Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 4 October 2019

Kikombe Cha Asubuhi;Isaya 26....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kisha nikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa na moto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwa kwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimama kando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivyopewa na Mungu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Nguvu, matendo yako ni makuu na ya ajabu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Wimbo wa ushindi
1Siku ile watu wataimba wimbo huu katika nchi ya Yuda:
Sisi tuna mji imara:
Mungu anatulinda kwa kuta na ngome.
2Fungueni malango ya mji,
taifa aminifu liingie;
taifa litendalo mambo ya haki.
3Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti,
wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea.
4Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zote
kwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.
5Amewaporomosha waliokaa pande za juu,
mji maarufu ameuangusha mpaka chini,
ameutupa mpaka mavumbini.
6Sasa mji huo unakanyagwakanyagwa
kwa miguu ya watu maskini na fukara.
7Njia ya watu wanyofu ni rahisi;
ewe Mungu mwadilifu, wasawazisha njia yao.
8Katika njia ya maamuzi yako
tunakungojea ee Mwenyezi-Mungu;
kulikumbuka jina lako ndiyo tamaa yetu.
9Moyo wangu wakutamani usiku kucha,
nafsi yangu yakutafuta kwa moyo.
Utakapoihukumu dunia,
watu wote ulimwenguni watajifunza haki.
10Lakini waovu hata wakipewa fadhili,
hawawezi kujifunza kutenda haki.
Hata katika nchi ya wanyofu,
wao bado wanatenda maovu,
wala hawajali ukuu wako wewe Mwenyezi-Mungu.
11Ee Mwenyezi-Mungu umeinua mkono kuwaadhibu,
lakini maadui zako hawauoni.
Waoneshe uwapendavyo watu wako nao wataaibika.
Moto wa hasira yako uwateketeze maadui zako!
12Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, umetupatia amani;
umefanikisha shughuli zetu zote.26:12 umefanikisha … shughuli zetu zote: Au umetutendea kadiri ya matendo yetu.
13Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
tulipata kutawaliwa na watu wengine na miungu yao,
lakini twakiri wewe pekee kuwa Mungu wetu.
14Watu hao wamekufa, wala hawataishi tena;
wamekuwa mizimu, wala hawatafufuka.
Maana wewe umewaadhibu na kuwaangamiza,
hakuna atakayeweza kuwakumbuka tena.
15Umelikuza taifa letu, ee Mwenyezi-Mungu,
naam, umelizidisha taifa letu.
Umeipanua mipaka yote ya nchi,
kwa hiyo wewe watukuka.
16Ee Mwenyezi-Mungu, walipotaabika walikutafuta,
walikuomba msaada ulipowaadhibu.26:16 ulipowaadhibu: Maana yake katika Kiebrania si dhahiri.
17Kama vile mama mjamzito anayejifungua
hulia na kugaagaa kwa uchungu,
ndivyo tulivyokuwa kwa sababu yako, ee Mwenyezi-Mungu.
18Sisi tulipata maumivu ya kujifungua
lakini tukajifungua tu upepo!
Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya nchi yetu,
hatukuweza kuongeza idadi ya watu katika nchi.
19Wafu wako wataishi tena,
miili yao itafufuka.
Wanaolala mavumbini wataamka na kuimba kwa furaha!
Mungu atapeleka umande wake wa uhai,
nao walio kwa wafu watatoka hai.
Baada ya dhiki faraja
20Njoni watu wangu, ingieni majumbani mwenu,
mkajifungie humo ndani.
Jificheni kwa muda mfupi,
mpaka ifike ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
21Maana Mwenyezi-Mungu aja kutoka kwake juu,
kutoka makao yake huko mbinguni;
kuwaadhibu wakazi wa dunia kwa uovu wao.
Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa,
ila itaufichua umwagaji damu wote.


Isaya26;1-21

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: