Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 29 October 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 43....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele: “Mkuu ni Artemi wa Efeso!” Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda wa saa mbili. Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, “Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Hakuna anayeweza kukana mambo hayo. Hivyo basi, tulieni; msifanye chochote bila hadhari. Mmewaita watu hawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumba ya mungu wala kumtukana mungu wetu wa kike.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Kama, basi Demetrio na wafanyakazi wake wana mashtaka yao kuhusu watu hawa, yapo mahakama na wakuu wa mikoa; wanaweza kushtakiana huko. Kama mna matatizo mengine, yapelekeni katika kikao halali. Kwa maana tungaliweza kushtakiwa kwa kusababisha ghasia kutokana na vituko vya leo. Ghasia hii haina msingi halali na hatungeweza kutoa sababu za kuridhisha za ghasia hiyo.” Baada ya kusema hayo, aliuvunja mkutano.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Mungu aahidi kuwaokoa watu wake
1Mwenyezi-Mungu aliyewaumba enyi watu wa Yakobo,
yeye aliyewafanya enyi watu wa Israeli, asema:
“Msiogope, maana mimi nimewakomboa;
nimewaita kwa jina nanyi ni wangu.
2Mkipita katika mafuriko,
mimi nitakuwa pamoja nanyi;
mkipita katika mito,
haitawashinda nguvu.
Mkitembea katika moto,
hamtaunguzwa;
mwali wa moto hautawaunguza.
3Maana mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,
Mungu Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wenu.
Nitaitoa nchi ya Misri iwe fidia yenu,
nitaitoa Kushi na Seba ili mwachwe huru.
4Kwa vile mna thamani mbele yangu,
kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda,
mimi nawaacha watu kusudi niwapate nyinyi,
nayaachilia mataifa badala ya maisha yenu.
5Msiogope maana mimi nipo pamoja nanyi.
“Nitawarudisha wazawa wenu toka mashariki,
nitawakusanyeni kutoka magharibi.
6Nitaiambia kaskazini, ‘Waache waondoke’,
na kusini, ‘Usiwazuie’!
Warudisheni watu kutoka mbali,
kutoka kila mahali duniani.
7Kila mmoja hujulikana kwa jina langu,
niliwaumba wote na kuwafanya
kwa ajili ya utukufu wangu.”
Israeli ni ushahidi wa Mwenyezi-Mungu
8Waleteni mbele watu hao,
ambao wana macho lakini hawaoni
wana masikio lakini hawasikii!
9Mataifa yote na yakusanyike,
watu wote na wakutane pamoja.
Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia?
Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa?
Wawalete mashahidi wao
kuthibitisha kwamba walifanya hivyo.
Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”
10Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu;
niliwachagua muwe watumishi wangu,
mpate kunijua na kuniamini,
kwamba ndimi peke yangu Mungu.
Kabla yangu hajapata kuwapo mungu mwingine,
wala hatakuwapo mungu mwingine.
11“Mimi peke yangu ndimi Mwenyezi-Mungu,
hakuna mkombozi mwingine ila mimi.
12Nilitangaza yale ambayo yangetukia,
kisha nikaja na kuwakomboa.
Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo,
nanyi ni mashahidi wangu.
13Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima.
Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu;
hakuna awezaye kupinga ninayofanya.”
Kukombolewa kutoka Babuloni
14Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu,
Mtakatifu wa Israeli, asema hivi:
“Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni.
Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake,
na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo.
15Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu;
Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.”
16Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Wakati mmoja nilifanya barabara baharini
nikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.
17Nililipiga jeshi lenye nguvu,
jeshi la magari na farasi wa vita,
askari na mashujaa wa vita.
Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena,
niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa.
Sasa nasema:
18‘Msiyanganganie mambo yaliyopita,
wala msifikirie vitu vya zamani.
19Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya.
Kinafanyika sasa hivi,
nanyi mtaweza kukiona.
Nitafanya njia nyikani,
na kububujisha mito jangwani.
20Wanyama wa porini wataniheshimu,
kina mbweha na kina mbuni,
maana nitaweka maji nyikani,
na kububujisha mito jangwani,
ili kuwanywesha watu wangu wateule,
21watu niliowaumba kwa ajili yangu mwenyewe,
ili wazitangaze sifa zangu!’
Dhambi ya Israeli
22“Lakini ewe taifa la Yakobo, hukuniabudu mimi;
enyi watu wa Israeli, mlinichoka mimi!
23Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa,
wala kuniheshimu kwa tambiko zenu.
Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka,
wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.
24Hamkuninunulia manukato kwa faida yenu,
wala kuniridhisha kwa nyama nono za tambiko.
Badala yake dhambi zenu zimekuwa mzigo kwangu,
mmenichosha kabisa kwa makosa yenu.
25Walakini mimi ndimi niliyefuta makosa yenu kwa heshima yangu,
ndimi niyafutaye makosa kwa ajili yangu mwenyewe,
na wala sitazikumbuka dhambi zenu.
26“Niambie kama mna kisa nami,
njoo tukahojiane;
toeni mashtaka yenu ili tuuone ukweli wenu!
27Babu yenu wa kwanza alitenda dhambi,
wapatanishi wenu waliniasi.
28Kwa hiyo niliwafanya haramu wakuu wa mahali patakatifu
nikawaacha watu wa Yakobo waangamizwe,
naam, nikawaacha Waisraeli watukanwe.”

Isaya43;1-28

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: