Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mswahili na Kisa/Hadithi. Show all posts
Showing posts with label Mswahili na Kisa/Hadithi. Show all posts

Saturday 25 January 2020

Kisa/Hadithi Na Mswahili-Yusuph Mbuguni...

Imeandikwa na Yusuph Mbuguni
"Nakumbuka zamani za udogo wangu,zamani za utoto huko...Mtu mmoja alimpatia babu Yangu Box la nguo chakavu za mitumba kama zawadi,Na katika zile nguo kuukuu nyingi zilikuwa ndogo ndogo,Babu yangu alichukua vipande vya nguo akaviunga akanitengenezea koti kwa kuwa sikuwa na koti kipindi cha baridi,hivyo ni koti ambalo nilijivunia sana,Babu aliniambia Hadithi Ya Yusuph kwenye biblia na koti lake ambalo alikuwa akilivaa,hivyo aliniambia ni kwa namna gani anaamini jinsi koti hilo litakavyoweza kuniletea bahati nzuri katika maisha na kunifanya niwe na furaha,Nikienda kucheza na watoto wenzangu walikuwa wakinicheka nakuona ni kwa namna gani koti langu ni kituko,lakini nilikuwa najaribu kuwaelezea uzuri wa koti langu na kwa namna gani koti langu ni la thamani sana kuliko nguo zao wote japo walikuwa hawanielewi kabisa,japo tulikuwa hatuna kipato lakini nilikuwa najiona tajiri sana na wa maana sana kuliko wote kutokana na koti langu.
wise man yusuph mbuguni

......FUNZO usiangalie wengine wanazungumza nini kuhusu hali yako na Maisha yako wewe ndio unaweza itengeneza furaha yako mwenyewe hata kipindi cha huzuni,Unaweza kujitengenezea hisia za utajiri ukiwa masikini chagua kuwa na furaha na sio huzuni wewe ni Nahodha wa nafsi yako vile unavyotaka.

wise man yusuph mbuguni


Friday 15 April 2016

Kisa cha Leo na Tweve HezronBosi wangu alikuwa akitembelea gari nzuri sana na kila siku ilikuwa ni kazi yangu kumfungulia mlango na kumsalimia.

Lakini tokea niajiliwe na mke wake kuwa kama mlinzi pale kwao hakuwahi kupokea salamu yangu hata siku moja. Nilimuona ananidharau sana ila sikuwa na jinsi.

Siku moja wakati akitoka ndani aliniona nje nikitafuta kama kuna chakula kilichobaki katika dustbean. Lakini kama kawaida yake alinitizama mara moja akaendelea na shughuli zake.

Siku iliyofuata niliona mfuko wa rambo palepale kwenye zile dustbean (ndoo za takataka), ila mifuko ile ilikuwa misafi mno na ndani kulikuwa kuna chakula kizuri tu ambacho pasina shaka nilijua tu kitakuwa kimetoka supermarket.

Sikujiuliza ni nani ametupa me nilifurahi kukipata. Kila siku nikawa nikiona mfuko wa rambo hapo kwenye dustbean ukiwa na vyakula vizuri. Hii ikawa ni utaratibu wa kila siku. Nami sikuuliza ni nani amekuwa akiweka.

Jioni ninaporudi nyumban kwenye makazi duni niliyokuwa nikiishi na familia yangu, nilirudi nacho na nikawa nakula na kushare hicho chakula na familia yangu.

Nikashangaa sana ni nani mpumbavu ambae anatupa chakula kizuri kama kile kila siku? Ila nikajijibu mwenyewe kwamba kuna gepu kubwa sana kati ya masikini na tajiri, wala sikujihangaisha kuuliza.

Siku moja kulikuwa na tatizo kubwa mahala nilipokuwa nikifanya kazi. Niliambiwa kuwa bosi wangu amefariki. Kulikuwa na wageni wengi sana waliokuja pale nyumbani na siku hiyo sikupata chakula katika zile dustbean kama kawaida.

Hivyo nikajua labda mmoja wa wageni labda alikiona na akachukua. Ila hali hiyo ikaendelea kujitokeza baada ya shughuli za msiba kuisha na hata week zingine zilizoendelea sikupata kitu. Na nikaona hali imekuwa ngumu tena kuihudumia familia yangu chakula kwa kuwa nilishakuwa nimewazoesha kuwaletea kila jioni.

Hivyo nikaamua kumuomba mke wa marehemu bosi wangu kwamba aniongezee mshahara ama vinginevyo niache tu kazi maana hali ilikuwa ngumu.

Baada ya kumueleza hilo alilalamika kwanini sikulalamika suala la mshahara miaka miwili sasa imeshapita nije nilalamike leo, kwanini mshahara usitoshe leo? Nilimpa sababu nyingi ila hazikumshawishi hata kidogo.

Mwishoni nikaamua kumueleza ukweli, nikamueleza ishu nzima ya mimi kupata chakula cha bure pale kwenye dustbean na kwa jinsi gani kilinisupport kuilisha familia yangu. Pia nikamueleza kukikosa kwa muda sasa.

Akaniuliza ni lini ilikuwa mwisho wa kukipata hicho chakula katika dustbean? Nikamueleza kuwa baada ya kifo tu cha mumewe sikupata tena chakula.

Nikajiuliza kimyakimya mbele yake, Je inamaana bosi wangu ndio alikuwa akinikiwekea kile chakula kila siku? Hapana sidhani maana kwa jinsi alivyokua akinidharau kwa kutopokea salamu zangu asingekuwa na ubinadamu wa kunipa chakula.

Mke wa bosi wangu akaanza kulia, nikamuomba anyamaze na nikamuomba radhi kwa kumuomba aniongezee mshahara.

Mke wa bosi akaniambia, ninalia kwa sababu nimempata mtu wa saba ambae mume wangu alikuwa akimsaidia kumpa chakula fresh toka supermarket kila siku.

Nilikuwa najua mume wangu anawasaidia chakula watu saba wasiojiweza kila siku, ila nilipata kuwafahamu sita tu. Na siku zote nilikuwa nikitaka nimjue wa saba alikuwa nani ili niendelee kutoa huduma ambayo mume wangu amekuwa akiifanya. Nimefurahi kwa kuwa kumbe ndio wewe!

Kuanzia siku ile nikaanza kupokea chakula tena kama kawaida, ila safari hii mwanae wa kiume ndio alikuwa akituletea nyumbani.

Ila kila nilipokuwa nikimshukuru hakuwahi kunijibu! Kama baba yake tu!

Siku moja alinipa chakula pale nyumbani kwao nikamwambia AHSANTEE kwa sauti ya juu sana, akabaki ananishangaa. Mama yake akatoka nje akaniambia usijisikie vibaya akiwa hakujibu ni kiziwi kama baba yake alivyokuwa kiziwi. Akanieleza kuwa mumewe alikuwa ni bubu pia kiziwi na huyo mwanae nae yuko hivyohivyo.

Nilisikitika sana kwa jinsi nilivyokuwa nikiwawazia vibaya, tofauti na jinsi walivyo.

_______________________________________

Oh! Tumekuwa tukikosea mara nyingi sana kuwahukumu wenzetu bila kujua ni nini nyuma ya kile wanachokifanya. Kuwa na busara katika kuishi na wanadamu wenzako, huwezi jua kila mmoja wetu anapigana vita ngumu.

Kuwa makini, sio kila kitu unajitizama wewe peke yako kabla huja assume mambo ni bora ukauliza. Usikimbilie kutoa maamuzi kabla hujachunguza jambo, huenda siku ukaumia au kupatwa jambo lolote lile baya.

Matatizo mengi katika jamii zetu yanasababishwa na jinsi sisi wenyewe tunavyowachukulia wenzetu. Usihukumu hali fulani ambayo hujawahi kuipitia. Kuwa na busara ya kujifunza, huwezi kujua vyote.

Kuanzia leo tubadili fikra mbaya juu yetu na kwa wenzetu. Kuna vitu viwili katika hadithi hii mosi, usiamini kila unachoambiwa, chunguza zaidi. Na cha pili tambua kwamba kila mmoja unaekutana nae anapigana vita ambayo wewe huijui.

Hima, tuifanye Dunia kuwa mahala salama pa kuishi.

Share

Tweve Hezron

Friday 31 October 2014

Wazo La Leo; Na Mswahili-Emu-three Wa Diary Yangu.....


WAZO LA LEO: Sio kila jambo la heri laweza kirahisi tu, kuna mambo mengine huja na mitihani yake, lakini mwisho wake huwa ni neema, na furaha kama utakuwa mvumilivu na kusimamia kwenye haki.Halikadhalika mambo ya ubaya, yana mvuto wake, usipokuwa makini unaweza kuzama kwenye giza nene, na mwisho wa ubaya ni kudhalilika, na kuumbuka, na kawaida majuto huja baadaye, kama utafanikiwa kujinasua. Tujitahidi sana kuwa makini katika matendo yetu, tusivutike tu kwa tamaa, tuangalie uzuri na ubaya wake kwanza.

kwa Hadithi/Visa/Mikasa ya Maisha,Usikose pitia hapa;http://miram3.blogspot.co.uk/

Dunia Yangu ndiyo hadithi/kisa kinachoendelea sasa....[Sehemu Ya 56]

Twende Pamoja..!!!!

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday 21 August 2013

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-Three;Wema Hauozi-Sehemu ya 52!!!!!Tulitoka nje ya lile pango huku tukiwa tumekata tamaa ya kumpata huyu mtu tena,ikizingatia kuwa yeye analifahamu hilo pango lilivyo, na sisi japokuwa tupo wengi, lakini njia za kupita zilihitajia mtu mmoja mmoja,…

Bado tukiwa na matumaini ya kumpata huyo mtu akiwa hai, tuliharakisha kutoka, ili kuungana na wenzetu waliokuwa wakijibisha risasi na huyo jamaa, na baadaye kukawa kimiya, ikiashiria kuwa huenda huyo mtu alishatoka nje,

Swali likawa je kama huyo mtu kawahi kutoka nje, itakuwaje, kwani hatukukumbuka kumuacha askari zaidi ya mwanasheria, wote tulikimbilia kuingia ndani..na je hiyo amri ya kutokutumia risasi huko nje, itawezaje kuepukika, na mtu kama huyo?

Tuendelee na kisa chetu......

Tukajitahidi na sisi kutoka nje kwa haraka haraka, na tulipofika nje, tuliwaona askari wetu wamesimama huku wameelekeza silaha zao upande wa pili, kama wanawinda kitu, na mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka na bastola yake mkononi, akawauliza vijana wake

‘Yupo wapi’ akauliza

‘Mkuu kaingia kwenye hicho kichaka, na cha ajabu haonekani tena, lakini tuna uhakika yupo hapo, na tunahisi kuwa hayupo peek yake,…’akasema mmoja wapo, na wote wakaelekea kwenye hicho kichaka na kwa mbele wakaona watu wawili wakiwa kwenye mapigano na kila mmoja akiwa kamshika mwenzake mkono, ili kuzuia silaha yake, isielekezwe kwake.

Msaidieni mwanasheria, lakini msitumie silaha, kumbukeni tulivyoambiwa, ….’akasema mkuu, huku nay eye akielekea kule ambapo mwanasheria alikuwa akipambana na huyo mtu, na ilikuwa vigumu kuingilia kwani zile silaha walizoshika zingeliweza kufyatuka na kuleta madhara kwa yule ambaye angeliwakaribia, kwahiyo ikawa kutafuta jinsi ya kusaidia.

Mwanadada ambaye alikuwa nyuma akiwa na yule binti, alifika eneo hilo na kuona hiyo hali, na hapo akasema;.

`Mbona mumesimama, hamumsaidi mwenzenu…’akasema mwanadada, akikimbilia kule kwenye mapigano kati ya mwanasheria na huyo jamaa na alipofika tu, akasikia mlipuko wa risasi,…..oh, mwanasheria akapanua mdomo, na kudondoka chini, na yule mtu alipoona hivyo, akainuka kutaka kukimbia, lakini hakuweza hata kuinua mguu.

Risasi ililengwa bara bara, kutoka kichani, na yule mtu akatoa macho ya uwoga, na kudondoka chini, na hapo mwanadada na mkuu, wakawa wameduwaa, ina maana kazi yote imekuwa ni bure, ina maana masharti ya msituni yamevunjwa, na haijulikani ni kitu gani kitatokea.

Mkuu akamkimbilia yule mtu, na kuhakikisha hana silaha, na akamshika kuangalia kama yupo hai, na akainua kichwa kumwangalia mwanadada na kusema;

soma zaidi ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Tupo pia kwenye: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three
https://twitter.com/emuthree"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Saturday 27 July 2013

Hadithi hii maana yake nini?Mmmhh katika pitapita zangu kutafuta hadithi za Watoto wetu j'mosi, Nikakutana nahii.. kila hadithi ina mafunzo/maana ili watoto/watu wajifunze..jee nini maana ya Hadithi hii?

 Usikose kusikiliza/kuangalia Hadithi,Katuni na mengine meengi yahusiyo Watoto na Jamii.Friday 11 January 2013

Kisa cha Leo na Mswahili Emu-Three;Uchungu wa Mwana Aujuaye ni Mzazi:46!!!!!‘Mama aliniambia kuwa siku aliyokutana na huyo mwanaume ambaye almuokoa ilikuwa kama pigo la pili katika maisha yake, maana hakutarajia kabisa kama itakuwa hivyo….’akaendelea kuongea huyo binti akisimulia kisa hiki.

*******

Turejee kidogo pale tulipoishia:

‘Haya sisi tunaondoka, tunashukuru sana kuwa mtoto amepatikana, na …safari ijayo tutakuja mimi na mume wangu,…’akasema malikia.

‘Na naomba mkija mje na huyo mwanaume aliyeniokoa….tafadhali mtafuteni popote alipo, …’akasema mama Maua.

‘Hilo usijali,..tutakuja naye….’akasema malikia huku akitabasamu,….na akafunua mdomo ili kumuelezea ukweli, ….

Lakini malikia alisita kumwambia ukweli je unafahamu ni kwanini, basi tuendelee na kisa hiki ili tujue ni kwanini malikia alisita kuelezea ukweli huo.

********

Wakati huo yule punda aliyempanda malikia akaanza kuondoka. Malikia aligeuka nyuma na kumwangalia yule mwanamke akiwa kasimama pale mlangoni huku akiwa kambeba mtoto wake, akatabasamu.

‘Mume wangu atafurahi sana kuwa hatimaye mtoto yupo mikononi mwa mama yake…’akasema na aliombea akifika huko kwao akute mambo yako shwari, ili safari ijayo warudi hapo pamoja, na kumtembea huyo mama, na ikiwezekana wamchuke wakaishi naye huko kwao msituni.

‘Lakini sheria hazimtaki…..’akasema na kuwaza

‘Sheria gani hizo za kubagua watu…kwani ana kosa gani, na kama ana kosa …hilo kosa hakulifanyia hapo, …hapana lazima hii hali iondolewe’akasema huku wakiendelea na safari ya kurudi kwao msituni. Na wakati wanaingia msituni, akakumbuka nyumbani kwao…..

‘Natamani sana nirudi niwaone ndugu zangu tena..lakinihaiwezekani, najua ipo siku nitarudi…’akasema huku machozi ya kimlenga lenga….

Wakati machozi yakimlenga , wakafika sehemu ambayo anaikumbuka sana, akasimamisha msafara, akaterema kwenye punda wake, na kuusogela ule mti. Akautizama na kuitafuta ile kamba ….huku akikumbuka tukio la siku ile….

Akakumbuka jinsi alivyomkimbia baba yake ….hebu turejee sehemu hiyo kidogo….....

Inaendelea ingia;

Ni Mswahili;Emu-Three na Diary Yangu[Yake!!]

                           

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Friday 30 November 2012

Kisa Cha Leo; na Mswahili Emu-Three-Uchungu-wa-mwana-aujuaye-ni-mzazi-31!!!!Waungwana; Si Mwingine ni Emu wa 3. "Kisa cha Leo" ni Uchungu wa Mwana.....Inaendelea,Si mimi ni yeye  na 

DiaryYangu [Yakeeeee!!!!]Marejeo: Tukumbuke hiki kisa alikuwa akisimulia yule binti niliyekutana naye akiwa kajiinamia kashika shavu, ….akiwa kasimuliwa na mama yake. Huyu binti kwa hali aliyokuwa nayo, alifikia hadi kukusudia hata kujiua.

Binti aliona kabisa , kuwa maisha kwake hayana thamani tena. Na binadamu anapofikia hapo, ujue kweli kuna jambo…nani asiyependa kuishi, hata yule anayekusudia kujiua, muda roho ikitaka kutoka, huwa anajitahidi kuiondoa ile kamba shingoni, lakini anakuwa keshachelewa, siku yake imeshafika, inabidi aonje umauti…na jamani kutoka kwa roho sio kitu cha mchezo.

Katika kisa hiki utagundua kuwa kuna mwanamama hapo ambaye ana jina hilo hilo, …jina ambalo nilisikia akiitwa huyu binti na mama yake mdogo, wakati namuulizia kuhusu maisha yake, kwanini imetokea hivyo, sasa tuendelee na kisa chetu, ………….

*********

‘Mimi sikujua kabisa huyo baba mlevi ninayeishi naye sio baba yangu wa kunizaa, kumbe alikuwa ni baba wa kufikia, hayo niliyajua baadaye, wakati najiandaa na safari ya kuja kuishi huku Dar, mji ambao kila mmoja kule kijijini alitamani kuja kuishi.

Mama yangu aliniambia huyo baba ndiye aliyekuja kumuokoa pale alipoachwa pale porini…..ili wenzake wafike huko wanapohitajika kwa wakati muafaka, na baadaye watarejea kumchukua, au kumtafutia sehemu ya kumuhifadhi.

Wakati kaachwa pale, akiwa kachoka, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu, baada ya safari ndefu, baada ya mapigano, na yeye kujitolea kumsaidia huyo jamaa aaliyeficha sura yake kwa kofia ya ngozi ….na haat kujeruhiwa tena…akawa anatamani kulala tu.

‘Wewe pumzika hapa, na utakula nyama hii…mimi nahitaji huko kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu walikuja kuniua, lakini tumeweza kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka, halafu nitarudi kuhakikisha kuwa upo mikono salama….’akasema.

‘Sawa wewe nenda tu, na nakutakia mafanikio mema, mungu yupo pamoja na wewe, ila ninachokuomba ni kuhusu mtoto wangu…..naomba siku ukija, uje na mtoto wangu, usije bila ya kuwa na mtoto wangu….’akasema huyo mwanamama.

‘Naahidi nitafanya hivyo…na wewe hakikisha unakuwa salama, usiondoke, hapa, …hapa ni salama zaidi’akasema na akambusu kichwani na kuondoka. Huyu mwanamama alikaa pale kwa muda, halafu akaona akatafute maji ya kuoga, maji yaliyokuwepo pale yalikuwa ni machache, ….........
Endelea kusoma Zaidi,Ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

                           "Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaaana.

Monday 19 November 2012

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-3-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 25!!!!!!Kwa marejeo: Kais alipohisi kuwa huyo mwanaume, aliyemuona na yule mwanamke, ni askari wa mzee Hasim, alikimbia….., je alikimbilia wapi, na huko alipokwenda aliishia wapi, ukumbuke kuwa binti huyo alikuwa mja mzito, je ujauzito wake uliishia wapi….tuendelee sehemu hiyo ya Kaisi……..

Kais, alipozindukana alijikuta yupo kwenye kitanda, na wakati hupo tumbo lilikuwa likimuuma sana, na harufu aliyoisikia hakuwahi kusikia kabla, akageuza kichwa huku na kule, lakini hakuona mtu kwa upeo wa mcho yake. Akainua kichwa na , kwa mbali akaona watu wamevaa nguo nyeupe, moyoni akajua ni malaika, akakumbuka hadithi alizowahi kusimuliwa za malaika kuwa ni wao ni weupe, na kwasababu hawana dhambi, kila kitu chao ni cheupe.

‘Ina maana nimeshakufa nipo mbinguni,…nipo peponi na malaika’akawaza na kabla hajaweza kuinua kichwa vyema, mara akahisi kuna watu wameshikilia miguuni yake, na sauti zikawa zinaongea, mmoja akasema,;

‘Huyu tusipomfanyia upasuaji, tunaweza tusiwaokoe wote’

Kais akawaza hawa malaika wanataka kumfanya nini, kumfanyia upasuaji, haiwezekani, kwao hakuna kitu kama hicho, wanaamini kuzaa ni kwa njia ya kawaida tu, kuna dawa unakunywa, na haichukui muda kujifungua, na kabla hajajua nini kinachoendelea, akahisi tumbo likaanza kumuua, liliuma sana, maumivui ambayo hakuweza kuyavumilia akaanza kupiga ukulele.

Mmoja wa wale, watu ambao yeye aliwaona kama malaika, wakaja na kumshika vyema, na mmoja akawa kashika sindano,..Kais aliogopa sana, lakini hakuweza hata kujitetea, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu hata ya kuinua mkono, kutokana nay ale maumivu, akapigwa sindano, ambayo ilimfanya atulie, na kuzama kwenye giza, …alipozindukana akasikia kitoto kikilia..

‘Mtoto wako mnzuri ana afya njema,..’ akaambiwa, na alipogeuza kichwa pembeni, akaona kitoto kimelazwa kwenye kitanda kidogo pembeni yake. Kilikuwa cheupe, kizuri, akatabasamu, na akainua mkono na kukishika. Baadaye aliwageukia wale watu ambao kipindi cha nyuma aliwaona kama malaika, lakini sasa akili ilikuwa imetulia, na ile hali ya mwanzo aliiona kama ndoto, akasema; kusoma zaidi ingiahttp://miram3.blogspot.co.uk/


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima

Tuesday 9 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili;Emu-Three-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 5!!!!!


Maua alikuwa katulia kwenye chumba huku akimuomba mungu wake, mwanzoni alikuwa anashindwa hata aombe nini. Akawa anajiuliza je nimuombe Mungu  anisamehe kwa hayanmakosa niliyofanya, lakini akajiuliza kichwani makosa gani, na kama ni makosa mbona ni yeye peke yake ndiye anayeadhibiwa, mbona mwenzake waliyeshirikiana naye , hayupo, je na yeye hastahili kuadhibiwa.

Alipowaza hilo akamkumbuka mwenzake, akakumbuka jinsi walivyokuwa wakiandikiana barua, lakini ghafla akawa hamjibu barua zake tena, hasa pale alipoandika kumuelezea jinsi gani anavyojisikia,na kumwambia anaogoa isije ikawa ni mimba. Ilikuwa barua ya mwisho kumwandikia, na hakuweza kupata jibu, na hata alipoandika nyingine, na nyingine, hakiweza kupata jibu kwa mtu aliyetokea kumpenda sana.

‘Hivi huyu mtu yupo aua kapotolea nchi gani, nakumbuka mara kwa mara anakwenda Arusha kwa mjomba wake, ambaye ni tajiri mmoja wa madini,na nia na lengo lake na yeye ni kujiunga kweney biashara hiyo, lakini kwanini asimwambia, au kumjibu baraua zake,lazima nimtafute tusaidiane hili tatizo’akasema huku akiangalia nje kwa kupitia dirishani.

Akawa bado anawaza ni mambo gani kwasasa anahitajika kumuomba Mungu wake, `Au  nimuombe Munguwangu anisaidie nisiweze kuangukia kwenye mikono ya baba, baba ambaye anataka kuitoa roho yangu, bila makosa, ‘ akasema na alipofikia kuwaza hili akatikisa kichwa na akili yake ikawa anajiuliza ‘Ina maana kweli mimi sio mkosaji,hivi kweli sistahili kuadhibiwa kwa kosa hili?’akatulia na kujarabi kutafakari zaidi. Hapo akakumbuka kauli ya baba yake, ambaye kila mara wakiwa naye alipenda kumuasa nayo;

‘Binti yangu nakupenda sana, na jinsi ninavyo kupenda,  nisingelipenda ukaja kuvunja huu upendo nilio nao juu yako, nakuomba  sana usije ukaniangusha, maana kila mtu hapa kijijini anakuona kama mtoto wa mfano, na mimi huwa natamba kwao kuwa  wewe ni binti mwenye akili, binti mwenye nidhamu, binti ambaye hakuna anayeweza kumfikia kwa jinsi ulivyo hapa kijijini’ilikuwa sauti ya baba yake.

Baba yake kweli alikuwa akimpenda, lakini sio ule upndo wa kumdekeza, kwani akifanay kosa alikuwa akiadhibiwa, mpaka anawaza vibaya kuwa baba yake anataka kumuua, na sio kweli anampenda kiasi hicho. Lakini kaam hajafanay kosa, baba yake alikuwa akribu sana na yeye na kila mwaka wakifanya sherehe za shule anakwenda kushuhudia mtoto wake akipewa zawadi ya kuwa mtoto wa kwanza, na wakirudi nyumbani huchinjiwa kuku kama zawadi maalumu. Na alipofaulu kwenda sekondari, baba alimnunulia zawadi nyingi sana.

`Sasa huyu ndiye binti , binti ambaye baba alikuwa akitamba kuwa ndiye binti wa mfano..’, Maua akajikuta akifuta machozi, akaliangalia tumbo lake, ambalo bado lilikuwa halijaonyesha dalili yoyote kuwa kuna kiumbe ndani , akakunja uso na kuanza kujpiga piga tumboni huku akilaani,i hicho kiumbe kilichopo tumboni,utafikiri ndicho chenye makosa akasema;Inaendele ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Diary 

Yangu

Yakeeeeeeeee!!!!!

"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima...

Tuesday 2 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili ,Emu-Three;Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi!!!!!!
Katika maisha haya, unaweza ukakutwa na majanga na kufikia hata kukufuru, ukizania wewe tu ndiye unayeonewa, lakini ugumu na matatizo ya kimaisha yapo katika watu wengi, ila ni kwasababu tu hujawahi kusikia au kukutana na watu kama hao. Nalisema hili pale nilipokumbuka kisa cha huyu mwanadada ambaye nilimkuta akiwa kainama upembezoni mwa nyumba huku kashika shavu na michirizi miwili ya machozi ikiwa imeshajichora mashavuni.

Niliingiwa na huruma nilipoona ule ukaaji aliokuwa kaka huyo binti, hasa kwa binti mkubwa kama yule, na ile nguo nyepesi aliyovaa asubuhi kama ile licha ya baridi kali.  Pembeni yake kulikuwa na ndoo ya maji, iliyo tupu. Niliingiwa na moyo wa huruma nikamsogelea kwa tahadhari, kwani dunia hii haina wema, unaweza ukajitia una huruma, na huruma hiyo ikakutokea puani.

Wakati namsogelea kwa tahadhari,nilikumbuka kisa cha jamaa yetu mmoja, ambaye alienda kusota jela, baada ya kujifanya msamarai mwema, kwa kumoenea huruma binti kama huyu. Yeye alimkuta huyo binti  njiani, akiwa analia, na hali aliyomkuta nayo, ilikuwa ya kusikitisha, kwani kama alivyodai, ana siku mbili , kula hali, anachoambulia ni makombo. Yule jamaa yangu alipomuona kwenye hiyo hali akamchukua kwake, lakini  kabla hajatahamaki polisi hawa wapo mlangoni pake.

‘Tumeskilia wewe umemchukua msichana  wa watu, umemficha hapa kwako , yupo wapi?’ akaulizwa.

‘Afande, mimi nimemuona huyu binti njiani, akiwa analia, nikajaribu kumuuliza ana tatizo gani, akawa hanijibu, lakini kwa hali aliyokuwa nayo ilionyesha dhahiri kuwa ana njaa, nikaona nimchukue kwangu, ili anywe chai, halafu atanielekeza kwao, au polisi ikibidi, kwani hali aliyokuwa nayo hata wewe ungelimuonea huruma, inaonyesha wazi ana njaa, na pia mahala kama pale nilipomkuta hapana usalama’akajitetea huyo jamaa yangu.

Wale maaskari wakaangua kicheko, na kusema;
‘Hivi wewe kweli una akili, ukutane na binti wa watu,tena msichana, badala ya kwenda naye polsi unampeleka kwako, kwanza wewe una mke, au ndio ulitaka awe mkeo wa muda baadaye umeshamuharibia maisha yake unamtelekeza!’ akasema yule askari  huku akiangalia huku na kule kama ataona mke wa jamaa yangu huyo.

‘Mimi ninaye mke, na kwasasa hayupo kaenda kwao,  hivi sasa nipo peke yangu, alikwenda kwao kusalimia.’akajitetea jamaa yangu huyo

‘Kwahiyo ukaona uchukue mwanya huo, kutorosha mabinti za watu,wewe huoni hilo ni kosa kubwa, linalinganishwana kuteka nyara. Na wewe hujui kuwa utakuwa na mtoto kama huyo siku za baadaye? 

’akasema yule askari huku akitikisa kichwa na mwenzake akatikisa kichwa kukubaliana naye.

‘Jamani, huyu binti wala sijamtorosha, sivyo kabisa mnavyozania nyie, kwanza yupo hapo ndani anakunywa chai, hebu ingieni mumuhoji wenyewe‘akasema na wale maaskari wakaingia ili kuhakikisha, na wakamkuta yule binti akiwa anakunywa chai, na alipowaona wale maaskari, akakurupuka pale mezani akitaka kukimbia, wakamshika.

‘Wewe ulikuwa wapi muda wote huo, ulikuwa na huyu muhuni, ndiyo yeye anayekuhadaa kila siku ehe, utatumabie vyema?’akasema yule askari huku kamkazia macho yule binti.

Inaendelea....Kusoma zaidi ingia;
http://www.miram3.blogspot.com


Kwa Visa vya kusisimua na kufundisha, Ungana na EMU-Three... Na;
Diary Yangu.
Yakeeeee!!!!!!!!!

"Swahili NA Wswahili" Pamoja Daima

Friday 17 August 2012

Kisa cha Leo ni Emu-Three na Mbio za Sakafuni,Huishia Ukingoni!!!!


Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 4

Waungwana leo nimewaletea Mswahili; Emu-Three na Diary Yangu[Yake]
ANASEMA;Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za maisha 
(diaries), 
visa na matukio na yale unayopenda kuchangia na wenzako (mijadala),
 maneno ya hekima,
 kusaidiana na pia kutoa dukuduku lako (kilio chako). 
Soma na uchangie chochote kwa 
kutoa maoni (comments) yako,
 au tutumie kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

Tupitie Kisa hiki kidogo, hii ni Sehemu ya 4:Kila mfanyakazi tunayemchukua hakai hapa nyumbani, sasa nimechoka kabisa kutafuta mfanyakazi wa nyumbani, naona ni heri nijifanyie kazi zangu mwenyewe, kwanza nililelewa kama mfanyakzia wa nyumbani…’akasema mke wangu.

Kipindi hicho maisha yetu yapo juu, tuna kila kitu, …lakini maisha ya ndani yalikuwa na mitihani yake, na ilionyesha wazi kuwa tulihitaji msaidizi, ili na yeye apate muda wa kufuatilia miradi yetu.Niliinuakichwa na kumtizama kwa macho ya huruma,maanaalikuwa mtu wa pilikapilika, shughuli zandani, shughuli zamiradi, shughuli za kijamii, zote alikuwa akijitahidi kujumuika nazo.

Nilimwangalia na kutabasamu, na hapo nikakumbuka siku za nyuma, wakati akiwa binti, wakati nampigania kumpata, ilikuwa kama kampeni za siasa ambazo nilikuwa nikipambana nazo, na hata siku anaingia kwangu kama mke wangu sikuamini.
‘Unanikumbusha mbali sana mke wangu, sijui kama ningekukosa ingelikwuaje…’nikasema.Inaendelea;kuanzia Sehemu ya 1-hii ya 4 na Kuendelea na Kisa hiki ingia;http://miram3.blogspot.co.uk
Mpendwa Unalolote la kuongezea kwa mwandishi huyu?Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.Karibu sana.


Hongera sana Emu-Three kwa Kazi zako,Mungu Azidi kukubariki sana sana kwa Kazi za Mikono yako na kila lililo Jema.Tunakutakia Swaumu Njema!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.