Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 12 March 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Ezekieli 17...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda. Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe,” wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji nyinyi.” Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Mfano wa tai na mzabibu
1Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: 2“Wewe mtu! Tega kitendawili, uwaambie fumbo Waisraeli. 3Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Kulikuwa na tai mmoja mkubwa sana
aliyekuwa na mabawa makubwa,
yenye manyoya marefu mengi
yenye rangi za kila aina.
Tai huyo aliruka mpaka mlimani Lebanoni,
akatua juu ya kilele cha mwerezi;
4akakwanyua tawi lake la juu zaidi,
akalipeleka katika nchi ya wafanyabiashara,
akaliweka katika mji wao mmoja.
5Kisha akachukua mmea mchanga nchini Israeli,
akaupanda katika ardhi yenye rutuba
ambako kulikuwa na maji mengi.
6Mmea ukakua ukawa mzabibu
wa aina ya mti utambaao;
matawi yake yakamwelekea,
na mizizi yake ikatanda chini yake.
Mzabibu ukachipua matawi na majani mengi.
7Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa;
alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi.
Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake,
ukamwelekezea matawi yake,
ili aumwagilie maji.
8Mzabibu ulikuwa umetolewa kitaluni mwake
ukapandikizwa penye udongo mzuri na maji mengi,
ili upate kutoa matawi na kuzaa matunda
uweze kuwa mzabibu mzuri sana!
9Sasa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nakuuliza:
Je, mzabibu huo utaweza kustawi?
Je, hawatangoa mizizi yake
na kuozesha matunda yake
na matawi yake machanga kuyanyausha?
Hakutahitajika mtu mwenye nguvu au jeshi
kuungoa kutoka humo ardhini.
10Umepandikizwa, lakini, je, utastawi?
Upepo wa mashariki uvumapo juu yake utanyauka;
utanyauka papo hapo kwenye kuta ulikoota.”
Maelezo yake
11Kisha neno la Mwenyezi-Mungu likanijia: 12“Sasa waulize hao watu waasi kama wanaelewa maana ya mfano huo. Waambie kuwa, mfalme wa Babuloni alikuja Yerusalemu, akamwondoa mfalme na viongozi wake, akawapeleka Babuloni. 13Kisha akamtawaza mmoja wa jamaa ya kifalme, akafanya naye mapatano, akamwapisha. Aliwaondoa humo nchini watu mashujaa akawapeleka mbali 14ili utawala huo uwe dhaifu na uzingatie agano lake mfalme wa Babuloni. 15Lakini yule mfalme mpya alimwasi mfalme wa Babuloni kwa kuwatuma wajumbe Misri kuomba farasi na askari wengi. Je, mfalme huyo atafaulu? Je, anayefanya hivyo na kuvunja agano lake ataweza kuepa adhabu?
16“Mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, kama niishivyo, mfalme huyu atafia katika nchi ya Babuloni, nchi ya mfalme yule aliyemweka awe mfalme, na ambaye amedharau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye. 17Hakika, Farao pamoja na jeshi lake kubwa hataweza kumsaidia vitani wakati Wababuloni watakapomzungushia ngome na kuta ili kuwaua watu wengi. 18Kwa kuwa alikidharau kile kiapo na kuvunja lile agano ambalo aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na kufanya mambo haya yote, hakika hataokoka.
19“Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema, kama niishivyo, kwa vile amekidharau kiapo alichoapa kwa jina langu na agano langu akalivunja, hakika nitamwadhibu vikali. 20Nitatandaza wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu; nitampeleka mpaka Babuloni na kumhukumu kwa sababu ya uhaini alioufanya dhidi yangu. 21Majeshi yake hodari yatauawa kwa upanga na watakaosalia hai watatawanyika pande zote. Hapo mtatambua kuwa mimi, naam, mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Ahadi ya Mungu ya tumaini
22Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi mwenyewe nitachukua kisehemu cha ncha ya juu ya mwerezi, naam, nitavunja tawi changa kutoka matawi yake ya juu na kulipanda juu ya mlima mrefu sana. 23Naam, nitalipanda juu ya mlima mrefu wa Israeli ili lichanue na kuzaa matunda. Litakuwa mwerezi mzuri, na ndege wa aina zote watakaa chini yake pia watajenga viota vyao katika matawi yake.17:23 Kigiriki: Lakini maneno na wanyama wa kila aina watakaa chini yake. 24Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”


Ezekieli17;1-24

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: