Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 3 June 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Yoel 2...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Niliwaleta katika nchi yenye rutuba, muyafurahie mazao yake na mema yake mengine. Lakini mlipofika tu mliichafua nchi yangu, mkaifanya chukizo nchi niliyowapa iwe yenu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza weweJehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’ Wataalamu wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Baali na kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Nzige: Onyo juu ya siku ya Mwenyezi-Mungu
1Pigeni tarumbeta huko Siyoni;
pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu!
Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda,
maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,
naam, siku hiyo iko karibu!
2Hiyo ni siku ya giza na huzuni;
siku ya mawingu na giza nene.
Jeshi kubwa la nzige linakaribia
kama giza linalotanda milimani.
Namna hiyo haijapata kuweko kamwe
wala haitaonekana tena
katika vizazi vyote vijavyo.
3Kama vile moto uteketezavyo
jeshi hilo laharibu kila kitu mbele yake
na kuacha nyuma kila kitu kinateketezwa;
kabla hawajapita, nchi ni kama bustani ya Edeni,
lakini wakisha pita, ni jangwa tupu.
Hakuna kiwezacho kuwaepa!
4 Taz Ufu 9:7-9 Wanaonekana kama farasi,
wanashambulia kama farasi wa vita,
5Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima,
wanarindima kama magari ya farasi,
wanavuma kama mabua makavu motoni.
Wamejipanga kama jeshi kubwa
tayari kabisa kufanya vita.
6Wakaribiapo, watu hujaa hofu,
nyuso zao zinawaiva.
7Wanashambulia kama mashujaa wa vita;
kuta wanazipanda kama wanajeshi.
Wote wanakwenda mbele moja kwa moja,
bila hata mmoja wao kubadilisha njia.
8Hakuna amsukumaye mwenziwe;
kila mmoja anafuata mkondo wake.
Wanapita kati ya vizuizi vya silaha,
wala hakuna kiwezacho kuwazuia.
9Wanauvamia mji,
wanapiga mbio ukutani;
wanaziparamia nyumba na kuingia,
wanapenya madirishani kama wezi.
10Nchi inatetemeka mbele yao,
mbingu zinatikisika.
Jua na mwezi vyatiwa giza,
nazo nyota zinaacha kuangaza.
11Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti;
askari wake ni wengi mno,
wanaomtii hawahesabiki.
2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana!
Nani atakayeweza kuistahimili?
Wito wa toba
12“Lakini hata sasa,”
nasema mimi Mwenyezi-Mungu,
“Nirudieni kwa moyo wote,
kwa kufunga, kulia na kuomboleza.
13Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni
bali nirudieni kwa moyo wa toba.”
Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu;
yeye amejaa neema na huruma;
hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili;
daima yu tayari kuacha kuadhibu.
14Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili nia
na kuwapeni baraka ya mazao,
mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
15Pigeni tarumbeta huko Siyoni!
Toeni amri watu wafunge;
itisheni mkutano wa kidini.
16Wakusanyeni watu wote,
wawekeni watu wakfu.
Waleteni wazee,
wakusanyeni watoto,
hata watoto wanyonyao.
Bwana arusi na bibi arusi
na watoke vyumbani mwao.
17Kati ya madhabahu na lango la hekalu,
makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu,
walie na kuomba wakisema:
“Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu.
Usiyaache mataifa mengine yatudharau
na kutudhihaki yakisema,
‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”
Mungu ataifanikisha nchi
18Ndipo Mwenyezi-Mungu akaipenda nchi yake
akawahurumia watu wake.
19Alisikiliza, akajibu sala zao; akasema,
“Sasa nitawapeni tena nafaka,
sitawafanya mdharauliwe tena na mataifa.
20Nitawaondoa hao adui watokao kaskazini,
nitawafukuza mpaka jangwani;
askari wa mbele nitawatupa katika Bahari ya Chumvi
na wale wa nyuma katika Bahari ya Mediteranea.
Watatoa uvundo na harufu mbaya,
hao ambao wamefanya maovu makubwa.
21“Usiogope, ewe nchi,
bali furahi na kushangilia,
maana Mwenyezi-Mungu ametenda makuu.
22Msiogope, enyi wanyama.
malisho ya nyikani yamekuwa mazuri,
miti inazaa matunda yake,
mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi.
23“Furahini, enyi watu wa Siyoni,
shangilieni kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,
maana amewapeni mvua za masika,2:23 mvua za masika: Au Mvua za masika kwa kuwa ni mwenye haki.
amewapeni mvua ya kutosha:
Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.
24Mahali pa kupuria patajaa nafaka,
mashinikizo yatafurika divai na mafuta.
25Nitawarudishia miaka ile iliyoliwa na nzige,
kila kitu kilicholiwa na tunutu, parare na matumatu,
hilo jeshi kubwa nililowaletea!
26Mtapata chakula kingi na kutosheka;
mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,
aliyewatendea mambo ya ajabu.
Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
27Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu,
enyi Waisraeli;
kwamba mimi Mwenyezi-Mungu,
ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine.
Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Siku ya Mwenyezi-Mungu
28katika Kiebrania sura ya 3 yaanza hapa.“Kisha hapo baadaye
nitaimimina roho yangu juu ya binadamu wote.
Watoto wenu wa kike na wa kiume watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono.
29Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike,
nitaimimina roho yangu wakati huo.
30“Nitatoa ishara mbinguni na duniani;
kutakuwa na damu, moto na minara ya moshi.
31Jua litatiwa giza,
na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,
kabla ya kufika siku ya Mwenyezi-Mungu,
siku iliyo kuu na ya kutisha.
32Hapo watu wote watakaoomba kwa jina la Mwenyezi-Mungu wataokolewa.
Maana katika mlima Siyoni na Yerusalemu,
watakuwako watu watakaosalimika,
kama nilivyosema mimi Mwenyezi-Mungu.

Yoeli2;1-32

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

No comments: