Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 21 August 2013

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-Three;Wema Hauozi-Sehemu ya 52!!!!!Tulitoka nje ya lile pango huku tukiwa tumekata tamaa ya kumpata huyu mtu tena,ikizingatia kuwa yeye analifahamu hilo pango lilivyo, na sisi japokuwa tupo wengi, lakini njia za kupita zilihitajia mtu mmoja mmoja,…

Bado tukiwa na matumaini ya kumpata huyo mtu akiwa hai, tuliharakisha kutoka, ili kuungana na wenzetu waliokuwa wakijibisha risasi na huyo jamaa, na baadaye kukawa kimiya, ikiashiria kuwa huenda huyo mtu alishatoka nje,

Swali likawa je kama huyo mtu kawahi kutoka nje, itakuwaje, kwani hatukukumbuka kumuacha askari zaidi ya mwanasheria, wote tulikimbilia kuingia ndani..na je hiyo amri ya kutokutumia risasi huko nje, itawezaje kuepukika, na mtu kama huyo?

Tuendelee na kisa chetu......

Tukajitahidi na sisi kutoka nje kwa haraka haraka, na tulipofika nje, tuliwaona askari wetu wamesimama huku wameelekeza silaha zao upande wa pili, kama wanawinda kitu, na mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka na bastola yake mkononi, akawauliza vijana wake

‘Yupo wapi’ akauliza

‘Mkuu kaingia kwenye hicho kichaka, na cha ajabu haonekani tena, lakini tuna uhakika yupo hapo, na tunahisi kuwa hayupo peek yake,…’akasema mmoja wapo, na wote wakaelekea kwenye hicho kichaka na kwa mbele wakaona watu wawili wakiwa kwenye mapigano na kila mmoja akiwa kamshika mwenzake mkono, ili kuzuia silaha yake, isielekezwe kwake.

Msaidieni mwanasheria, lakini msitumie silaha, kumbukeni tulivyoambiwa, ….’akasema mkuu, huku nay eye akielekea kule ambapo mwanasheria alikuwa akipambana na huyo mtu, na ilikuwa vigumu kuingilia kwani zile silaha walizoshika zingeliweza kufyatuka na kuleta madhara kwa yule ambaye angeliwakaribia, kwahiyo ikawa kutafuta jinsi ya kusaidia.

Mwanadada ambaye alikuwa nyuma akiwa na yule binti, alifika eneo hilo na kuona hiyo hali, na hapo akasema;.

`Mbona mumesimama, hamumsaidi mwenzenu…’akasema mwanadada, akikimbilia kule kwenye mapigano kati ya mwanasheria na huyo jamaa na alipofika tu, akasikia mlipuko wa risasi,…..oh, mwanasheria akapanua mdomo, na kudondoka chini, na yule mtu alipoona hivyo, akainuka kutaka kukimbia, lakini hakuweza hata kuinua mguu.

Risasi ililengwa bara bara, kutoka kichani, na yule mtu akatoa macho ya uwoga, na kudondoka chini, na hapo mwanadada na mkuu, wakawa wameduwaa, ina maana kazi yote imekuwa ni bure, ina maana masharti ya msituni yamevunjwa, na haijulikani ni kitu gani kitatokea.

Mkuu akamkimbilia yule mtu, na kuhakikisha hana silaha, na akamshika kuangalia kama yupo hai, na akainua kichwa kumwangalia mwanadada na kusema;

soma zaidi ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Tupo pia kwenye: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three
https://twitter.com/emuthree"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

1 comment:

emu-three said...

Ndugu wa mimi nashukuru sana na tupo pamoja daima.