Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 16 March 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Ezekieli 19...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki/nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...


Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu

Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

Ndugu, nyinyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure. Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....

Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote. Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Maana kama mjuavyo, sisi hatukutumia maneno ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi! Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote,
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimamie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.


Maombolezo
1Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli:
2Mama yenu alikuwa simba wa fahari
miongoni mwa simba wengine.
Alikaa kati ya simba vijana,
akawalisha watoto wake.
3Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake,
mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari.
Akajifunza kwa mama yake kuwinda,
akawa simba mla watu.
4Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake,
wakamnasa katika mtego wao,
wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.
5Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja,
matumaini ya kumpata yamekwisha,
alimchukua mtoto wake mwingine,
akamfanya simba kijana hodari.
6Huyo alipokuwa amekua,
akaanza kuzurura na simba wengine.
Naye pia akajifunza kuwinda,
akawa simba mla watu.
7Aliziandama ngome za watu
na kuiharibu miji yao.
Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake,
kwa sauti ya kunguruma kwake.
8Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote,
wakatandaza wavu wao juu yake,
naye akanaswa katika mtego wao.
9Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao,
wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni.
Huko, wakamtia gerezani,
ili ngurumo yake isisikike tena
juu ya milima ya Israeli.
10Mama yako alikuwa kama mzabibu shambani,
uliopandikizwa kando ya maji,
ambao ulizaa sana kwa kuwa na maji tele.
11Ulikuwa na matawi yenye nguvu,
ambayo yalikuwa fimbo za kifalme.
Mzabibu huo ulikua kupita miti mingine,
watu waliusifu ukubwa wa shina lake
na wingi wa matawi yake.
12Lakini ulingolewa kwa hasira
ukatupwa chini ardhini;
upepo wa mashariki ukaukausha,
matunda yake yakapukutika;
matawi yake yenye nguvu yalikaushwa,
nao moto ukauteketeza.
13Na sasa umepandikizwa jangwani,
katika nchi kame isiyo na maji.
14Lakini moto umetoka kwenye shina lake,
umeyateketeza matawi na matunda yake.
Matawi yake kamwe hayatakuwa na nguvu,
wala hayatakuwa fimbo za kifalme.
Huo umekuwa wimbo wa maombolezo; ndivyo unavyoimbwa daima.



Ezekieli19;1-14

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: