Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 9 April 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 99...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Kwa amri yake vyote huzunguka huku na huko, kutekeleza kila kitu anachokiamuru, kufanyika katika ulimwengu wa viumbe. Mungu hutekeleza matakwa yake duniani; iwe ni kwa ajili ya kuwaadhibu watu, au kwa ajili ya kuonesha upendo wake.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

“Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Je, wajua jinsi Mungu anavyovipa amri yake, na kufanya umeme wa mawingu yake ungae? Je, wajua jinsi mawingu yanavyoelea angani? Ndizo kazi za ajabu za yule aliye mkamilifu wa maarifa!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Wewe wajiona umevaa nguo za joto sana, wakati upepo wa kusi unaivamia nchi. Je, waweza, kuzitandaza mbingu kama yeye zikawa ngumu kama kioo cha shaba? Tufundishe tutakachomwambia Mungu; maana hoja zetu si wazi, tumo gizani. Je, nani anathubutu kumwambia: Nataka kuongea? Nani aseme apate balaa? “Ghafla mtu hawezi tena kuona waziwazi: Jua limefichika nyuma ya mawingu, na upepo umefagia anga! Mngao mzuri hutokea kaskazini; Mungu amezungukwa na utukufu wa kutisha. Mungu Mwenye Nguvu asiyeweza kufikiwa na mtu, uwezo na uadilifu wake ni mkuu, amejaa wema wala hapotoshi haki kamwe. Kwa hiyo, watu wote humwogopa; yeye hamjali mtu yeyote mwenye kiburi.”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Mungu mtawala mkuu
1Mwenyezi-Mungu anatawala,
mataifa yanatetemeka!
Ameketi juu ya viumbe vyenye mabawa,99:1 viumbe vyenye mabawa: Taz. maelezo ya Mwa. 3:24
nayo dunia inatikisika!
2Mwenyezi-Mungu ni mkuu katika Siyoni;
ametukuka juu ya mataifa yote.
3Wote na walisifu jina lake kuu la kutisha.
Mtakatifu ndiye yeye!
4Ee mfalme mkuu, mpenda uadilifu!
Umethibitisha haki katika Israeli;
umeleta uadilifu na haki.
5Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu;
angukeni kifudifudi mbele zake.
Mtakatifu ndiye yeye!
6Mose na Aroni walikuwa makuhani wake;
Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia.
Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza.
7Alisema nao katika mnara wa wingu;
waliyazingatia matakwa yake na amri alizowapa.
8Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wewe uliwasikiliza;
kwao ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliwaadhibu kwa makosa yao.
9Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu;
abuduni katika mlima wake mtakatifu!99:9 mlima wake mtakatifu: Taz Zab 2:6.
Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu.


Zaburi99;1-9

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: