Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 16 June 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Amosi 8...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Muda mrefu ulikuwa umepita, na hata siku ya kufunga ilikuwa imekwisha pita. Sasa ilikuwa hatari sana kusafiri kwa meli. Basi, Paulo aliwapa onyo: “Waheshimiwa, nahisi kwamba safari hii itakuwa ya shida na hasara nyingi si kwa shehena na meli tu, bali pia kwa maisha yetu.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Lakini yule ofisa alivutiwa zaidi na maoni ya nahodha na ya mwenye meli kuliko yale aliyosema Paulo.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kwa kuwa bandari hiyo haikuwa mahali pazuri pa kukaa wakati wa baridi, wengi walipendelea kuendelea na safari, ikiwezekana mpaka Foinike. Foinike ni bandari ya Krete inayoelekea kusini-magharibi na kaskazini-magharibi; na huko wangeweza kukaa wakati wa baridi.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Maono ya nne: Kikapu cha matunda
1Bwana Mwenyezi-Mungu alinijalia maono mengine: Niliona kikapu kilichojaa matunda ya kiangazi. 2Naye Mwenyezi-Mungu akaniuliza: “Amosi, unaona nini?” Nami nikamjibu, “Naona kikapu cha matunda ya kiangazi.”8:2 Maneno “matunda ya kiangazi” na neno “mwisho” katika Kiebrania yanakaribiana sana kimatamshi. Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia:
“Mwisho umewafikia watu wangu wa Israeli.
Sitavumilia tena maovu yao.
3Siku hiyo, nyimbo za ikulu zitakuwa maombolezo.
Kutakuwa na maiti nyingi,
nazo zitatupwa nje kimyakimya.”8:3 nje kimyakimya: Au “nje. Kimya!”
Mungu ataiadhibu Israeli
4Sikilizeni enyi mnaowakandamiza wanyonge
na kuwaletea maangamizi fukara wa nchi.
5Mnajisemea mioyoni mwenu:
“Sikukuu ya mwezi mwandamo itakwisha lini
ili tuanze tena kuuza nafaka yetu?
Siku ya Sabato itakwisha lini
ili tupate kuuza ngano yetu?
Tutatumia vipimo hafifu vya wastani na uzito,
tutadanganya watu kwa mizani isizo sawa,
6hata kuuza ngano hafifu kwa bei kubwa.
Tutaweza kununua watu fukara kwa fedha,
na wahitaji kwa jozi ya kandambili.”
7Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa:
“Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.
8Kwa hiyo, dunia itatetemeka
na kila mtu nchini ataomboleza.
Nchi yote itayumbayumba;
itapanda na kushuka,
kama yanavyojaa na kupwa maji ya mto Nili!”
9Bwana Mwenyezi-Mungu asema,
“Siku hiyo nitalifanya jua litue adhuhuri,
na kuijaza nchi giza mchana.
10Sherehe zenu nitazigeuza kuwa kilio,
na nyimbo zenu za furaha kuwa maombolezo.
Nitawafanya nyote mvae magunia kwa huzuni
na kunyoa vipara vichwa vyenu,
kama kuomboleza kifo cha mtoto wa pekee;
na siku ya mwisho itakuwa ya uchungu mkubwa.”
11Bwana Mwenyezi-Mungu asema,
“Siku zaja ambapo nitaleta njaa nchini.
Lakini sio njaa na kiu ya chakula na maji,
bali njaa ya kusikia maneno ya Mwenyezi-Mungu.
12Watu watatangatanga kutoka bahari hata bahari,
kutoka upande wa kaskazini mpaka mashariki.
Watakimbia huko na huko wakitafuta neno la Mwenyezi-Mungu,
lakini hawatalipata.
13“Siku hiyo, hata vijana wenye afya,
wa kiume kwa wa kike,
watazimia kwa kiu.
14Wale wanaoapa kwa mungu wa uongo wa Samaria,
na kusema: ‘Kwa nafsi ya mungu wako ee Dani’;
na, ‘Kwa nafsi ya mungu wa Beer-sheba’,
wote wataanguka na hawatainuka tena kamwe.”

Amosi8;1-14

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

No comments: