Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 26 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 27...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Mtu yeyote anayegusa kitu chochote kilicho najisi, au kitu najisi cha mtu, au mnyama aliye najisi, au kitu chochote najisi ambacho ni chukizo, akila nyama ya sadaka ya amani aliyotolewa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: Msile mafuta ya ng'ombe au ya kondoo au ya mbuzi. Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Mtu yeyote akila mafuta ya mnyama aliyetolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atatengwa na watu wake. Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

1 Taz Yak 4:13-16 Usijisifie ya kesho,
hujui nini kitatokea leo mpaka kesho.
2Acha watu wengine wakusifu,
kuliko mdomo wako wewe mwenyewe.
3Jiwe ni zito na mchanga kadhalika,
lakini usumbufu wa mpumbavu ni mzito zaidi.
4Ghadhabu ni katili na hasira huangamiza;
lakini ni nani awezaye kuukabili wivu?
5Afadhali mtu anayekuonya waziwazi,
kuliko yule afichaye upendo.
6Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu,
lakini busu la adui ni udanganyifu.
7Aliyeshiba hata asali huikataa,
lakini kwa mwenye njaa kila kichungu ni kitamu.
8Mtu aliyepotea mbali na kwake,
ni kama ndege aliyepotea mbali na kiota chake.
9Mafuta na manukato huufurahisha moyo,
lakini taabu hurarua roho.27:9 maana katika Kiebrania si dhahiri; Kigiriki kina: Taabu huikosesha roho raha.
10Usisahau rafiki zako wala wa baba yako.
Ukipatwa na janga usikimbilie kwa nduguyo;
afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.
11Uwe na hekima mwanangu upate kunifurahisha moyo,
nami sitakosa la kumjibu yeyote anayenilaumu.
12Mwenye busara huona hatari akajificha,
lakini mjinga hujitokeza mbele akaumia.
13Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni, chukua nguo yake;
mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.27:13 Taz 20:16.
14Amwamkiaye jirani kwa kelele alfajiri,
itaeleweka kwamba amemtakia laana.
15Mke mgomvi daima,
ni sawa na tonatona ya maji siku ya mvua.
16Kumzuia ni sawa na kuzuia upepo,
au kukamata mafuta kwa mkono.27:16 au … kwa mkono: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
17Chuma hunoa chuma,
kadhalika mtu hufundishwa na wenzake.
18Anayeutunza mtini hula tini,
anayemhudumia bwana wake ataheshimiwa.
19Kama uso ujionavyo wenyewe majini,
ndivyo ujijuavyo mwenyewe moyoni.
20Kuzimu na Uharibifu kamwe havishibi,
kadhalika na macho ya watu hayashibi.
21Ubora wa fedha au dhahabu hupimwa kwa moto,
na mtu hupimwa kutokana na sifa zake.
22Mtwange mpumbavu katika kinu pamoja na nafaka,
lakini hutafaulu kumtenganisha na upumbavu wake.
23Angalia vizuri hali ya mifugo yako;
tunza vizuri wanyama wako.
24Maana utajiri haudumu milele,
wala taji haidumu vizazi vyote.
25Baada ya kukata nyasi na kuzihifadhi,
kata majani toka milimani,
huku nyasi zinachipua upya.
26Kondoo watakupatia sufu kwa mavazi,
mbuzi nao utauza na kujinunulia mashamba;
27watakupa maziwa ya kukutosha wewe na jamaa yako,
na kwa ajili ya watumishi wako wa kike.

Methali27;1-27

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: