Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 11 June 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Amosi 5...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Kijana msichana aweza kusahau mapambo yake au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau kwa muda wa siku zisizohesabika. Kweli wewe ni bingwa wa kutafuta wapenzi! Hata wanawake wabaya huwafundisha njia zako.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Nguo zako zina damu ya maskini wasio na hatia, japo hukuwakuta wakivunja nyumba yako. “Lakini licha ya hayo yote, wewe wasema: ‘Mimi sina hatia; hakika hasira yake imegeuka mbali nami.’ Lakini mimi nitakuhukumu kwa sababu unasema: ‘Sikutenda dhambi.’
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza weweJehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kwa nini unajirahisisha hivi, ukibadilibadili mwenendo wako? Utaaibishwa na Misri, kama ulivyoaibishwa na Ashuru. Na huko pia utatoka, mikono kichwani kwa aibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimewakataa wale uliowategemea, wala hutafanikiwa kwa msaada wao.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Maombolezo ya Amosi
1Sikilizeni maombolezo yangu juu yenu,
enyi Waisraeli:
2Umeanguka na hutainuka tena
ewe binti Israeli!
Umeachwa pweke nchini mwako,
hamna hata mtu wa kukuinua.
3Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupigana
lakini watarejea 100 tu;
wataondoka watu 100 wa kijiji kimoja
lakini watanusurika watu kumi tu.”
4Mwenyezi-Mungu awaambia hivi Waisraeli:
“Nitafuteni mimi nanyi mtaishi!
5Lakini msinitafute huko Betheli
wala msiende Gilgali
wala msivuke kwenda Beer-sheba.
Maana wakazi wa Gilgali,
hakika watachukuliwa uhamishoni,
na Betheli utaangamizwa!”
6Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi!
La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto;
moto utawateketeza wakazi wa Betheli
na hakuna mtu atakayeweza kuuzima.
7Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu,
na kuuona uadilifu kuwa kama takataka!
8Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni,
ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana,
na mchana kuwa usiku;
yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari
na kuyamwaga juu ya nchi kavu,
Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.
9Yeye ndiye anayewaangamiza wenye nguvu,
na kuziharibu ngome zao.
10Nyinyi huwachukia watetezi wa haki
na wenye kusema ukweli mahakamani.
11Nyinyi mnawakandamiza fukara
na kuwatoza kodi ya ngano kupita kiasi.
Mnajijengea nyumba za mawe ya kuchonga,
lakini nyinyi hamtaishi humo;
mnalima bustani nzuri za mizabibu,
lakini hamtakunywa divai yake.
12Maana mimi najua wingi wa makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu;
nyinyi mnawatesa watu wema,
mnapokea rushwa
na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.
13Basi, kutakuwa na wakati mbaya
ambao hata mwenye busara atanyamaza.
14Tafuteni kutenda mema na si mabaya,
ili nyinyi mpate kuishi
naye Mwenyezi-Mungu wa majeshi
awe pamoja nanyi kama mnavyosema.
15Chukieni uovu, pendeni wema,
na kudumisha haki mahakamani.
Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.
16Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi,
naam, Mwenyezi-Mungu asema:
“Patakuwa na kilio kila mahali mitaani;
watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’
Wakulima wataitwa waje kuomboleza,
na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.
17Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu;
maana nitapita kati yenu kuwaadhibu.
Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.”
Siku ya Mwenyezi-Mungu
18Ole wenu nyinyi mnaoingojea kwa hamu
siku ya Mwenyezi-Mungu!
Kwa nini mnaitaka sana siku hiyo?
Siku hiyo, itakuwa siku ya giza na sio ya mwanga!
19Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba,
halafu akakumbana na dubu!
Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake,
akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
20Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;
itakuwa huzuni bila uangavu wowote.
21Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nazichukia na kuzidharau sikukuu zenu;
siifurahii mikutano yenu ya kidini.
22Mjaponitolea sadaka zenu za kuteketezwa na za nafaka,
mimi sitakubali kuzipokea;
na sadaka zenu za amani za wanyama wanono
mimi sitaziangalia kabisa.
23Ondoeni mbele yangu kelele za nyimbo zenu!
Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!
24Lakini acheni haki itiririke kama maji,
uadilifu uwe kama mto usiokauka.
25“Enyi Waisraeli, wakati ule mlipokuwa kule jangwani kwa miaka arubaini, je, mliniletea tambiko na sadaka hata mara moja? 26Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe? 27Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi.

Amosi5;1-27

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

No comments: