Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 17 December 2019

Kikombe Cha Asubuhi; Yeremia 12....


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetuUtukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

“Na sasa basi, ninawaweka nyinyi chini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga na kuwawezesha mzipate zile baraka alizowawekea watu wake. Mimi sikutamani hata mara moja fedha, wala dhahabu, wala nguo za mtu yeyote.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Mnajua nyinyi wenyewe kwamba nimefanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na ya wenzangu. Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza weweJehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Baada ya kusema hayo, Paulo alipiga magoti pamoja nao wote, akasali. Wote walikuwa wanalia, na kumwaga kwa kumkumbatia na kumbusu. Jambo lililowahuzunisha zaidi lilikuwa neno alilosema kwamba hawangemwona tena. Basi, wakamsindikiza hadi melini.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.


Yeremia anamhoji Mwenyezi-Mungu
1Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu,
ingawa nakulalamikia.
Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako:
Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao?
Mbona wote wenye hila hustawi?
2Unawaotesha nao wanaota;
wanakua na kuzaa matunda.
Wanakutaja kwa maneno yao,
lakini mioyo yao iko mbali nawe.
3Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua;
wayathibiti maelekeo yangu kwako.
Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa,
watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
4Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame,
na nyasi za mashamba yote kunyauka?
Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake;
wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”12:4 Kiebrania: Mwisho wetu; baadhi ya tafsiri nyingine: Yale tunayofanya.
5Mwenyezi-Mungu asema,
“Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka,
utawezaje kushindana na farasi?
Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi,
utafanyaje katika msitu wa Yordani?
6Hata ndugu zako, jamaa yako mwenyewe,
nao pia wamekutendea mambo ya hila;
wanakukemea waziwazi.
Usiwaamini hata kidogo,
japo wanakuambia maneno mazuri.”
Mungu anaiacha nyumba yake na watu wake
7Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Nimeiacha nyumba yangu;
nimeitupa mali yangu mimi mwenyewe.
Israeli, mpenzi wangu wa moyo,
nimemtia mikononi mwa maadui zake.
8Wateule wangu wamenigeuka,
wamekuwa kama simba porini,
wameningurumia mimi;
ndiyo maana nawachukia.
9Wateule wangu wamekuwa ndege mzuri
wanaoshambuliwa na kozi pande zote.
Nenda ukawakusanye wanyama wote wakali
waje kushiriki katika karamu.
10Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu,
wamelikanyagakanyaga chini lililo mali yangu;
shamba langu zuri wamelifanya jangwa.
11Wamelifanya kuwa tupu;
katika ukiwa wake lanililia.
Nchi yote imekuwa jangwa,
wala hakuna mtu anayejali.
12Juu ya milima yote jangwani,
watu wamefika kuangamiza.
Upanga wangu unapita kuiangamiza nchi,
toka upande mmoja hadi mwingine,
wala hakuna mtu atakayeishi kwa amani.
13Walipanda ngano, lakini walivuna magugu;
walifanya bidii, lakini hawakupata kitu.
Kwa sababu ya hasira yangu kali,
mavuno watakayoyapata yatakuwa aibu tupu.”
Mungu na majirani wa Israeli
14Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya jirani wabaya wa watu wangu: “Wamekigusa kile kilicho changu, kile nilichowapa watu wangu Israeli! Basi nitawangoa kutoka katika nchi yao. Hata watu wa Yuda nitawangoa katika nchi yao. 15Lakini baada ya kuwangoa, nitawahurumia tena; nitalirudisha kila taifa katika sehemu yake na katika nchi yake. 16Na kama watajifunza njia za watu wangu kwa moyo wote, kama wataapa kwa jina langu kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu,’ kama vile walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa jina la mungu Baali, basi watajengeka miongoni mwa watu wangu. 17Lakini taifa lolote ambalo halitanitii, nitalingoa kabisa na kuliangamiza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”Yeremia12;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: