiangalia nyama kwa historian a taswira tu bila kuiangalia madhara yake kiafya ambayo ni lukuki kiasi hayaorodhesheki hapa leo. Nyama inatakiwa iliwe kwa dharura tu na sio kama mlo kamili kwa kuwa nyama ina rekodi ya kuua walaji wake kimya kimya bila wao kujijua kama wanateketea. Mfano watu mia waliokula nyama kilo moja kila mtu kwa siku, watu 30 walikufa baada ya miaka kumi na kuwaacha wengine taabani kwa magonjwa ya moyo kama kisukari, BP, kupooza, ganzi n.k. Si hayo tu, bali magonjwa ya ini, figo na mapafu yalisababisha vifo pia.
Unapokula nyama unaongeza lehemu na mafuta yabisi mwilini ambayo hupenya na kuingia katika mishipa ya damu na kuganda katika kuta zake. Kadiri mgando unavyoongezeka ndivyo njia ya damu inavyopungua na mwisho kuziba kabisa! Sumu hizo zinapoanza kuganda mgonjwa ataanza kuhisi matatizo na akipimwa atakuta mapigo ya moyo yamefeli yaani BP. Kadiri atakavyoendelea kula nyama na kuziba mishipa basi siku moja damu itapita kwa shida sana na ataanza kusikia ganzi sehemu zote zisizopata damu. Mwisho mishipa ikiziba kabisa ndio huwa tunaita mtu amepooza. Maana hakuna damu inayoenda huko tena! Dawa za wagonjwa hawa ni kitunguu swaumu na mafuta ya Sardine toka Ueskimo tu. Kitunguu swaumu niliwahi kukiongelea na nafikiri walionisikia wanaelewa cha kufanya. Ila haya mafuta ya Sardine toka Ueskimo nitayaongelea siku nyingine.
Nyama inadhuru kisaikolojia pia:
Watu wa jamii za wafugaji na walaji wakubwa wa nyama kwa ujumla ni wakorofi sana. Ni waoga na wanaweza wakakudhuru bila kuwa na sababu za kutosha. Hawa jamaa wanaamini kuwa kama huna silaha basi wewe si mwanaume. Hii imetokana na kujilundikia kiasi kikubwa cha lehemu na sumu nyingine toka katika ulaji wa nyama uliokithiri. Hupenda kulala wakiweka silaha kwenye mto ili wajiridhishe kuwa wanalala salama. Kama ni hohehahe ataweka sime hata kisu tu, wakati mwenye pesa ataweka bastola kabisa. Cha kukuchekesha msomaji wangu leo ni kuwa watu hao nchini tumewapa “kibali baridi” cha kutembea na silaha popote! Kama huamini toka wewe na jambia lako mkononi kama utafika popote kabla polisi na watu wa usalama hawajakukamata. Utakamatwa kwa sababu si sheria kutembea na silaha hadharani wote tunalijua hili, lakini hawa ndugu zetu asili yetu imewakubali watembee hata na mikuki na hatuwaulizi kulikoni.
Ikaja pia staili mpya ya kuwaajiri kazi za ulinzi baadhi ya wala nyama hawa. Wenye akili zetu tulibaki midomo wazi tukiamini staili hii itakufa siku si nyingi baada ya wanaowaajiri kukutana na hasara ya kuibiwa kila kukicha. Na kweli leo hii wamesahaulika… Mtu mwenye kiasi kikubwa cha lehemu mwilini ni mwoga, hajiamini, na vitu kama hivyo kwa kuwa damu haitembei ipasavyo. Sasa mtu mwoga atalindaje wakati yeye mwenyewe hajiamini na anatembea na silaha lundo! Yatakuwa maajabu sana.
Madhara ziada ya nyama:
Lakini madhara ya nyama bado hayaishi kama nilivyodokeza hapo awali. Kuna hili ambalo sitaliacha. Ng’ombe, mbuzi, kondoo na mifugo mingine huwa wanakula chochote kitamu kwao wanachokiona ardhini sote tunajua. Lakini tumeshuhudia wanyama hao wakila nailoni, misumari, nywele bandia, na sumu nyingine nyingi tu tunazozalisha binadamu. Sumu hizi tunakutana nazo tunapokula nyama na hakika zinatudhuru vilivyo. Haya, Wanyama hao hao huwa tunawapeleka josho kuua wadudu mwilini. Sumu ya zile dawa ni lazima ukutane nazo ukila nyama. Unalijua hilo? Wachilia mbali sumu hizo, wanyama hupewa dawa wanapopatwa na maradhi tena dawa kali (antibiotics) ambazo utazila na nyama na hatari yake ni kukujengea usugu dhidi ya dawa za kibinadamu pale utakapougua. Ni hatari sana.
Kwa mila na desturi zetu watanzania tuna nunua nyama pale buchani. Utakuta gogo moja limevilia damu na ndilo linalotumika kukatakata nyama. Pale utajiuliza kwanza usalama wa nyama juu ya lile gogo upoje maana hujui ni mti gani, una kamikali gani, zinaua au ni salama na maswali mengine lukuki. Lakini ukimwuliza muuza nyama hatakupa jibu lolote la kukuridhisha pale. Hajui. Upo mtaa Fulani wanaume walikuwa wafanyakazi wa reli ambao walikuwa wakila nyama kwa wingi kuliko wake na watoto wao. Leo hii mtaa hauna baba wote wamefariki. Kwa niaba ya watanzania wote naishauri wizara ya afya kupitia mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kufunga misumeno ya kukatia nyama katika mabucha ya nyama maana ndio utaratibu duniani kote na ndio ustaarabu. Vinginevyo kuna watu wanakufa kimya kimya.
Bado tu nyama inaonekana ina maambukizi dhidi ya maradhi zaidi kuliko mboga za majani, matunda na nafaka. Nyama hubeba wadudu wanaojulikana na wasiojulikana kila unapoila kuja kukuambukiza maradhi ya aina mbalimbali.
Nile ua nisile nyama?
Lakini, nyama bado ina utetezi wa kutosha kuwa na faida za kiafya. Msomaji wangu ona nyama jinsi ilivyo shetani maana haieleweki kama tule, au tusile. Nyama hasa nyekundu ni muhimu sana kwa afya yako lakini, inakubidi ule kidogo sana kama finyango tatu tu kwa wiki, hiyo ni kitaalamu. Ukiifanya mlo rasmi utakufa! Cha ajabu wakati vyakula vingine vikipikwa hupoteza ladha na uthamani wake, kwa nyama mambo ni tofauti kabisa maana ikipikwa, ikichomwa, ikikaangwa ikiokwa nk ladha huwa tamu ajabu na uthamani wake mwilini huongezeka mara dufu. Ukila nyama unajipatia madini ya chuma, zinki, na protini kwa wingi mno.
Wengi wa wagonjwa walioshindwa vitandani wanahitaji sana chuma, zinki na protini kuamka na kupona haraka. Chuma humsaidia mtu kuwa na kinga dhidi ya maradhi sasa kama hukupata virutubisho vya madini hayo basi unaweza kufa hapo kitandani kwa kuwa hukula nyama mpaka chuma imeisha mwilini, hivyo usubiri ugonjwa utakaofuata Anemia na baadaye kaburini. Mgonjwa huyu utamjua kwa dalili hizi: Kapoteza uzito, ngozi imemkauka, mapigo yake ya moyo yanaenda mbio au taratibu sana, Hana pumzi, kifua kinambana, kizunguzungu, hakumbuki tena kitu, kichwa kinamuuma lakini sio malaria, miguu na mikono imekufa ganzi nk.
Usipokula nyama pia tumesema utakosa madini ya zinki. Zinki pia ni kiboko kukupa kinga ya mwili upambane na maradhi sasa kama hamna lazima maradhi yakulaze kitandani. Wanandugu mpeni virutubisho vya zinki kabla hamjampoteza ndugu yenu. Mkitaka kumjua kuwa anahitaji zinki angalieni yafuatayo: Mgonjwa hana utulivu na usiku hapati usingizi, kama ana vidonda haviponi, ana vidoadoa au alama ya nusu mwezi katika kucha zake vidoleni, anakosa nguvu nk. Ukiona dalili hizo hebu wahi umpe virutubisho vya zinki apone vinginevyo mtamkosa.
Lakini pia usipokula nyama unajikosesha protini. Protini ikipungua mwilini utaona mgonjwa anapata tabu kupona vidonda, analalamika viganja vinawaka moto, analalamika miguu inamuuma na muda mwingine atasema tumbo pia linamuuma mara kwa mara, hana nguvu, anashambuliwa na maradhi ya ngozi na wengine hukonda vibaya.
NATIVA ni suluhu:
Hapa Tanzania kuna virutubisho vya kurejesha afya ya mgonjwa huyo haraka na salama. Makampuni mengi yapo kiushindani katika biashara hiyo kila mtu akikushauri kutumia zake. Mimi kwa uzoefu wa maradhi haya nakuelekeza msomaji wangu tumia virutubisho vya kampuni ya NATIVA toka Afrika Kusini kama unatafuta suluhu ya uhakika na haraka kwa mgonjwa wako. Nativa wapo mji mzima na ukihitaji dawa nipigie tu simu nitakusaidia kuzipata.
Wapo wakulima ambao si wafugaji nap engine kupata nyama si kitu rahisi. Kizazi cha Abeli yaani Wakulima wao madini ya chuma, zinki na protini wamejaziwa kwenye mazao yao hivyo utavipata vitu hivi ukila mboga za majani, karanga na jamii yote ya njugu, maharage na jamii zake, matunda kwa wingi nk. Hivyo hakuna sababu ya kungoja upungukiwe na madini hayo mwilini.
Kula nyama msomaji wangu. Lakini usiigeuze kuwa mlo rasmi, kula kama waislamu walivyoambiwa katika msaafu kuwa nguruwe ni haramu aliwe kwa dharura tu. Lakini mimi leo nakuambia wewe kula nyama yoyote kwa dharura tu. Kama Mungu alimkatalia mjukuu wake Kaini sadaka ya nyama aliyomtolea jiulize nyama ina nini?
Bwana pori mmoja alisema hivi: Baba anayekula nyama kwa wingi anajijengea uhayawani wa ndege na wanyama wanaowala wenzao (predetors) msituni. Na ndio maana huwa baba wa aina hii huzinyanyasa familia zao…
Kama umekula nyama kwa muda mrefu na unajihisi dalili zilizopo hapo juu tafadhali tuwasiliane nikusaidie. Kama una mgonjwa wa kisukari, kupooza, presha zote, kupungua na kuzidi uzito pamoja na dalili za maradhi kwa kukosa madini kama nilivyoorodhesha hapo awali basi usisite kunitafuta ili nikupe dawa za uhakika upone.
Asanteni sana kwa kunisoma na mungu awabariki sana.

            "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.  

Thursday 3 January 2013

Afya na Jamii;na Mswahili John Haule-Refusha maisha kwa MAJI!!!!!!!!


Refusha maisha kwa MAJI

Hivi karibuni kumetokea uhaba mkubwa wa maji duniani. Kwa wale tuliozaliwa miaka ya sabini na kurudi nyuma tulishuhudia watoto wakiogelea katika mabwawa yaliyokuwa yamezagaa nchi nzima, mito ilikuwa imejaa mpaka watoto walikuwa wakizama na kufa maji, mabomba yalikuwa yakitoa maji safi na yenye uhakika kila nyumba kwa vile huko yalikokuwa yakitoka kulikuwa kuna chemchem zenye uhakika wa kutoa neema ya maji safi pia kwa wakazi wa vijijini.

Maji yanauzwa:
Nyumba za vijijini kama kawaida zilikuwa na mitungi mikubwa ya kuwekea maji na juu yake kuliwekwa kata ya kuchotea na kunywea maji hayo ambayo yalikuwa na harufu na ladha nzuri ya ajabu isiyoelezeka labda msomaji wangu unisaidie kuielezea. Lakini maji hayo pia yalipatikana kwa gharama ya kupiga hodi, kusalimia na kuomba maji ya kunywa tosha! Vivyo hivyo mijini nako mambo yalikuwa si haba, hakika iliwezekana pia kupiga hodi nyumba yoyote ukasalimia vizuri na kuomba maji ya kunywa na wakakuletea galoni la maji lenye umande toka katika friji pamoja na glasi
ujisevie...
Lakini mambo leo hii yamebadilika. Ndiyo, maji yanauzwa! Si kiyama hiki jamani? Kiyama kwa maana maji ndio uhai wa binadamu sasa uhai unauzwa shilingi ngapi? Yanauzwa! kwenye chupa haya, kwenye mifuko ya plastiki ambayo bila adabu yamepewa jina "maji ya viroba" haya, ya kupimiana kwenye glasi tuambukizane maradhi haya. Yanauzwa...

Maji ya chupa:
Lakini, hebu tuyaangalie kwanza maji haya yanayoitwa ya chupa jinsi yanavyopewa urasmi katika matumizi kwa mipango ya "lifestyle..." Hapana, japo ninaweza nikagusa maslahi ya watengenezaji wa maji ya chupa nchini kwa hili nitawaomba waniwie radhi maana wanywaji ni sisi raia tusiojua kitu na kuwapa wao maisha yetu kirehani-rehani tu. Tabia imejengeka tena ya kukereketa kabisa rohoni kuona watu eti wananunua lundo la maji ya chupa na kuyaweka majumbani familia ipate maji ya kisasa zaidi. Wengine ndio imekuwa kawaida kuzunguka na maji hayo kutishia wenzao kuwa wao hunywa kilicho bora, mambo yao safi.
Maji yaliyofungiwa kitaalamu ni maji maiti. Maji maiti kwa maana maji ni kitiririka na hupoteza maana halisi au hufa mara tu yanapokatazwa kutiririka. Hii inajulikana dunia nzima. Kwa kutambua hilo ndio maana maji yaliyofungiwa huwa yanaharibika yakikaa muda fulani (Expire date) hii inahitaji macho tu kuisoma katika chupa ya maji yoyote. Hivyo kwa kuwa maji yakifungiwa hufa, ndio maana unashauriwa kuyarudishia uhai kiujanja kwa kuyaweka katika ubaridi kabla ya kuyanywa. Na kwa kuhakikisha hilo hebu kunywa maji ya chupa ya moto uisikie ladha yake ilivyokufa. Hapa sisemi kuwa maji ya chupa hayafai, ila najaribu kukufahamisha msomaji wangu kuwa maji ya chupa si rasmi kwa matumizi bali ni msaada tu pale maji rasmi yanapokosekana. Wewe unatakiwa unywe maji hai tena ikibidi ukinge mdomo katika chemchem....

Maji ya Madimbwi:
Binadamu akishikwa na pilika za kiu huwezi kumzuia. Akina mama watakuwa mashahidi wangu wazuri maana kesi za watoto kunywa mafuta ya taa wakidhani ni maji wameshazizoea. Eneo fulani wanaweza wakawa na shida ya maji salama. Hawa wanaweza kuwa wana madimbwi na mifereji ya maji lakini wanayaogopa kuyanywa kwa kuwa yameshawapeleka ahera wengi na wengi wao pale wameshalazwa kwa kuambukizwa maradhi na vimelea vya maradhi vilivyomo mle.
Niliposhiriki "Route Match" na jeshi fulani hapa duniani nakumbuka nilifundishwa kuweka "Iodine pellets" ndani ya mkoba wangu kama kinga ya kunywa maji yoyote mbele yangu kwa kuwa tulitembea siku nane usiku na mchana ndio kikaeleweka. Iodine pellets kwa kiswahili ni "shabu" tena zipo tele masokoni na pengine madukani. hutataabika kuzipata na kama itakusumbua nitafute nikusaidie. Chukua punje moja tu yenye ukubwa wa kunde, tia katika glasi yako yenye maji, acha ikae kwa dakika tano hadi kumi kisha kunywa maji hayo. Utakuwa salama salimini.
Lakini angalia kuwa kunywa maji ya aina hii kunataka upelelezi mdogo kwa kutumia akili ya kawaida kabisa. Inakubidi kwanza kabisa kabla hujafanya chochote chunguza vyanzo vya dimbwi ua mfereji huo kama unatoka kwenye viwanda au makazi ya binadamu? Siri yako msomaji wangu, viwanda na binadamu ni wazalishaji wakubwa wa sumu zisizojulikana hivyo ukigundua vyanzo ni hivyo USINYWE maji hayo.

Maji yenye chumvi:
Kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam hasa maeneo ya Mbagala wanayajua sana maji haya. Wao wanayapata toka katika visima vilivyozagaa maeneo hayo maana ndivyo vyanzo vyao vikubwa vya maji wanayotumia. Maji chumvi kitaalamu si maji salama japo unaweza ukayapata yakiwa safi. Usalama wake si wa kuaminika kwa kuwa ardhi ina utajiri wa madini ya aina nyingi zenye tija kwa binadamu lakini ardhi inabeba pia madini yenye sumu baridi (slow killer agents) ambayo unaweza kuyaonja katika maji na kusema ni "chumvi" bila kujua ni chumvi gani, na kama ni sumu au la.
Kisima kinachotoa maji yenye sumu baridi za aina hii hudhoofisha afya za wakazi wanaolizunguka eneo hilo kila wanapoyatumia maji hayo na siku moja sumu ikiwakolea ndipo mnakutana hospitali wakazi wa mtaa mzima bila kumjua mchawi wenu na huku dakitari akijikuta haujui ugonjwa wenu pia... Mtajikuta mmefanana na wakazi wa mji fulani waliokula nyama toka bucha moja ambalo bila kujua muuza bucha alikuwa anakatia nyama katika gogo la mti wenye asili ya sumu baridi. Ugonjwa wa ajabu mtaa mzima! Walijikuta mtaa mzima wamejaa hospitali, hawajulikani wanaumwa nini..... Tutaizungumza mungu akipenda.
Lakini msomaji wangu siwezi kukuacha yakukute. Unajua kuitenganisha chumvi na maji ya kunywa ni shughuli kubwa, yenye mipango mingi pengine kufungua kiwanda. Hapa ninayo mbinu ya kijeshi na ya kisayansi zaidi unayoweza kujichujia chumvi hiyo na ukapata maji japo kidogo ya kunywa. Fanya hivi: Chukua beseni tia maji hayo haramu yenye chumvi nenda kaweke juani.
Chukua jagi au kikombe kizito kisichoelea weka katikati ya beseni lako lakini angalia maji yasizidi yakaingia kwenye chombo chako na uhakikis ` he chombo hicho hakielei kimetuama kabisa. Chukua karatasi la nailoni ziba juu ya beseni lako kisha funga na kamba ikaze beseni lizibe kabisa. Chukua jiwe dogo saizi ya ndimu weka katikati ya karatasi pale juu ili lilete kauzito fulani.Pamoja na kauzito hako angalia karatasi lisikiguse chombo ulichoweka ndani.
Subiri maji yajichuje, baada ya masaa matatu nenda kafunue karatasi. Utakuta maji yenye chumvi ndani ya beseni yamekuwa ya moto yanatoa mvuke ambao unatengeneza umande kwenye karatasi la nailoni kwa ndani. Sasa, kwa kuwa nje umeweka jiwe katikati, basi umande ule pale ndani utatiririka kuja kati kwenye uzito na kisha ni kuangukia kwenye chombo kitupu ulichokitega kwa ndani. Utakapofungua lile karatasi utakuta chombo chako kina maji na ukiyanywa ni bariiidi kabisa hayana chumvi. Unaweza ukatengeneza chombo kikubwa zaidi kama matumizi yako ni makubwa ila utatakiwa kujua namna ya kupiga hesabu za kifundi. Ukishindwa niite nikusaidie.

Maji ni nini?
Maji ni neema ya kiuumbaji tuliyopewa na mola wetu bure! Shika hilo maana ukituuliza wanasayansi tutakuambia maji ni molekule yenye atomi mbili za haidrojeni na atomi moja ya oxygen. Molekule hizo ndizo zinazounda kitu kiitwacho maji. Hakuna kitu muhimu duniani kama kunywa maji. Lakini kunywa maji safi na salama ndio busara ya kawaida kwa kila mtu. Maji hupatikana toka katika chemchem, mvua na vyanzo vingine vingi tu kama vile maji madini ya visima virefu nk. Umuhimu wa maji kwa binadamu ni mkubwa kupita maelezo kiasi kwamba wataalamu wa afya wa aina zote duniani wamekiri kuwa maji ndio uhai. Unaweza ukanywa, ukaoga, ukapikia, ukaoshea, ukanyweshea n.k. lakini usisahau shughuli za kiroho kama kubatiza, kusilimisha, kutibu, kuapisha na hata ukija kwangu nitakutibu kwa maji tu! ndiyo, nina ibada ya kuomba chochote kiwe mwilini mwako kwa maji na ukapona.

Kwanini unywe maji?
Kuna tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mtu aliyekunywa lita mbili za maji au glasi nane tu kwa siku alitupa dawa za maumivu ya viungo baada ya wiki mbili tu. Mwingine alitupa dawa za kizunguzungu na kuumwa kichwa. Wapo pia walioi
pona bila kujijua maradhi ya aina nyingi sana. Hebu tujiulize maji huwa yanaenda wapi mwilini?
Kwa ujumla binadamu yeyote ni maji kwa 55% hadi 78% kulingana na ukubwa wa umbo lako. Labda nikuambie kuwa maji ni theluthi mbili ya mwili wa binadamu yeyote yule aliye hai hivyo ndio maana watu wakiamua kukuua hukuchinja. wanakata mshipa mkubwa ubebao maji yote ya mwili pale shingoni na ukikauka maji umetuaga!
75% ya misuli ya binadamu ni maji
. Mtu asiyekunywa maji hana nguvu, amini kabisa. kama vipi jiulize mbona mtu akiwa mgonjwa taabani huomba maji na si kinginecho. Umewaona wauguzi wajanja? Kabla ya yote mgonjwa anapewa dripu za maji kwanza. Shangaa...
90% ya ubongo wa binadamu ni maji.
Maji katika ubongo humfanya mtu awe na uwanja mpana mno kifikra katika kufikiri, kutoa maamuzi, kukiri, kusamehe, kushauri na kila kitu kiitwacho fikra sahihi. Alama ya kwanza kwa mtu asiyekunywa maji ni ubishi. Ukiona mtu anakuwa mbishi bila msingi basi mthibitishe kwa kumwangalia sura yake utagundua ni mzee kuliko umri wake... Maji. Ukimsogelea usoni mdomo wake unanuka vyakula vimevunda tumboni, huyo hanywi maji. Jichunguze msomaji wangu. Wewe si kikwazo kwa ubishi kwa wenzio? Kama vipi, kunywa maji.
22% ya mifupa ya binadamu ni maji.
Wazee mliofikia umri wa miaka 50 na kuendelea hebu nawaomba msogee mbele huku. Hapa nawaomba mnisikilize maana nyinyi ndio walalamishi mno wa maradhi ya mifupa lakini kunywa maji hamjui kuwa ni dawa. Ukinywa glasi 8 za maji kila siku kwa wiki mbili tu utanipigia simu kuwa maumivu yameanza kupungua. na ukiendelea kunywa maji kwa miezi mitatu utakuwa umepona sio tu mgongo, miguu, nyayo, kiuno, kizunguzungu na mengineyo, bali hata ujana unarudi! Niamini kabisa uone maajabu.
83% ya damu ya binadamu ni maji.
Hili sina haja sana ya kulijadili tena maana nimelisema hapo mwanzo na nafikiri hata wewe msomaji wangu tutakubaliana tu katika hili hata uwe mtoto mdogo. Usipokunywa maji unauakaribia mstari wa kupungukiwa na damu. Utakaribisha pia maradhi ya moyo kwa vivunde vya unavyokula bila kuviyeyusha na maji vinakuwa sumu kali mwilini na mwisho utakufa

Kazi za maji mwilini:
Maji yana kazi nyingi mno mwilini, na hata hivyo nyingi bado hazijawekwa bayana bado mpaka leo lakini nakupa tu hizi chache ambazo zinatosha kabisa kukushawishi msomaji wangu kuwa mnywaji mzuri wa maji. Maji yanasafirisha virutubisho vyote tunavyokula pamoja na hewa ya oksijeni kwenda sehemu zote za mwili. Maji ndio yanayoirutubisha hewa ya oksijeni katika mapafu, huku yakiwa bado kama korokorokoni kulinda na kukarabati seli zote za mwili.
Ukisikia mtu anasema kichwa kinauma mara kwa mara basi huyo hanywi maji! sio kichwa tu kinachouma pale, hata ngozi ya midomo inabanduka kwa ukavu, ni mwoga, hajiamini n.k. Maji pia hurekebisha joto la mwili, na ndio maana wakati wa jua wauza maji baridi ni neema kwao na wakati wa baridi wauza kahawa nao si haba... Lakini ukinywa maji basi ujue hayataishia mwilini bali yataenda kuchukua nafasi ya yale yaliyotumika na ndio maana ukiuonja mkojo una ladha kali lakini maji ulikunywa yakiwa matamu.
Shangaa. Kabla ya maabara duniani kisukari kilipimwa kwa dokta kuuonja mkojo wa mgonjwa ili aubaini ugonjwa! Upo ushahidi wa kumtibu mgonjwa wa maleria kwa kumpa maji kwa masaa kadhaa tu na akapona. Wazee narudia tena, mgongo, kiuno, miguu, usingizi, na shida zote za uzee kunywa maji glasi nane kila siku kwa wiki mbili uone maajabu! Elewa kuwa, hakika hakuna kisichotegemea maji toka unywele hata kufika miguuni kwenye ukucha wako.

Faida za maji mwilini:
Ukinywa maji utajisikia mwepesi maana yanavunja lehemu na sumu na kuzitolea kwenye mkojo. Ukinywa maji vile vile utapunguza njaa. Wataalamu wa lishe wanasema maji ni kirekebisho cha hamu ya kula ambacho unatakiwa unywe kabla ya kula ili usije vimbiwa kwa kula zaidi. Hivyo utajikuta njaa imepungua. Maji hayo pia ni dawa kwa waliozidiwa na uzito mwili (overweight) maana yanayeyusha mafuta yaliyozidi na kuyatoa kwa mkojo na jasho na kukupunguzia uzito kila siku.
Maji ni tiba binafsi (pocket doctor) pale unapo banwa na mawazo labda umechacha, bosi mkali, biashara imedoda, mwandani anasumbua kichwa chako n.k. kunywa maji mengi kukupunguzia mzigo huo wa mawazo na hakika utaukubali mpango huu. Maji humfanya binadamu aonekane kama mmea ulioota kando ya mto na asiyekunywa huonekana kama mmea uliooteshwa juu ya kichuguu! Wazee, Hakika ujana unarudi. Akina mama, mtaungua sana na hayo madawa ya kemikali kwa kutojua tu. Maji yanafanya kazi kushinda krimu au losheni yoyote ile duniani! Hata mimi natafuta mchumba anayekunywa maji walau glasi sita kwa siku, na nikimtazama kwa macho ajae katika mizani. Anayetaka kuamini aanze kunywa glasi nane tu kwa siku halafu baada ya wiki mbili aone maajabu.
Maji kwa wafanyakazi. Wewe kama ni mfanyakazi bila kujali ni wa sekta gani, jenga tabia ya kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja halafu baada ya majuma mawili tu utanipigia ukikiri ulivyonufaika. Maji yanakufanya uwe mjanja. Kwa kuwa yanamiliki 90% ya ubongo basi mtu asiyekunywa maji ni rahisi kudanganywa, kutapeliwa, kuzubaa, kutoeleweka maamuzi yako n.k. Maji kwa kuwa yanajaa mwilini kukupa afya na nguvu, basi anayekunywa maji si mwoga! Ni mtu anayejiamini na ni mshindi kwa wasiokunywa maji popote: darasani, kazini, biashara, shambani, michezoni n.k. Lakini ukinywa maji, huumwi hovyo! Amini msomaji wangu, wakati nakupa simulizi hii tamu malaika wa heri mbinguni wanapiga vinanda kuisifia nguvu hii kuu ya uumbaji duniani ambako pia Wataalamu wa afya duniani kote wameshikana mikono wakiirusha juu na kusema "REFUSHA, FURAHIA MAISHA KWA MAJI"


John Haule ni mpelelezi binafsi (Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Tuesday 1 January 2013

Afya na Jamii; na MSwahili John Haule-Panda maua yafukuzayo Mbu!


Panda maua yafukuzayo Mbu!

Msimu wa mvua unakuja. Hauji kimya kimya. Ni lazima unakuja na maambukizi makubwa ya malaria yatokanayo na madimbwi yanayozalisha mbu kwa wingi zaidi na mbaya sana mbu jike wa anofelesi huzaliwa wengi pia. Mbu hawa ndio vinara wa kuwaambukiza watu malaria na habari mbaya zaidi nilizonazo mkononi nikuwa wanawake hasa wajawazito ndio waathirika wakuu wa maambukizi ya ugonjwa huu kwa vile huzalisha hewa ya karboni nyingi kuliko wanaume na hivyo kuwavutia mbu hawa ambao wanaambukiza malaria kuwafuata na kuwadunga. Hii ndio siri ya foleni ndefu za akina mama na watoto mahospitalini.
Mbu hawa wapoje?
·        Wana rangi ya kahawia. Akitua katika mwili wako hutega tumbo lake kubwa juu kwa nyuzi 45 na kuleta miguu yake ya nyuma kuwa stendi za kubeba uzito wa damu atakayo kudunga!
·        Huweza kunusa binadamu alipo toka umbali wa mita 50!

Ni kawaida ya msimu wa mvua kuja na hali ya joto inayowavutia watu wengi kutoka nje na kupunga upepo usiku ambao ndio muda muafaka mbu hao kundunga na kuambukiza watu malaria kwa mujibu wa wataalamu. Rumours Africa tumetafiti namna bora ya kuwafukuza mbu toka katika maeneo yote ya nyumba yako, ofisi, hoteli, shule, hospitali, kiwanda na sehemu zingine za kazi ambazo watu hukaa usiku hasa mabaa yanayokesha ambayo pia ni wazalishaji wakubwa wa wagonjwa wa malaria.

Maua yafukuzayo Mbu?
Njia hiyo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizotugharimu mno kuokoa maisha ya watanzania ni kupanda maua yenye harufu na rangi zinazofukuza mbu kama vile rosemary, cintronella, mchaichai n.k.
Tulitafiti pia ni jinsi gani watanzania watazipata mbegu hizi za maua kwa urahisi lakini tukagundua kuwa ni sehemu chache sana wanazoishi watu wenye uelewa hasa wazungu ndio hupanda maua haya bila kuwaambia wengine  na kuwaacha watanzania wengine wapande maua kama urembo tu badala ya dawa na vyakula, na hivyo kujikuta wakipata wakati mgumu kupambana na malaria.

Kwa sasa bado tunafanya mpango wa kutafuta wadau wa kuwekeza kuanzisha bustani ya maua hayo ili tupate mbegu kusaidia watu lakini kwa mwenye haraka zake kujikinga na malaria ni gharama kidogo maana itabidi kusafiri mpaka Peramiho Mission au Uwemba Mission ambako nimeyaona kwa macho mashamba yanayozalisha maua yakiwemo hayo na kusafirishwa ulaya. Pengine labda niliwahi sikia tu kuwa hata Arusha pia kuna mashamba ya maua pia lakini upatikanaji wake kwa kweli siujui.

Maua haya hatimaye yatasambaa. Kila mtu nahisi angependa kupanda maua yenye maana halisi katika maisha na hasa kumlinda yeye, familia, wafanyakazi na wateja pia. Hivyo yeyote ambaye amevutiwa na habari hii na angependa kushiriki kwa namna yoyote kuwekeza katika fursa hii muhimu na adimu kwa taifa letu basi angewasiliana na rumoursafrica kupitia simu namba 0768215956 au email rumoursafrica@gmail.com.

Ujumbe huu unaweza kuwa muhimu kwako, lakini unaweza kuwa muhimu kwa wengine pia hivyo ningekuomba msomaji wangu uufikishe ujumbe huu kwa wapendwa wako ukisisitiza umuhimu wa kujikinga na malaria.

Asanteni kwa kunisoma.

John Haule ni mpelelezi binafsi (Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com


         "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.