Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 26 April 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 112...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumba zitakavyodumu milele kwa uwezo wangu, ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Sala katika taabu
(Sala ya mtu aliye katika shida na ambaye anamwekea Mwenyezi-Mungu malalamiko yake)
1Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu,
na kilio changu kikufikie.
2Usijifiche mbali nami wakati wa taabu!
Unitegee sikio lako,
unijibu upesi wakati ninapokuomba!
3Siku zangu zapita kama moshi;
mifupa yangu yaungua kama katika tanuri.
4Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka;
sina hata hamu ya chakula.
5Kutokana na kusononeka kwangu,
nimebaki mifupa na ngozi.
6Nimekuwa kama ndege wa jangwani;
kama bundi kwenye mahame.
7Ninalala macho wazi,
kama ndege mkiwa juu ya paa.
8Mchana kutwa maadui zangu wananisimanga,
wanaonidhihaki hutumia jina langu kulaania.
9Majivu yamekuwa chakula changu,
machozi nayachanganya na kinywaji changu,
10kwa sababu ya ghadhabu na hasira yako,
maana umeniokota na kunitupilia mbali.
11Maisha yangu ni kama kivuli cha jioni;
ninanyauka kama nyasi.
12Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, watawala milele;
jina lako lakumbukwa vizazi vyote.
13Wewe utainuka na kuurehemu mji wa Siyoni;
maana wakati umefika wa kuutendea mema;
wakati wake uliopangwa umefika.
14Watumishi wako wanauthamini sana,
ujapokuwa magofu sasa;
wanauonea huruma,
ingawa umeharibika kabisa.
15Mataifa yataliheshimu jina la Mwenyezi-Mungu;
wafalme wote duniani wataogopa utukufu wake.
16Mwenyezi-Mungu ataijenga upya Siyoni,
na kuonekana alivyo mtukufu.
17Ataikubali sala ya fukara;
wala hatayakataa maombi yao.
18Andika jambo hili kwa ajili ya vizazi vijavyo;
watakaozaliwa baadaye wamsifu Mwenyezi-Mungu.
19Kwamba aliangalia chini kutoka patakatifu pake juu,
Mwenyezi-Mungu aliangalia dunia kutoka mbinguni,
20akasikia lalamiko la wafungwa;
akawaachilia huru waliohukumiwa kuuawa.
21Hivyo watu watatangaza jina la Mwenyezi-Mungu huko Siyoni;
sifa zake zitatangazwa huko Yerusalemu,
22wakati mataifa yatakapokusanyika pamoja
na falme zitakutana kumwabudu Mwenyezi-Mungu.
23Mungu amenipunguzia nguvu ningali kijana;
ameyafupisha maisha yangu.
24Ee Mungu wangu, usinichukue sasa
wakati ningali bado kijana.
Ee Mwenyezi-Mungu wewe wadumu milele.
25 Taz Ebr 1:10-12 Wewe uliiumba dunia zamani za kale,
mbingu ni kazi ya mikono yako.
26Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki;
hizo zitachakaa kama vazi.
Utazitupilia mbali kama nguo,
nazo zitapotelea mbali.
27Lakini wewe ni yuleyule daima,
na maisha yako hayana mwisho.
28Watoto wa watumishi wako watakaa salama;
wazawa wao wataimarishwa mbele yako.



Zaburi112-;1-28

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: