Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 8 April 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 98...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah ni siku/wiki  nyingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!

“Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka, na kuruka kutoka mahali pake. Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu, na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake. Huufanya uenee chini ya mbingu yote, umeme wake huueneza pembe zote za dunia. Ndipo sauti yake hunguruma, sauti ya Mungu hunguruma kwa fahari na muda huo wote umeme humulikamulika.
Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

Mungu hupiga radi ya ajabu kwa sauti yake, hufanya mambo makuu tusiyoweza kuyaelewa. Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’ Na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’ Hufunga shughuli za kila mtu; ili watu wote watambue kazi yake.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Wanyama wa porini hurudi mafichoni mwao, na hubaki katika mapango yao. Dhoruba huvuma kutoka chumba chake, na baridi kali kutoka ghalani mwake. Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea, uso wa maji huganda kwa haraka. Mungu hulijaza wingu manyunyu mazito; mawingu husambaza umeme wake.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

Mungu mtawala wa dunia yote
1Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu!
Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi.
2Mwenyezi-Mungu ameonesha ushindi wake;
ameyadhihirishia mataifa uwezo wake wa kuokoa.
3Amekumbuka fadhili na uaminifu wake kwa Waisraeli.
Pande zote za dunia zimeuona ushindi wa Mungu wetu.
4Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu;
imsifu kwa nyimbo na vigelegele.
5Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa shangwe,
msifuni kwa sauti tamu za zeze.
6Mpigieni vigelegele Mwenyezi-Mungu mfalme wetu,
mshangilieni kwa tarumbeta na sauti ya baragumu.
7Bahari na ivume na vyote vilivyomo;
dunia na wote waishio ndani yake.
8Enyi mito pigeni makofi;
enyi vilima imbeni pamoja kwa shangwe.
9Shangilieni mbele ya Mwenyezi-Mungu,
maana anakuja kutawala dunia.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
atawatawala watu kwa uadilifu.


Zaburi98;1-9

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: