Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 23 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 24...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu

Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Sheria ni moja kuhusu sadaka ya kuondoa hatia na sadaka ya kuondoa dhambi: Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeichukua.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa ya mtu yeyote, atachukua ngozi ya mnyama aliyetolewa. Sadaka yoyote ya nafaka iliyookwa jikoni au katika sufuria au katika kikaango itakuwa mali ya kuhani anayeitoa.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au kavu, itakuwa ya wazawa wa Aroni, na wote wagawiwe kwa sawa.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

- 19 -
1Usiwaonee wivu watu waovu,
wala usitamani kuwa pamoja nao,
2maana fikira zao zote ni juu ya ukatili,
hamna jema lolote litokalo midomoni mwao.
- 20 -
3Nyumba hujengwa kwa hekima,
na kuimarishwa kwa busara.
4Kwa maarifa vyumba vyake hujazwa
vitu vya thamani na vya kupendeza.
- 21 -
5Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu,24:5 Kuwa … nguvu: Au Mwenye hekima anampita mwenye nguvu.
naam, maarifa ni bora kuliko nguvu.
6Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita,
na kwa washauri wengi ushindi hupatikana.
- 22 -
7Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa;
penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo.
- 23 -
8Afikiriaye kutenda maovu daima
ataitwa mtu mwenye fitina.
9Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi;
mwenye dharau huchukiwa na kila mtu.
- 24 -
10Ukifa moyo wakati wa shida,
basi wewe ni dhaifu kweli.
- 25 -
11Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure;
usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia.
12Usiseme baadaye: “Hatukujua!”
Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona;
yeye atakulipa kulingana na matendo yako!
- 26 -
13Mwanangu, ule asali maana ni nzuri;
sega la asali ni tamu mdomoni.
14Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako;
ukiipata utakuwa na matazamio mema,
wala tumaini lako halitakuwa la bure.
- 27 -
15Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema,
wala usijaribu kuiharibu nyumba yake,
16maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka,
lakini mtu mwovu huangamizwa na janga.
- 28 -
17Usishangilie kuanguka kwa adui yako;
usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake,
18maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa;
huenda akaacha kumwadhibu.
- 29 -
19Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya,
wala usiwaonee wivu watu waovu,
20maana mwovu hatakuwa na mema baadaye;
taa ya uhai wake itazimwa.
- 30 -
21Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme,
wala usishirikiane na wale wasio na msimamo,
22maana maangamizi yao huwapata ghafla.
Hakuna ajuaye maafa watakayozusha.24:22 Hakuna … watakayozusha: Au Hakuna ajuaye maafa yatakayosababishwa na Mungu au mfalme.
Misemo zaidi
23Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima:
Kupendelea watu katika hukumu si vizuri.
24Anayemwachilia mtu mwenye hatia,
hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa.
25Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha,
na baraka njema zitawajia.
26Jibu lililo la haki,
ni kama busu la rafiki.
27Kwanza fanya kazi zako nje,
tayarisha kila kitu shambani,
kisha jenga nyumba yako.
28Usishuhudie bure dhidi ya jirani yako,
wala usiseme uongo juu yake.
29Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda!
Ni lazima nilipize kisasi!”
30Nilipitia karibu na shamba la mvivu;
shamba la mzabibu la mtu mpumbavu.
31Nilishangaa kuona limemea miiba,
magugu yamefunika eneo lake lote,
na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32Nilitazama, nikawaza,
mwishowe nikapata funzo:
33 Taz Meth 6:10-11 Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo!
Kunja mikono yako tu upumzike!
34Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini,
umaskini utakuvamia kama mnyanganyi,
ufukara kama mtu mwenye silaha.


Methali24;1-34

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: