Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 3 July 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 10...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Naye akajibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kunipeleka majini wakati yanapotibuliwa. Kila nikijaribu kuingia, mtu mwingine hunitangulia.” Yesu akamwambia, “Inuka, chukua mkeka wako utembee.” Mara huyo mtu akapona, akachukua mkeka wake, akatembea. Jambo hili lilifanyika siku ya Sabato.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kwa hiyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia huyo mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali kubeba mkeka wako.” Lakini yeye akawaambia, “Yule mtu aliyeniponya ndiye aliyeniambia: ‘Chukua mkeka wako, utembee.’”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Nao wakamwuliza, “Huyo mtu aliyekuambia: ‘Chukua mkeka wako, utembee,’ ni nani?” Lakini yeye hakumjua huyo mtu aliyemponya, maana Yesu alikuwa amekwisha ondoka mahali hapo, kwani palikuwa na umati mkubwa wa watu. Basi, baadaye Yesu alimkuta huyo aliyeponywa hekaluni, akamwambia, “Sasa umepona; usitende dhambi tena, usije ukapatwa na jambo baya zaidi.” Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Methali za Solomoni
1Hizi ni methali za Solomoni:
Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake;
lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake.
2Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai,
lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni.
3Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa,
lakini huzipinga tamaa za waovu.
4Uvivu husababisha umaskini,
lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.
5Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno,
kulala wakati wa kuvuna ni aibu.
6Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
7Waadilifu hukumbukwa kwa baraka,
lakini waovu watasahaulika kabisa.
8Mwenye hekima moyoni hutii amri,
lakini mpumbavu aropokaye ataangamia.
9Aishiye kwa unyofu huishi salama,
apotoshaye maisha yake atagunduliwa.
10Akonyezaye kwa nia mbaya huzusha taabu,
lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani.
11Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
12 Taz Yak 5:20; 1Pet 4:8 Chuki huzusha ugomvi,
lakini upendo hufunika makosa yote.
13Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima,
lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.
14Wenye hekima huhifadhi maarifa,
lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.
15Mali ya tajiri ndio ngome yake,
umaskini wa maskini humletea maangamizi.
16Tuzo la mtu mwema ni uhai,
lakini mwovu huishia katika dhambi.
17Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,
lakini anayekataa kuonywa amepotoka.
18Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,
anayemsingizia mtu ni mpumbavu.
19Penye maneno mengi hapakosekani makosa,
lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.
20Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora;
akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.
21Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi,
lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.
22Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka,
juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.10:22 huzuni … nazo: Au na haongezi hapo huzuni.
23Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;
lakini watu wenye busara hufurahia hekima.
24Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,
lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.
25Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,
lakini mwadilifu huimarishwa milele.
26Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,
ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.
27Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,
lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.
28Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,
lakini tazamio la mwovu huishia patupu.
29Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,
lakini watendao maovu atawaangamiza.
30Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini,
lakini waovu hawatakaa katika nchi.
31Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima,
lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.
32Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika,
lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Methali10;1-32

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: