Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 28 November 2012

Watanzania waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera !!!
Watanzania waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera !
Jumamosi 08-December 2012 mjini Berlin,UjerumaniUmoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote
wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya kumuaga
Mheshimiwa balozi  Bw. Ahmada Ngemera ambaye anamaliza mda wake wa kufanya kazi,
Afla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .
Mhe.Balozi bwana Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania
wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa
karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania
 wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo
 Mhe.Balozi Bw.Ngemera na msaidizi wake Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania 
waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu 
ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya
 ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha 
watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia
 watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda
ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU)  Umoja ambao ni chombo
 cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia !
UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,
TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
 kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.
VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.: 59641   BLZ: 71160161
Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera


Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
simu namba +491734297997 au Katibu simu namba 01734744265 .
No comments: