Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 2 April 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 94...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Maana Waisraeli na watu wa Yuda hawakufanya chochote mbele yangu isipokuwa uovu tangu ujana wao; watu wa Israeli hawakufanya chochote isipokuwa kunikasirisha kwa matendo yao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mji huu umechochea hasira yangu na kuniudhi tangu siku ulipojengwa mpaka leo hii. Kwa hiyo, nitautoa kabisa mbele yangu,
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

kwa sababu ya uovu wote waliotenda watu wa Israeli na watu wa Yuda, pamoja na wafalme na viongozi wao, makuhani na manabii wao, na wakazi wa Yerusalemu. Wao walinipa kisogo badala ya kunigeuzia nyuso zao; ingawa nimewafundisha tena na tena, wao hawakusikiliza na kuyapokea mafundisho yangu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Waliweka sanamu za miungu yao ya kuchukiza katika nyumba hii inayojulikana kwa jina langu, wakaitia unajisi. Walimjengea mungu Baali madhabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, ili wamtolee mungu Moleki wavulana wao na binti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo, wakawafanya watu wa Yuda watende dhambi.”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.
Mungu hakimu wa wote
1Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwenye kulipiza kisasi,
ewe Mungu mlipiza kisasi, ujitokeze!
2Usimame, ee hakimu wa watu wote;
uwaadhibu wenye kiburi wanavyostahili!
3Waovu wataona fahari hata lini?
Watajisifia mpaka lini, ee Mwenyezi-Mungu?
4Hata lini waovu watajigamba kwa maneno?
Waovu wote watajivuna mpaka lini?
5Wanawaangamiza watu wako, ee Mwenyezi-Mungu,
wanawakandamiza hao walio mali yako.
6Wanawaua wajane na wageni;
wanawachinja yatima!
7Wanasema: “Mwenyezi-Mungu haoni,
Mungu wa Yakobo hajui!”
8Enyi wajinga wa mwisho, fikirini kidogo!
Enyi wapumbavu, mtapata lini maarifa?
9Aliyefanya sikio, je, hawezi kusikia?
Aliyeumba jicho, je, hawezi kuona?
10Mwenye kutawala mataifa, je, hawezi kuadhibu?
Mkufunzi wa wanadamu, je, hana maarifa?
11 Taz 1Kor 3:20 Mwenyezi-Mungu ayajua mawazo ya watu;
anajua kwamba hayafai kitu.
12Heri mtu unayemfunza nidhamu, ee Mwenyezi-Mungu,
mtu unayemfundisha sheria yako,
13ili siku ya taabu apate utulivu,
hadi waovu wachimbiwe shimo.
14Mwenyezi-Mungu hatawaacha watu wake;
hatawatupa hao walio mali yake.
15Maana hukumu zitatolewa kwa haki tena,
na wanyofu wote wa moyo wataizingatia.
16Nani aliyenisaidia kumpinga mtu mwovu?
Nani aliyekuwa upande wangu dhidi ya wabaya?
17Mwenyezi-Mungu asingalinisaidia,
ningalikwisha kwenda kwenye nchi ya wafu.94:17 nchi ya wafu: Au nchi ya kimya.
18Nilipohisi kwamba ninateleza,
fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, zilinitegemeza.
19Mahangaiko ya moyo wangu yanapozidi,
wewe wanifariji na kunifurahisha.
20Wewe huwezi kushirikiana na mahakimu dhalimu,
wanaotunga kanuni za kutetea maovu.
21Wao wanaafikiana kuwaangamiza waadilifu,
na kuwahukumu watu wasio na hatia wauawe.
22Lakini Mwenyezi-Mungu ni ngome yangu;
Mungu wangu ni mwamba wa usalama wangu.
23Uovu wao atawarudishia wao wenyewe,
atawafutilia mbali kwa sababu ya ubaya wao.
Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, atawafutilia mbali!



Zaburi94;1-23

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: