Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 15 April 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Ezekieli 41...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako,
Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
 ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea

Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

“Sikiliza! Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki.” Mimi Yohane, niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuona, nikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliyenionesha mambo hayo, nikataka kumwabudu.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Lakini yeye akaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!” Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...

Nawapenda.

1Kisha, yule mtu akanipeleka kwenye ukumbi wa ndani, mahali patakatifu. Akaipima nafasi iliyoelekea humo ndani, nayo ilikuwa na kina cha mita 3,41:1 makala ya Kiebrania ina maneno mawili zaidi ambayo maana yake si dhahiri. 2na upana wa mita 5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita 2.5. Akaupima ukumbi wenyewe, nao ulikuwa na urefu wa mita 20 na upana mita 10.
3Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha mita 1 na upana mita 3.5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita tatu u nusu.41:3 na kuta … na nusu: Makala ya Kiebrania: Na unene wa mita tatu na nusu. 4Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha mraba pande zake zikiwa na upana wa mita 10. Chumba hiki kilikuwa mbele ya ukumbi wa katikati. Kisha, akaniambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu kabisa.”
Vyumba vilivyojengwa mkabala na kuta za hekalu
5Yule mtu aliupima unene wa ukuta wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nao ulikuwa mita tatu. Kulikuwa na mfululizo wa vyumba vidogovidogo kuizunguka nyumba ya Mwenyezi-Mungu, vyenye upana wa mita mbili. 6Vyumba hivi, vilikuwa katika majengo ya ghorofa tatu, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Ukuta wa nje wa hekalu kila kwenye ghorofa ulikuwa mwembamba kuliko ule wa ghorofa ya chini, ili vile vyumba viwe imara bila ya kuutegemea ukuta wa hekalu. 7Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea nje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini hadi juu. Mkabala na ukuta wa nje wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya vyumba, kulikuwa na ngazi mbili, ambazo zilifanya iwe rahisi kwenda juu kutokea ghorofa ya chini hadi ile ya juu.41:7 maana ya aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
8Kisha, nikaona kuwa hekalu lilikuwa na sakafu iliyonyanyuliwa kulizunguka, nayo ilikuwa ndio msingi wa zile ghorofa tatu mkabala na hekalu, kimo cha msingi wa ghorofa hizo ulikuwa sawa na ule ufito wa kupimia, mita tatu. 9Unene wa ukuta wa nje wa vyumba vya ndani ulikuwa mita mbili u nusu. Nafasi wazi kati ya vyumba vya pembeni mkabala na hekalu 10na vyumba vya walinzi vilikuwa na upana wa mita 10, kuzunguka hekalu. 11Kulikuwa na milango kwenye vyumba vya pembeni kutokea kwenye uwanja, mmoja upande wa kaskazini na mwingine upande wa kusini. Na msingi uliounganishwa na uwanja ulikuwa na upana wa mita 2.5.
Jengo la upande wa Magharibi
12Mwishoni kabisa mwa uwanja, upande wa magharibi kulikuwa na jengo lenye urefu wa mita 45 na upana wa mita 35. Kuta zake zilikuwa na unene wa mita 2.5.
Jumla ya vipimo vya jengo la hekalu
13Yule mtu akapima upande wa nje wa hekalu nao ulikuwa na urefu wa mita 50. Tokea nyuma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kupitia ile nafasi ya kupitia, hadi mwisho wake, upande wa magharibi, umbali wake ulikuwa pia mita 50. 14Urefu mbele ya hekalu tangu upande huu hadi upande huu ukichanganya na ile nafasi wazi, ulikuwa pia mita 50. 15Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50.
Maelezo juu ya jengo la hekalu
Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa, 16vyote vilipambwa kwa mbao tangu sakafuni hadi kwenye madirisha. Madirisha haya yangeweza kufunikwa.41:16 makala ya Kiebrania si dhahiri. 17Mpaka kwenye nafasi juu ya mlango hata kwenye chumba cha ndani na nje yake, pia juu ya kuta ndani ya chumba cha ndani na kwenye ukumbi palikuwapo na michoro iliyofanana na 18mitende na picha za viumbe wenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote. Kila kiumbe alikuwa na nyuso mbili: 19Uso wa mwanadamu ulioelekea kwenye mtende upande mmoja na uso wa simba ulioelekea kwenye mtende wa upande mwingine. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwenye nyumba nzima, 20tangu sakafu hadi juu ya milango palichorwa viumbe wenye mabawa na mitende. 21Miimo ya mahali patakatifu ilikuwa ya mraba.
Madhabahu ya mbao
Mbele ya mlango wa kuingilia mahali patakatifu kabisa kulikuwa na kitu kilichoonekana kama 22madhabahu ya mbao. Kimo chake kilikuwa nusu mita na upana wa mita moja. Pembe zake, tako lake,41:22 tako: Makala ya Kiebrania: Urefu. na pande zake zote zilikuwa zimetengenezwa kwa mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ndiyo meza inayokaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Milango
23Kulikuwako na mlango wa tarabe wa kuingia kwenye ukumbi wa hekalu na mlango wa tarabe wa kuingia mahali patakatifu kabisa. 24Milango hiyo ilikuwa ya tarabe, kwa hiyo kila mlango uliweza kufunguka katikati.
25Kwenye mlango wa kuingilia ukumbi kulichorwa viumbe vyenye mabawa na mitende, kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa na kifuniko cha ubao kikifunika mlango kwa nje kwenye sehemu ya kuingilia ndani. 26Pembeni mwa chumba hiki, kulikuwa na madirisha madogo na kuta zilipambwa kwa michoro ya mitende.

Ezekieli41;1-26

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)


"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: