Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 19 November 2012

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-3-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 25!!!!!!Kwa marejeo: Kais alipohisi kuwa huyo mwanaume, aliyemuona na yule mwanamke, ni askari wa mzee Hasim, alikimbia….., je alikimbilia wapi, na huko alipokwenda aliishia wapi, ukumbuke kuwa binti huyo alikuwa mja mzito, je ujauzito wake uliishia wapi….tuendelee sehemu hiyo ya Kaisi……..

Kais, alipozindukana alijikuta yupo kwenye kitanda, na wakati hupo tumbo lilikuwa likimuuma sana, na harufu aliyoisikia hakuwahi kusikia kabla, akageuza kichwa huku na kule, lakini hakuona mtu kwa upeo wa mcho yake. Akainua kichwa na , kwa mbali akaona watu wamevaa nguo nyeupe, moyoni akajua ni malaika, akakumbuka hadithi alizowahi kusimuliwa za malaika kuwa ni wao ni weupe, na kwasababu hawana dhambi, kila kitu chao ni cheupe.

‘Ina maana nimeshakufa nipo mbinguni,…nipo peponi na malaika’akawaza na kabla hajaweza kuinua kichwa vyema, mara akahisi kuna watu wameshikilia miguuni yake, na sauti zikawa zinaongea, mmoja akasema,;

‘Huyu tusipomfanyia upasuaji, tunaweza tusiwaokoe wote’

Kais akawaza hawa malaika wanataka kumfanya nini, kumfanyia upasuaji, haiwezekani, kwao hakuna kitu kama hicho, wanaamini kuzaa ni kwa njia ya kawaida tu, kuna dawa unakunywa, na haichukui muda kujifungua, na kabla hajajua nini kinachoendelea, akahisi tumbo likaanza kumuua, liliuma sana, maumivui ambayo hakuweza kuyavumilia akaanza kupiga ukulele.

Mmoja wa wale, watu ambao yeye aliwaona kama malaika, wakaja na kumshika vyema, na mmoja akawa kashika sindano,..Kais aliogopa sana, lakini hakuweza hata kujitetea, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu hata ya kuinua mkono, kutokana nay ale maumivu, akapigwa sindano, ambayo ilimfanya atulie, na kuzama kwenye giza, …alipozindukana akasikia kitoto kikilia..

‘Mtoto wako mnzuri ana afya njema,..’ akaambiwa, na alipogeuza kichwa pembeni, akaona kitoto kimelazwa kwenye kitanda kidogo pembeni yake. Kilikuwa cheupe, kizuri, akatabasamu, na akainua mkono na kukishika. Baadaye aliwageukia wale watu ambao kipindi cha nyuma aliwaona kama malaika, lakini sasa akili ilikuwa imetulia, na ile hali ya mwanzo aliiona kama ndoto, akasema; kusoma zaidi ingiahttp://miram3.blogspot.co.uk/


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima

No comments: